Waziri Jerry Slaa: Mimi siyo Mtoto wa Maskini, baba yangu alikuwa Rubani. Nimekataa Rushwa ya Milioni 300

Waziri Jerry Slaa: Mimi siyo Mtoto wa Maskini, baba yangu alikuwa Rubani. Nimekataa Rushwa ya Milioni 300

“Imeandikwa, ‘Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.’”— Mathayo 4:4



Ayubu 21:23,24,30,31,32.



23. Baadhi ya watu hukaa na afya njema mpaka siku ya kufa; wanakufa wakiwa na furaha na raha, miili yao ikiwa na lishe nzuri. [Ili upate lishe bora, lazima uweze kumudu gharama za kununua chakula chote ambacho soko linaweza kukuuzia au uwe na bustani ya nyuma ya nyumba yako ambayo inatunzwa vizuri]



24. Wengine hawana furaha hata kidogo; wanaishi na kufa wakiwa na mioyo yenye uchungu.[ Inasikitisha lakini ni ukweli usiopingika katika maisha]



30. Siku Mungu anapokasirika na kuadhibu, waovu ndio wanaoachwa daima. [Jiulize kwa nini? Jibu linaweza kupatikana katika Luka 16:19-31]



31. Hakuna wa kuwashitaki waovu wala kuwalipa kwa yote waliyoyatenda. [Hata kama kulikuwa na mtu wa kuwashtaki, sheria haitakuruhusu kufanya hivyo, watapata njia ya kutokea kwa njia za rushwa?!]



32. Wanapopelekwa makaburini, kwenye makaburi yao yaliyohifadhiwa vizuri, maelfu hujiunga na msafara wa mazishi, na hata ardhi inalala kwa upole juu ya miili yao. [Kila mtu angependa kuhudhuria mazishi ya watu maarufu ili tu kushuhudia maonyesho maridadi ya siku yao ya mwisho]



*** Hili si shambulio kwa watu wenye ukwasi bali aya hizi zilizochaguliwa zitatoa tafakari ya kibinafsi juu ya na jinsi tunavyoupata huo utajiri. Ningependa tutafakari maswali haya machache; majibu ambayo natumaini yatakubadilisha kuwa mtu bora kwako na kwa jamii inayokuzunguka.



1. Ni nani anayechukua nafasi ya kwanza katika harakati zako za kutafuta utajiri?



2. Ulitumia njia gani kupata mali?



3. Umetumiaje mali yako kufanya amani na wale wanaokuzunguka?
 
Waziri wa Ardhi mh Jerry Slaa amesema kuna Wanasiasa wanaona Sifa kujiita Watoto wa Maskini Lakini yeye siyo Maskini baba yake alikuwa Rubani na hadi leo anakula hela ya Urithi.

Mh Slaa ametuma salamu kwa mafisadi wote kwamba yeye hana Njaa na hapokei Rushwa kwa sababu Biblia imesema mla Rushwa ni kipofu.

Waziri amekataa Rushwa ya tsh 300 milioni kutoka kwa tajiri Mmoja aliyejenga kituo cha Mafuta Kinyume cha utaratibu pale Mikocheni.

I wish you a Merry Christmas 😀

======

Dar es Salaam

“Nimekataa Rushwa ya Tsh. Milioni 300”- Waziri wa Ardhi Mhe . Jerry Silaa

Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Jerry Silaa, ametangaza kusitisha matumizi ya kituo cha mafuta cha Barrel kilichopo Mikocheni, mkoani Dar es Salaam, kutokana na kituo hicho kujengwa bila kufuata utaratibu wa Wizara hiyo.

Mhe. Silaa amesema hayo alipotembelea eneo hilo, kilipojengwa kituo hicho, ambapo amebainisha kuwa, kuna watu walimfuata wakitaka kumpa rushwa ya Tsh. Mil. 300/= ambazo amedai amezikataa huku akibainisha kuwa ukichukua rushwa kila kitu utaona kipo sahihi.

Waziri huyo pia amewaagiza Wakuu wa Idara wa Ardhi na Mipango Miji nchi nzima kufanya uhakiki wa vituo vya mafuta vilivyo kwenye maeneo yao, kwa kuangalia matumizi yake pamoja na mchakato uliotumika kupatikana kwa viwanja hivyo
View attachment 2851260
Tapeli huyu
 
Back
Top Bottom