Waziri Jerry Slaa: Mimi siyo Mtoto wa Maskini, baba yangu alikuwa Rubani. Nimekataa Rushwa ya Milioni 300

Huyo mmiliki wa hiyo petrol station atafute wakili amfungulie kesi huyu waziri kwa sababu amemdhalilisha. Hapo mimi ningefungua kesi ya defamation na angenilipa mamilioni.
Hiyo rushwa ambayo nilimpa akakataa kwa nini asiwaite Takukuru wanikamate? Ndio kuja kunichafua hadharani hapana kwa kweli.

Huwezi kutafuta umaarufu kwa kumchafua mtu mwingine hadharani. Wewe mwenye petrol station chukua hatua
 
Je alimripoti TAKUKUKURU mtu aliyetaka kumpa rushwa hiyo ya m300/-?
 
Nimesikiliza video ya tukio lote niseme wazi tu mimi sina shida na waziri lakini katika hili namkosoa. Ndio kasema Rushwa kakataa lakini rushwa sio pesa tu unaweza kufanya jambo kwa kwa manufaa ya mtu au kikundi fulani na hapo haki utaikanyaga tu. Katika maongezi yote unajuwa kabisa hakuna kusikiliza na kuamua haki emekuja na matokeo mfukoni na kufanya tukio kwenye media. Kama alikuwa serious kweli hili ni jambo kulifanyia kazi ofisini ita wote lete vithibitisho vyote au internal audit wapitie utaratibu wote mwisho wanatoa report kama utaraibu haukufuatwa au uko sawa. Kama hukupenda nenda peleka maombi kubadilishia sheria. Kaambiwa JPM alitoa maagizo, waziri akatoa waraka halafu anamwambia usingekubali waraka wa waziri ungemwambia hautekelezeki, hivi huyu anajuwa maana ya malekezo ya Rais? anajuwa power ya Raisi kikatiba. Kila wizara ina legal department kupitia kila maelekezo kuona yako sawa.
Lakini hii sio tatizo anaweza kuwa sawa ila je Tanzania nzima shida hii iko Mikocheni tu? na kwanini kituo hiki tu? sababu ya vigogo wanakaa hapo. au yule Mama. Maana alishakuwa waziri wa ardhi aliwahi kuzuia hali kama hii. Yule Mama ana kiburi sana. Sasa waziri hebu wala usiende Tanzania nzima hapo Dar tu vituo vingapi viko kwenye makazi ya watu na wako kisheria sababu sheria zinaruhusu kuomba kubalisha matumizi, Kama kuna mianya rekebisha sheria. Kauli aliyotoa pale sijui S. Bridge kulikuwa na nini sijui kikabadilishwa matumizi kabla hamjaja mjini bado mko uko mikoani sijui wapi, hii ni kauli ya dharau na inaonesha wazi kaja pale na matokeo mfukoni wazi ana target mtu na kumshambulia kwa maisha yake binafsi, huko ulikokuwa.... Huyu hana maisha marefu na drama zake.
 
Pamoja na kwamba rushwa ni changamoto kubwa katika siasa zetu, Jerry anastahili pongezi nyingi kwa kupambana kwa maneno na vitendo. Amesema hadharani kwamba alipelekewa rushwa akakataa na amewaachisha watumishi kazi.
Hapana kama alikuwa anataka kuzuia hii hali angepokea halafu akachukua na ku report palepale ili hawa wachukuliwe hatua. Sheria inakutaka u report haya mambo.
 
Kama huyo mwenye kituo ana vibali vyote, basi amburuze Waziri wa Aridhi Mahakamani ili apate haki yake!!
Nakuhakikishia jamaa hakutaka drama kwenye media za waziri, ataenda mahakamani na atashinda rahisi kabisa ndio maana alikuwa mpole tu, sana sana ataambiwa tu rekebisha baadhi ya sehemu.
 
Jerry Slaa akikataa milioni 300 nakula ndala. Hana ubavu huo mwongo mkubwa.
Labda aliona ndogo sana kauliza kwa mwenyewe je ulitoa 300 au ulitoa zaidi watu wakapiga cha kwao. au kama anawaambia 300 ndogo. Ila Waziri rushwa sio pesa tu unaweza kuwa unafanya kumsaidia washkaji zao kama yule Mama hio pia rushwa, kuna aina nyingi za rushwa sio pesa tu. Sheria ilifuatwa ikiwa yes basi waziri kaa pembeni ka deal na sheria. Kusema bango mliweka mkapiga picha na kuliondoa kabla ya mwezi, hizo ni shutuma tu huna ushahidi.
 
Yeye kama Wazir amechukua hatua Gani baada ya hao anaodai walitaka kumpa rushwa?
 
Hapana kama alikuwa anataka kuzuia hii hali angepokea halafu akachukua na ku report palepale ili hawa wachukuliwe hatua. Sheria inakutaka u report haya mambo.
Rushwa za mamilioni mengi hazitolewi mkononi kama 50,000 anayopewa mtendaji kata au 5000 za polisi za kung'arisha viatu.
TAKUKURU hupewa taarifa na kuzuia zaidi kuliko kuweka mitego ambayo ni ngumu kupata ushahidi wa kutosha kutia hatiani.
Hata hivyo, hajasema alipelekewa pesa, Ila nilivyomsikia alipelekewa ujumbe kuwa pesa yake (300m) ipo kwenye mchakato huo wa ki rushwa.
Kitendo cha kuzungumza hadharani kina faida katika mapambano;
1. Kwenye kituo (mtuhumiwa) anaweza kuhojiwa na mwisho ataogopa kutoa tena rushwa. Vivyo hivyo maafisa waliohusishwa (kazi kwa TAKUKURU)
2. Waliohusishwa kimazingira (akiwemo mwenye kituo) aweza kudai fidia ya kuchafuliwa na waziri, kwa kuthibitisha uongo aliosema)
 
Quran imekataza kabisa rushwa.
Muislam hatakiwi kabisa kuikaribia rushwa. Sijajua ndugu zetu wa imani nyengine kama ktk vitabu vyao vimezungumzia.
jamani uislam ndio chaguo sahihi

β€œWALA MSILIANE MALI ZENU KWA BATILI NA KUZIPELEKA KWA MAHAKIMU ILI MPATE KULA SEHEMU YA MALI YA WATU KWA DHAMBI NA HALI MNAJUA” [2:188].
 
Je alimripoti TAKUKUKURU mtu aliyetaka kumpa rushwa hiyo ya m300/-?
Mkuu, hawa watu wanacheza na akili za watanzania ambazo hazitafakari wala kuhoji tunaloambiwa. Hivi waziri akihongwa anatakiwa fanye nini? Yaani waziri wa serikali anahongwa sh mil 300 halafu hachukui hatua? Kwa kifupi alizira kwa sababu aliona ni kidogo la sivyo angechukuwa hatua.
 
Pumbafu kabisa wewe. Huna akili. Au wewe ndiyo huyo Jerry. Unataka kutuaminisha waziri anayepelekewa ujumbe wa kupewa rushwa hawezi kuchukuwa hatua? Idiot!
 
Hatar sana πŸ˜…
 
Pumbafu kabisa wewe. Huna akili. Au wewe ndiyo huyo Jerry. Unataka kutuaminisha waziri anayepelekewa ujumbe wa kupewa rushwa hawezi kuchukuwa hatua? Idiot!
Mpumbavu, masikini wa akili hujibu hoja kwa matusi.
Siyo kosa lako, wasio na akili ni wengi kiasili, wewe ukiwa mmoja wao.
Kinachojadiliwa hapa ni hatua alizochukua. Amemsimamisha kazi mkurugenzi, amefika kituoni amesimamisha mchakato wa ujenzi na kutangazia Uma.
Wengine ubongo wenu bado upo kwenye hatua za mwanzo za evolution.
Hasira kama za wanyama tu, hata sokwe na jamii yake wana afadhali.
Fikiria kama binadamu, tafakari, jibu hoja kwa kuona mbali badala ya matusi.
 
Duh! Braza msamehe basi, ahahahah!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…