Waziri Kabudi akanusha kuthibitisha kifo cha Mwanahabari, Azory Gwanda

Waziri Kabudi akanusha kuthibitisha kifo cha Mwanahabari, Azory Gwanda

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi amekanusha kuwa amethibitisha 'kifo' cha mwanahabari Azory Gwanda.

Msemaji mkuu wa serikali ya Tanzania, Dkt Hassan Abbas amemnukuu Profesa Kabudi kwa kupitia mtandao wake wa kijamii wa Twitter akisema: "Nimepokea kwa masikitiko taarifa potofu zinazoendelea kuchapishwa kwenye mitandao ya kijamii ikinukuu kimakosa mahojiano yangu kwenye kipindi cha BBC FOCUS ON AFRICA zikidai kuwa nimethibitisha kwamba mwanahabari Azory Gwanda amefariki dunia."

Lakini Prof Kabudi pia amesema bado haijulikani kama Bw Gwanda yungali hai: "Mpaka sasa hakuna uthibitisho kuwa Azory yuko hai au amefariki. Vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea kuchunguza tukio hilo na matukio mengine yaliyotokea katika machafuko ya Kibiti, Pwani yaliyosababisha ama watu kadhaa kupoteza maisha au kupotea."

Kabudi amesema kuwa, kilichotokea ni tafsiri potofu ya kile alishokisema: "Hii sio tafsiri sahihi kuhusu kile nilichokisema. Katika mahojiano hayo nilieleza kuwa tukio lililotokea Kibiti lilikuwa ni la kuhuzunisha na wapo watanzania waliouawa na wengine kupotea. SIKUTHIBITISHA kuwa Azory Gwanda amefariki."

ZAIDI, SOMA:
 
Waziri amechemka on camera. Maelezo yake yaliacha mwanya kwa watu kuwa na tafsiri sahihi kuwa Aazory Gwanda amefariki.

Kakosea kwanza kwa kusema hivyo, halafu anaendelea kukosea kwa kushindwa kuomba radhi na kukubali kosa, analaumu tafsiri.
Ujumbe tulioupata hapa ni kurudi darasani kujifunza lugha upya. Maana ni wengi tumemuelewa tofauti na alichokusudia kutueleza.
 
Ujumbe tulioupata hapa ni kurudi darasani kujifunza lugha upya. Maana ni wengi tumemuelewa tofauti na alichokusudia kutueleza.
Yeye ndiye anapaswa kurudi darasani kujifunza tofauti ya "disappeared and died" na "disappeared or died".

Kama hawa ndio watu wanaosimamia mikataba yetu, si ajabu tunapigwa changa la macho kila siku.
 
Alipaswa kusema ‘waliopotea au kuuwawa’.

Siyo ‘waliopotea na kuuwawa’ maana hiyo inaacha mwanya wa tafsiri zingine.

Yeye kama mwanasheria nguli nilitegemea awe makini sana na uchaguzi wa maneno atumiayo.
Jamaa anaongea kwa kasi, jazba na pupa sana.

Ukimsikiliza kakosea hata jina kataja Azory Rwanda.

Huku katoa mimacho kama mjusi kabanwa na mlango.
 
Waziri amechemka on camera. Maelezo yake yaliacha mwanya kwa watu kuwa na tafsiri sahihi kuwa Aazory Gwanda amefariki.

Kakosea kwanza kwa kusema hivyo, halafu anaendelea kukosea kwa kushindwa kuomba radhi na kukubali kosa, analaumu tafsiri.
prof. hakukosea kabisa ila tumewazoea mkitengeneza tafsiri zenu mnapomchukia mtu na natambua Prof anachukiwa kwa nguvu na uwezo alionao katika kujenga hoja.

mlipokosea ni kudhani kwamba prof anaweza kuongea kama Sugu au Mbowe, lazima daima ujue kwamba yule mtu anapoongea anaongea mambo mazito na magumu kwa watanzania wengi kuyaelewa haraka
 
Jamaa anaongea kwa kasi, jazba na pupa sana.

Ukimsikiliza kakosea hata jina kataja Azory Rwanda.

Huku katoa mimacho kama mjusi kabanwa na mlango.

Huyo jamaa anaonekana ni mbabaishaji flani hivi!

Nguli gani wa sheria hajui matumizi ya ‘na’ na ‘au’ na implications zake?

Hapo kwenye maelezo yake alipaswa tu kusema kuwa aliteleza kidogo na hakumaanisha kama ilivyopokelewa na watu.

Instead, he’s doubling down on it and blaming others!

Ndo maana baadhi yetu tuliguna na kukuna vichwa vyetu tuliposikia kateuliwa kuwa waziri wa mambo ya nje.
 
prof. hakukosea kabisa ila tumewazoea mkitengeneza tafsiri zenu mnapomchukia mtu na natambua Prof anachukiwa kwa nguvu na uwezo alionao katika kujenga hoja.

mlipokosea ni kudhani kwamba prof anaweza kuongea kama Sugu au Mbowe, lazima daima ujue kwamba yule mtu anapoongea anaongea mambo mazito na magumu kwa watanzania wengi kuyaelewa haraka
Ungeeleza kwa nini hakukosea, kwa ushahidi wa maneno aliyotumia, ambayo yapo kwa ushahidi wa video mtandaoni, ningekuona wa maana zaidi.

Sasa hivi naona unapinga kitu bila ushahidi.

Mimi nimeeleza kwamba matumizi yake ya maneno "disappeared and died" yalimaanisha wote aliowaongelea wamekufa, angeweza kutetewa kama angetumia maneno "disappeared or died".

Hujagusa hata kidogo hoja yangu kwa kutumia maneno hayo aliyotumia.

Kwa nini?

1. Wewe ni mvivu tu wa kufikiria, kitabia, na hujui kupinga kitu kwa hoja?
2. Wewe ni mshenzi tu wa tabia unajua kwamba kakosea lakini hutaki kujadili hoja, unapinga kijumlajumla tu?
 
Back
Top Bottom