Waziri Kabudi kuzindua bodi ya ithibati ya waandishi wa habari machi 3

Blasio Kachuchu

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2016
Posts
366
Reaction score
243
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Palamagamba Kabudi, Wiki ijayo anatarajiwa kuzindua Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB).

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Bw. Gerson Msigwa imeeleza kuwa uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika tarehe 03 Machi, 2025 katika Hotel ya Johari Rotana jijini Dar es Salaam.

Katika Uzinduzi huo Waziri Kabudi pia atamkabidhi zana za Kazi Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Bw. Tido Mhando, zinazojumuisha Sera ya Habari, Sheria ya Huduma za Habari na Kanuni zake.

Miongoni mwa majukumu ya Bodi hiyo yanayotarajiwa kuanza kutekelezwa mapema mara baada ya kuzinduliwa ni pamoja na kutoa Ithibati na Vitambulisho (Press Card) kwa Waandishi wa Habari waliokidhi vigezo vilivyoainishwa kisheria na kusimamia maadili ya taaluma ya Uandishi wa Habari.

Kwa kuzingatia matakwa ya Sheria ya Huduma za Habari, Sura ya 229, Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari imepewa mamlaka ya kutoa Vitambulisho kwa Waandishi wote kutoka vyombo vya habari vya umma, binafsi, pamoja na waandishi wa kujitegemea.

Awali, utoaji wa vitambulisho hivyo kwa Waandishi wa Habari ulikuwa ukifanywa na Idara ya Habari-MAELEZO kabla Bodi ya Ithibati kuundwa na kuanza majukumu yake rasmi.

Bodi hiyo ilitangazwa Septemba 18 mwaka jana baada ya Waziri mwenye dhamana kumteua Bw. Mhando na wajumbe wengine sita kuunda bodi hiyo, sanjari na kuwahamishia watumishi sita kutoka wizarani kuunda Sekretarieti ya bodi hiyo.
 
Na Mwandishi Wetu, JAB, Dar es Salaam

Ukichunguza kwa umakini Sana kuhusiana na madhumuni hasa ya kuanzishwa kwa Bodi hiyo ya Waandishi wa Habari hasa ni Serikali kutaka kuwadhibiti Waandishi wa Habari ili kusudi Waandishi wote kabisa wawe Machawa na Waimba Mapambio ya Kusifu na Kuabudu Watawala pamoja na Vibaraka wao. Nothing good!

Waandishi wa Habari watakaokataa Kusifu na Kuwaabudu Watawala na Vibaraka wao basi watakumbana na Visa na majanga ya Kufungiwa Leseni zao, Kunyang'anywa pamoja na Kufutiwa Usajili wa kufanya kazi za Uandishi wa Habari hapa Tanzania.

Kwa hiyo Waandishi wa Habari wajiandae Kisaikolojia kukabiliana na janga hili jipya linalowanyemelea.
Wakumbuke kisa Cha Fatma Karume kufungiwa Leseni ya Uwakili hapa Tanganyika.

Waandishi wa Habari wa Tanzania sasa watakuwa na kazi moja tu ya :
Kusifu na Kuabudu Watawala!
 
Ithibati gani wakati fani na taaluma ya uandishi wa habari inataka utashi na ubunifu binafsi na haiishii kusomea masetifiketi, madiploma na madigrii tu? Hiyo ni fani huria no limit labda code of journalism ethics tu ndio iwe guideline doctrine. Kuna waandishi wamekosa ubunifu kabisa huku ni degree holder
 
Ile dhana ya kuita waandishi wa habari chipukizi wenye weledi na wabunifu kuwaita MAKANJANJA iliishia wapi? Tena kipindi hicho hakukuwa na online media. Zama hizi za kidigitali kuleta rules/terms and conditions kwenye masuala ya uandishi wa habari kwa mtazamo wa ukale hizo rules/condition will not applicable otherwise new perspection acted on it. Media zimepanuka sana kiasi kwamba kila mtu anaweza kuandika habari popote alipo
 
Back
Top Bottom