Waziri Kalemani: Bwawa la Nyerere kujazwa Maji Novemba 15, 2021. Umeme wa maji ni nafuu kuliko wa vyanzo vingine

Uko sahihi. Hata Muhongo hajawahi kuikazania nyukilia. Anajua. Yeye anahamasisha vyanzo vingine, kubwa gesi
 
Prof Muhongo yupo Bungeni maana siku kadhaa nyuma nilimsikia kwamba umeme wa gesi ndio wa gharama nafuu na wa uhakika ukilinganisha na huu wa kizamani wa maji.
Muhongo hajawahi kusema kuwa umeme wa maji ni ghali au usiendelezwe. Yeye anataka energy mix ya vyanzo vingi vya kisasa, siyo kuweka mategemeo kwenye maji pekee. Kwanza maji hupunguzwa na shughuli-ongezeko za binadamu au ukame.

Kwa sababu hiyo wale wajuaji wa America na Ulaya walishabakisha asilimia ndogo sana, chini ya 10%, ya umeme ambayo inatokana na maji. Ni Norway peke yao ambao umeme wao karibu wote ni wa maji. Energy mix ndio ushauri wa wataalamu kama Muhongo
 
Prof Muhongo si aliapa kuwa hatatoa siri za Baraza la mawaziri
Muhongo ni Mtaalamu wa Madini, siyo Umeme. Anachokisema siyo kwa ajili ya taaluma yake. Hana huo utaalamu.

Enzi akiwa Waziri wa Nishati alizungumzia kutuletea umeme toka Ethiopia, ambao ni wa maji akidai kuwa ni utakuwa wa bei nafuu. Kitendo cha yeye kuusimanga huu mradi inatia wasiwasi sana na nia yake hasa kwenye hii issue.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]wamesema mwezi wa nane SGR safari za Dar-Moro zinaanza..
 
Nuclear ni cheaper zaidi..
Maji kuna gharama za mazingira kubwa Sana
Kufyeka heka zote zile utasema hakuna gharama?

Amepima loss yake? Kufyeka heka zaidi ya milioni?
Nuclear ki mazingira ni hatari zaidi kwakua effect yake ni generational...Belgium waliufinga mtambo wao wa nuclear miaka 5 iliyopita, Japan pia ili pata hasara kubwa sana.

Umeme cheapest ni maji, hakuna ubishi ila si nchi zote zina comparative and competitive advantage kutokana na kukosa geographical feature zenye kuwezesha miradi kama hiyo.

Norway karibia 100% ni hydropower na wanaiza umeme wao hadi nje ya nchi yao, sweden wanatumia biofuel kugenerate energy...Prof. aliitumia taaluma yake vibaya kulipiza kisasi japo he had a point...Dhamira yake ndiyo inayomhukumu
 
Watu wengi wanaokazania mambo ya gas inatilia shaka sana, pengine wana miradi yao humo ndani binafsi, labda hilo lingechunguzwa kwanza.

Na kisha mkataba wake uwekwe wazi kwani sheria ya sasa inaruhusu hivyo. Kama wapo bold enough na wana dhamira njema waiweke wazi mikataba yote hiyo ya zamani watanzania waone na waamue kipi ni kweli kipi si kweli na kwa faida ya nani
 
Hizo bei zimepangwa na EWURA?Tusipotoshe umma kwa propaganda mfu.Wakati wa ujenzi wa bomba la gas toka Mtwara tuliambiwa maneno matamu kuwa tatizo la umeme Tanzania limepata muarobaini wake,CCM hii hii leo wanaanza mradi Mpya wa HydoPower wanatulazimisha tuwaamini tena?
Bomba gas lipo under utilized,hilo hawalijadili wanapigia debe miradi ambayo kufanya ufisadi ni rahisi kuliko kuwekeza kwenye mitambo ya kuzalisha umeme kwa Gas wanasingizia kwamba imechukuliwa na wajanja.Pathetic Minister!
 
Bado mwezi na nusu ifike hiyo Novemba.
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…