Waziri Kalemani: Bwawa la Nyerere kujazwa Maji Novemba 15, 2021. Umeme wa maji ni nafuu kuliko wa vyanzo vingine

Waziri Kalemani: Bwawa la Nyerere kujazwa Maji Novemba 15, 2021. Umeme wa maji ni nafuu kuliko wa vyanzo vingine

Tanzania wamejaa akina profesa Muhogo ambao enzi zao walikuwa wanaingia mikataba mingi ya kitapeli kwa manufaa yao na wakati mwendazake alipokuwa hai hawakuwa na jeuri ya kubweka kama wanavyobekwa hivi sasa, kweli mwendazake alikuwa chiboko mijizi na mitapeli yote ilikuwa kimya
Mkuu mpambe wa Kalemani tunaomba utueleze sisi watumiaji tutalipa bei gani? Porojo hazitakusaidia kitu
 
Sio story ni vitu halisia, TANESCO ilikuwa katika hali ngumu sana kibiashara kipindi cha JK, umeme wa Dowans na IPTL ulikuwa unatumia mafuta mazito ambao ndio umeme wa gharama zaidi, kama isingekuwa maamuzi ya kibabe na kishujaa ya Magu mpaka saivi tungekuwa tunaongelea hasara tu za TANESCO.
Tusisahau ndugu zangu watz tunaposema "KIPINDI CHA JK" tusiwe na maana kwamba ilikuwa upigaji mtupu. Tukumbuke wakati anaingia tu nchi ilikuwa na matatizo makubwa ya umeme tena makubwa sana naamini jukumu lake kubwa lilikuwa kuhakikisha umeme unarejea katika hali ya kawaida.

Utapata wapi kwa haraka vyanzo vya kuzalisha umeme, jibu ni kukodisha magenarator ambayo yapo tu sokoni, katika hilo na wapiga deal wakawemo kama tunavyoona sasa hivi pamoja na hayati Rais wetu JPM kuwa mkali sana kwenye matumizi ya fedha za serikali, wapigaji kumbe walikuwemo tu!!! Kwa hiyo watz tuwe tunaweka kumbukumbu vizuri wakati wote.
 
Mleta mada umetafuniwa Kwanza ndipo ukaona uulize Hilo swali la kipuuzi, propesa Wakati analaumu uwekezaji na ujenzi wa bwawa la umeme, hakutaja gharama za uzalishaji wa umeme aliokuwa akiutetea,

Huyu waziri kaja na data, huoni kwamba kuna mtu anatafuta uteuzi Kwa nguvu?
 
Ninawasalimu wote,

Waziri wa Nishati Dkt. Kalemani amesema Bwawa la Nyerere litajazwa Maji Novemba 15 mwaka huu wa 2021 na ameeleza gharama za kuzalisha umeme kwa kila chanzo kuwa,

• Maji ni shilingi 36 kwa unit moja.

• Nyuklia ni shilingi 65 kwa unit moja.

• Solar na upepo shilingi 103 kwa unit moja.

• Makaa ya mawe shilingi 118 kwa unit moja.

• Joto Ardhi shilingi 119 hadi 120 kwa unit moja.

• Gas shilingi 147 kwa unit moja.

• Mafuta mazito shilingi 546 kwa unit moja.

Pia alisema umeme wa maji ndio wa nafuu kuliko vyanzo vingine vyote. (Alipokuwa akitoa Taarifa hii kulikuwa na shangwe za kutosha).

Binafsi nampongeza sana kwa ufafanuzi alioutoa.

Lakini nahitaji Mheshimiwa Waziri wa Nishati atuambie na Kututhibitishia kwa UWAZI kabisa GHARAMA AMBAYO MTUMIAJI WA UMEME ATATOZWA KWA KILA UNIT MOJA (1) baada ya BWAWA LA MWALIMU NYERERE Kuanza kuzalisha Umeme.

Hii habari ya kutuambia na kutuaminisha kuwa Umeme wa Maji ni umeme wa Gharama nafuu bila kutuambia na kutuhakikishia Gharama halisi kwa Unit Kwa Mtumiaji wa Mwisho ni kutuona Sisi Watanzania kuwa ni Wajinga.
Cc:- Prof.S. Muhongo
 
tusisahau ndugu zangu watz tunaposema "KIPINDI CHA JK" tusiwe na maana kwamba ilikuwa upigaji mtupu. tukumbuke wakati anaingia tu nchi ilikuwa na matatizo makubwa ya umeme tena makubwa sana naamini jukumu lake kubwa lilikuwa kuhakikisha umeme unarejea katika hali ya kawaida. utapata wapi kwa haraka vyanzo vya kuzalisha umeme jibu ni kukodisha magenarator ambayo yapo tu sokoni, katika hilo na wapiga deal wakawemo kama tunavyoona sasa hivi pamoja na hayati Rais wetu JPM kuwa mkali sana kwenye matumizi ya fedha za serikali, wapigaji kumbe walikuwemo tu!!! kwa hiyo watz tuwe tunaweka kumbukumbu vizuri wakati wote
Acha kutetea ujinga, kama ilikuwa temporary solution kwa nini aliingia mikataba ya kijinga ya Dowans na IPTL? JK alikuwa ameifilisi Tanesco, hadi 2015 umeme ilikuwa ni luxurious service kwa watz, saivi bila aibu tena mifisadi na mishetani ile ile inatumia njia zile zile tena kutaka kuanza kuinajisi nchi hii.
 
Mkuu mbona maneno mengi sana? Jibu swali Stiglaz ikikamilika umeme utauzwa kiasi gani kwa unit 1? . Kama hujui ni vyema useme hujui ili Waziri atuambie
 
Unaonyesha umbumbu wako, hiyo hapo ni bei ya kuzalisha, ukiuza unit 1 sh 37 inamaanisha Maintainance cost na kurudisha pesa ya investment hamna, bei itashuka kidogo sana Ila shirika la Tanesco litaanza kutengeneza faida ambayo inaweza kutumika kuanzisha miradi mingine badala ya kuchota serikali kuu.

FYI; Kipindi cha JK Tanesco walikuwa wanauziwa unit moja zaidi ya Tsh 400 sababu ya mikataba ya kijinga ya Dowans, IPTL na ifananayo...

Sasa hivi unit chini ya hiyo 400 na kama tarif yako ndogo bei inakua kama shs 100 na kidogo kwa unit..
Mimi natumia umeme sana nanunua unit kwa 357
 
Ninawasalimu wote,

Waziri wa Nishati Dkt. Kalemani amesema Bwawa la Nyerere litajazwa Maji Novemba 15 mwaka huu wa 2021 na ameeleza gharama za kuzalisha umeme kwa kila chanzo kuwa,

• Maji ni shilingi 36 kwa unit moja.

• Nyuklia ni shilingi 65 kwa unit moja.

• Solar na upepo shilingi 103 kwa unit moja.

• Makaa ya mawe shilingi 118 kwa unit moja.

• Joto Ardhi shilingi 119 hadi 120 kwa unit moja.

• Gas shilingi 147 kwa unit moja.

• Mafuta mazito shilingi 546 kwa unit moja.

Pia alisema umeme wa maji ndio wa nafuu kuliko vyanzo vingine vyote. (Alipokuwa akitoa Taarifa hii kulikuwa na shangwe za kutosha).

Binafsi nampongeza sana kwa ufafanuzi alioutoa.

Lakini nahitaji Mheshimiwa Waziri wa Nishati atuambie na Kututhibitishia kwa UWAZI kabisa GHARAMA AMBAYO MTUMIAJI WA UMEME ATATOZWA KWA KILA UNIT MOJA (1) baada ya BWAWA LA MWALIMU NYERERE Kuanza kuzalisha Umeme.

Hii habari ya kutuambia na kutuaminisha kuwa Umeme wa Maji ni umeme wa Gharama nafuu bila kutuambia na kutuhakikishia Gharama halisi kwa Unit Kwa Mtumiaji wa Mwisho ni kutuona Sisi Watanzania kuwa ni Wajinga.

Wewe Utakuwa wa Gesi haya Kachukue gesi yako Uzalisha....
Na Hatutatumia Gesi ng’ooo
 
Tanzania wamejaa akina profesa Muhogo ambao enzi zao walikuwa wanaingia mikataba mingi ya kitapeli kwa manufaa yao na wakati mwendazake alipokuwa hai hawakuwa na jeuri ya kubweka kama wanavyobekwa hivi sasa, kweli mwendazake alikuwa chiboko mijizi na mitapeli yote ilikuwa kimya
Prof Muhongo si aliapa kuwa hatatoa siri za Baraza la mawaziri
 
Mkumbuke ni enzi za JPM service charge ya kila mwezi ilifutwa rasmi
Na bado Tanesco ikiweza kufanya maintainance, watz tunasahau mapema sana ujinga na upumbavu uliyokuwa Tanesco, Tanesco ilishashindikana hadi wabunge walisha shauri ikatwe mara tatu yaani ili tu kujaribu kuongeza ubunifu. Uthubutu wa JPM kuvunja mikataba ya kishenzi na kujenga na kumalizia miradi ya Kinyerezi ndio imeiokoa TANESCO.
 
Watanzania wanazaliwa mpaka uzee wanapewa hadith za megawatts na bei za umeme ila kutumia jiko la umeme kama kupikia itabaki kuwa Hadith tena...hiyo gesi tuu mtihani mnaendelea kudanganya na tsh 37 ya unit ya umeme kwa unit moja kwa kipindi hiki...
 
Back
Top Bottom