Waziri Kamwelwe atangaza mkakati wa kupambana na ugonjwa wa Coronavirus kwenye vyombo vya usafiri

Mh Waziri achana na siasa. Magari yote ya kusafirisha abiria idadi ya abiria inajulikana na pale wanaporuhusiwa kusimamisha pia idadi inajulikana. Latra hawahitaji kuitamka kwa sababu tayari iko katika ruhusa yao ya biashara. Kinachotakiwa Mh Waziri ni kutekeleza, kitu ambacho kimetushinda wakati wote. Nchi zinazotuzunguka abiria katika daladala zao ni level seating.
 
Huyu bado hajatumbuliwa tu jamani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu unapotoa mifano,au kulinganisha vitu uwe unatafakari kwanza!
 
Mamlaka ya Kudhibiti usafiri wa ardhini nchini (Latra) imetoa maelekezo kwa wamiliki wa mabasi ya abiria kuhakikisha abiria wote wanakaa yaani "level seat"

Source: Mwananchi
 
Bro!! johnthebaptist Hilo agizo umeolionaje? Hawa viongozi wenu wa Lumumba Wana akili za kuvukia barabara tu
Bwashee level seat ni kwa mujibu wa sheria na imeelezwa bayana kwenye kadi ya gari idadi ya abiria.

Hata kwenye mlango wa dereva huandikwa idadi ya abiria wanaoruhusiwa kisheria.

Maendeleo hayana vyama!
 
Wakitaka ivyo walete mabasi yao hao Latra,lakini kwa hawa wenye daladala biashara kwao itakuwa ngumu sana,Sipati picha iyo asubuhi ama jioni kwa gari za Mbagara ama Gongo la Mboto wataweza iyo level seat
Nimekuelewa sana!
 
Sidhani kama ili linahusiana na Corona maana sheria ipo ila utekelezaji wake ndio ulikuwa hafifu. Bado serkali haijajua namna ya kuwakinga watu na corona au wanafanya kusudi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama kweli wapo serious nashauri utekelezaji uanzie kwanye mabasi ya mwendo kasi pamoja na treni ya jiji (treni ya Mwaikembe?)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…