Waziri Katambi: Rais Samia usiumie inapotokea mtu anafanana na Choroko

Waziri Katambi: Rais Samia usiumie inapotokea mtu anafanana na Choroko

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
Wakuu

Waziri wa mambo ya ndani Patrobas Katambi anawabatiza watu wenye mitazamo mbadala kama "wasaliti" na "choroko zisizoiva," huku akitumia mifano ya kidini kumweka Rais kwenye nafasi ya asiyekosea.

Waziri Katambi ameyasema hayo katika hafla ya kuhitimisha Mafunzo ya Maafisa na Wakaguzi Wasaidizi wa Polisi, Kurasini, Da es Salaam tarehe 28 Mei, 2026.

"Lakini pia Usukumani, ipo kitu kinaitwa... tunaita sisi nduru, zinaitwa choroko hizi Mheshimiwa Rais. Hata upike kwa moto wa gesi ya blue huu, moto ule... blue flame, ipo choroko moja haitaiva Mheshimiwa Rais, ipo. Na watu wapo hivyo hivyo."

"Kwa hiyo usiumie Mheshimiwa Rais, inapotokea kuna mtu anafanana na choroko. Usiumie Mheshimiwa Rais, kama wakati wa Yesu, mfano... Mwana wa Mungu, aliteua 12 lakini wakatokea wasaliti wawili; mmoja akamkana, aliitwa Petro, na mwingine Yuda Iskariote alimsaliti."

"Kwa hiyo hata wapo pia ambao tunaweza tukawa wasaliti kwako, na wapo wa kukukana. Usi... usiwe na wasiwasi kwa sababu mpango wapo... mpewa hapokonyeki Mheshimiwa Rais. Songa mbele, vyombo vya ulinzi na usalama tuko pamoja na wewe kwa sababu tunataka maslahi ya wananchi yasimamiwe, haki, ulinzi na usalama uwepo, amani na utulivu kwa taifa letu uendelee kuwepo."

"Sheria tunazijua na taratibu tunazijua, wanaopindisha tutakutana nao kwenye nyanja mbalimbali."



 
Wakuu

Waziri wa mambo ya ndani Patrobas Katambi anawabatiza watu wenye mitazamo mbadala kama "wasaliti" na "choroko zisizoiva," huku akitumia mifano ya kidini kumweka Rais kwenye nafasi ya asiyekosea.

Waziri Katambi ameyasema hayo katika hafla ya kuhitimisha Mafunzo ya Maafisa na Wakaguzi Wasaidizi wa Polisi, Kurasini, Da es Salaam tarehe 28 Mei, 2026.
hizi kazi ya uchawa ni ngumu kubabake. ngumu sana
 
"Polisi akitishiwa kulengwa jiwe na raia mara moja polisi anatakiwa kushambulia kwa silaha aliyo nayo ambayo ni bunduki Shut and kill"

THABIT KOMBO
 
Back
Top Bottom