Waziri Kombo afanya mazungumzo na Uongozi wa Kampuni ya Viettel

Waziri Kombo afanya mazungumzo na Uongozi wa Kampuni ya Viettel

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo, amefanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Kampuni ya Viettel, ambayo ni kampuni tanzu ya Kampuni ya Mawasiliano ya Haotel Tanzania Kanali Dao Xuan Vu, katika makao makuu ya kampuni hiyo jijini Hanoi, Vietnam.

WhatsApp Image 2025-04-28 at 21.55.57_230161b0.jpg

WhatsApp Image 2025-04-28 at 21.55.58_fcfbe42c.jpg
Mazungumzo hayo yalilenga kujadili kuhuhusu fursa mpya za uwekezaji zilizopo nchini na kuimarisha ushirikiano katika sekta za biashara na uwekezaji.

WhatsApp Image 2025-04-28 at 21.55.58_b10eec1a.jpg

WhatsApp Image 2025-04-28 at 21.55.58_5abd562a.jpg
Waziri Kombo yuko nchini Vietnam kwa ziara ya kikazi, akiwa ameambatana na Balozi wa Tanzania nchini humo mwenye Makazi yake Jamhuri ya Watu wa China, Khamis Omar, Mkurugenzi wa Idara ya Diplomasia ya Uchumi na Biashara ya Kimataifa Balozi John Ulanga, Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia Bi. Felista Rugambwa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania, Gilead Teri na Viongozi wa Sekta Binafsi na Wafanyabiashara.
WhatsApp Image 2025-04-28 at 21.55.57_006b19d7.jpg

WhatsApp Image 2025-04-28 at 21.55.57_3e746625.jpg
 
Back
Top Bottom