PostGE2025 Waziri Kombo akutana na Balozi wa India nchini Tanzania Bishwadip Dey

PostGE2025 Waziri Kombo akutana na Balozi wa India nchini Tanzania Bishwadip Dey

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,773
Reaction score
1,174
Waziri Kombo akutana na Balozi wa India nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa India nchini, Mhe. Bishwadip Dey, katika ofisi ndogo za Wizara, jijini Dar es Salaam, tarehe 06 Desemba, 2025.

Mazungumzo hayo yamezingatia maeneo ya ushirikiano zaidi kati ya Tanzania na India, kwa lengo la kuimarisha diplomasia ya kiuchumi kupitia biashara na uwekezaji.

Akizungumza katika kikao hicho, Mheshimiwa Kombo ameishukuru Serikali ya India, kupitia ubalozi wake nchini, kwa mchango wake katika maendeleo ya sekta ya afya, ikiwemo kambi maalum ya kugawa viungo bandia kwa Watanzania waliopoteza viungo, iliyofanyika hivi karibuni kwa ushirikiano kati ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) na Ubalozi wa India nchini.

Mheshimiwa Kombo ameiomba India kuendelea na kampeni hizo, ikiwemo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na Kilimanjaro Christian Medical Center (KCMC), ili kuwafikia watu wengi zaidi waliopatwa na ulemavu baada ya kupoteza viungo vyao.

Naye Balozi wa India nchini, Mhe. Bishwadip Dey, ameonesha azma ya India ya kuongeza ushirikiano na Tanzania katika sekta za kilimo (mbaazi/pigeon peas), maji, mafunzo kwa madaktari na wafamasia, ufadhili wa masomo katika vyuo vikuu vya India, biashara na uwekezaji, kwa lengo la kuimarisha diplomasia ya watu kwa watu na kuchochea ukuaji wa uchumi wa mataifa haya mawili.

Aidha, Balozi Bishwadip Dey amesisitiza umuhimu wa Tanzania na India kushirikiana katika kuelimisha wananchi kuhusu mafanikio ya miradi ya maendeleo na thamani ya uhusiano wa nchi hizi kimataifa, ili kuviendeleza kwa vizazi vijavyo.
IMG-20251207-WA0033.jpg
IMG-20251207-WA0043.jpg
IMG-20251207-WA0047.jpg
IMG-20251207-WA0053.jpg
IMG-20251207-WA0036.jpg
 
Baada ya manyonyo kujikosha mbele ya wazee wasio na akili, sasa mnarudi kujisafisha kwa kulamba makalio watu wa nje ili muendelee kusaidiwa hizo pesa ndogo mlizozikataa 😂
 
Mbona km mtu na nduguye, au macho yanguu??
 
Waziri Kombo akutana na Balozi wa India nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa India nchini, Mhe. Bishwadip Dey, katika ofisi ndogo za Wizara, jijini Dar es Salaam, tarehe 06 Desemba, 2025
Deal limeshatik. Korosho na Dengu zaidi india, Dhahabu na madini zaidi. Majibu ya vikwazo hayo.... Kuna zaidi ya nchi 20 zipo kwenye foleni. Hatufi njaa.
 
Back
Top Bottom