Waziri Kombo ampokea Makamu wa Rais Dkt. Mpango Jijini Roma

Waziri Kombo ampokea Makamu wa Rais Dkt. Mpango Jijini Roma

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,773
Reaction score
1,174
WAZIRI KOMBO AMPOKEA MAKAMU WA RAIS DKT. MPANGO JIJINI ROMA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo amempokea Makama wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango jijini Roma, Italia ambapo atamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Misa ya Mazishi ya aliyekuwa Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani Baba Mtakatifu Francisko itakayofanyika katika Mji wa Vatican Aprili 26, 2025.

Katika mapokezi hayo Waziri Kombo aliambatana na Balozi wa Tanzania katika Mji wa Vatican mwenye makazi yake nchini Ujerumani, Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika (DEA) katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushikiano wa Afrika Mashariki Balozi Swahiba Mndeme, na watendaji wengeni wa Serikali.
IMG-20250426-WA0012.jpg
IMG-20250426-WA0016.jpg
IMG-20250426-WA0022.jpg
IMG-20250426-WA0021.jpg
 

Attachments

  • IMG-20250426-WA0018.jpg
    IMG-20250426-WA0018.jpg
    479.7 KB · Views: 44
  • IMG-20250426-WA0017.jpg
    IMG-20250426-WA0017.jpg
    547.3 KB · Views: 46
Safi . Pongezi kwa viongozi wetu wa Serikali kwa kushiriki kikamilifu mazishi ya mpendwa wetu Papa Francis
 
Ee Mungu unapowazuru wengine uanzie kwangu Ee Bwana.
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango, akishiriki Misa ya Mazishi ya aliyekuwa Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, hayati Baba Mtakatifu Francisko iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro - Vatican
 

Attachments

  • publer-1746579504283.mp4
    31.2 MB
Back
Top Bottom