Habari za Zanzibar
JF-Expert Member
- Dec 18, 2024
- 651
- 433
WAZIRI KOMBO AMUAGA BALOZI WA SWEDEN HAPA NCHINI.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Mahmoud Thabit Kombo (Mb), tarehe 17 Julai, 2026 amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Sweden hapa nchini Mhe. Charlotta Ozaki Macias, ambaye anamaliza muda wake wa utumishi wa kibalozi nchini.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kumuaga iliyofanyika ofisi ndogo za wizara jijini Dar es Salaam, Mhe. Waziri Kombo alimpongeza Balozi Charlotta kwa utendaji wake mzuri wa kazi na ushirikiano mkubwa aliouonyesha katika kipindi chote alichokuwa hapa nchini, akimuelezea kama mtu wa tofauti katika utendaji kazi na utekelezaji wake wa majukumu kwa kuwa alijitolea kikamilifu kuhakikisha ushirikiano kati ya Tanzania na Sweden unaimarika na kukua zaidi.
Kwa upande wake Balozi Charlotta ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ushirikiano iliompatia wakati wote alipokuwa nchini akitekeleza majukumu yake ya kibalozi, aidha ameelezea kufurahishwa na uhusiano mzuri uliopo baina ya Sweden na Tanzania na amepongeza hatua mbalimbali ambazo Serikali ya Tanzania imeendelea kuzichukua katika kuimarisha diplomasia ya uchumi duniani.