Waziri Kombo amuwakilisha Makamu wa Rais kwa Rais wa Mfuko wa OPEC

Habari za Zanzibar

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2024
Posts
651
Reaction score
433
Mheshimiwa Balozi Dkt. Mahmoud Thabit Kombo, (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, alimwakilisha Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius John Ndejembi kwenye mazungumzo na Dkt. Abudlhamid Alkhalifa, Rais wa Mfuko wa Maendeleo wa OPEC yaliyofanyika tarehe 16 Septemba 2026 Makao Makuu ya Mfuko.

Katika mazungumzo hayo, Mheshimiwa Waziri alimshukuru Dkt. Alkhalifa kwa kuidhinisha miradi mbalimbali inayotekelezwa nchini Tanzania kwa mikopo na misaada kutoka Mfuko wa OPEC.

Mheshimiwa Balozi Kombo alithibitisha dhamira ya dhati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuendelea kushirikiana na Mfuko katika kutekeleza miradi mbalimbali ya kipaumbele ikiwemo nishati hususan nishati safi ya kupikia, miundombinu ya usafirishaji, afya, elimu na kilimo.

Dkt. Alkhalifa alipongeza jitihada zinazofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuletea maendeleo wananchi kupitia miradi mbalimbali ya kipaumbele.

Aidha, aliahidi kwa niaba ya Mfuko kuendeleza ushirikiano mzuri uliopo Kati ya Tanzania na Mfuko wa OPEC na kuifanya Tanzania kielelezo cha ushirikiano wa mfano barani Afrika.

Kwenye mazungumzo hayo, Mheshimiwa Balozi Kombo aliambatana na Mhe. Saada Salum Mkuya, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Prof. Adolf Mkenda (Mb.), Waziri wa Elimu, Sayansi na Taknolojia; Mhandisi Felchesmi Mramba, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Prof. Carolyne Nombo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Taknolojia, na Bw. Rished Bade, Kamishna wa Fedha za Nje kutoka Wizara ya Fedha.
 
Attachments

  • Mheshimiwa Balozi Dkt. Mahmoud Thabit Kombo, (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afr.jpg
    Mheshimiwa Balozi Dkt. Mahmoud Thabit Kombo, (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afr.jpg
    118.1 KB · Views: 11
  • Mheshimiwa Balozi Dkt. Mahmoud Thabit Kombo, (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa A...jpg
    Mheshimiwa Balozi Dkt. Mahmoud Thabit Kombo, (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa A...jpg
    114.2 KB · Views: 6

    119.3 KB · Views: 10

    102.6 KB · Views: 8

    91.9 KB · Views: 15

    125.7 KB · Views: 13

    118.6 KB · Views: 11
Mheshimiwa Balozi Dkt. Mahmoud Thabit Kombo, (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, alimwakilisha Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius John Ndejembi kwenye mazungumzo na Dkt. Abudlhamid Alkhalifa, Rais wa Mfuko wa Maendeleo wa OPEC yaliyofanyika tarehe 16 Septemba 2026 Makao Makuu ya Mfuko.

Katika mazungumzo hayo, Mheshimiwa Waziri alimshukuru Dkt. Alkhalifa kwa kuidhinisha miradi mbalimbali inayotekelezwa nchini Tanzania kwa mikopo na misaada kutoka Mfuko wa OPEC.

Mheshimiwa Balozi Kombo alithibitisha dhamira ya dhati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuendelea kushirikiana na Mfuko katika kutekeleza miradi mbalimbali ya kipaumbele ikiwemo nishati hususan nishati safi ya kupikia, miundombinu ya usafirishaji, afya, elimu na kilimo.

Dkt. Alkhalifa alipongeza jitihada zinazofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuletea maendeleo wananchi kupitia miradi mbalimbali ya kipaumbele.

Aidha, aliahidi kwa niaba ya Mfuko kuendeleza ushirikiano mzuri uliopo Kati ya Tanzania na Mfuko wa OPEC na kuifanya Tanzania kielelezo cha ushirikiano wa mfano barani Afrika.

Kwenye mazungumzo hayo, Mheshimiwa Balozi Kombo aliambatana na Mhe. Saada Salum Mkuya, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Prof. Adolf Mkenda (Mb.), Waziri wa Elimu, Sayansi na Taknolojia; Mhandisi Felchesmi Mramba, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Prof. Carolyne Nombo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Taknolojia, na Bw. Rished Bade, Kamishna wa Fedha za Nje kutoka Wizara ya Fedha.
well done waziri Kombo 🐒
 
Back
Top Bottom