Habari za Zanzibar
JF-Expert Member
- Dec 18, 2024
- 651
- 433
Wakati wa kuingia katika ukumbi wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) jijini New York, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio, akiwa pamoja na First Lady wa Marekani, Melania Trump, na ujumbe wa Marekani, alisimama kumsalimia Mheshimiwa Dkt. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Rubio na Waziri Kombo walisalimiana kabla ya kuelekea kwenye maeneo yao ya kuketi, katika tukio lililojiri wakati viongozi na wajumbe kutoka mataifa mbalimbali wakiwasili ukumbini kushiriki Mjadala Mkuu wa Mkutano wa 81 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Salamu hiyo kati viongozi hao imeonekana kuwa ishara ya ukaribu na mahusiano ya kidiplomasia kati ya Marekani na Tanzania yanayojengwa na viongozi katika jukwaa hilo la kimataifa.
📹 - Real America's Voice