Waziri Kombo asimulia Madereva 75 wa Tanzania walivyofeli kuendesha magari Qatar

Waziri Kombo asimulia Madereva 75 wa Tanzania walivyofeli kuendesha magari Qatar

Mhh pana kitu hakipo sawa hawa madereva wanaoenda DRC uwape truck ipi watashindwa kuendesha..
 
Kwanini madereva wenyewe hawajahojiwa tuwasikie wanasemaje?

mbona sijasikia wakifeli kuendesha Trucks kule USA ama Canada?

This is a pure scam and news hype
Nchi nyingi za Kiarabu wao LHD sasa wewe umezoea RHD kwa ghafla ghafla lazina ufeli kwenye test.
Inanikumbusha enzi zile gari za automatic zinaanza kuingia.
Kuna fundi alitakiwa akachukue gari sehemu aipele gereji, fundi akamtuma fundi mwenzake.
Kufika ikamshinda kuiondoa yeye alisha zoea manual ikabidi mhusika mwenyewe ndio aje kuichukua.
 
Hili ni kosa moja kwa moja la Serikali na NIT; ni kwamba hawakufundisha watu kitu kilichopo sasa.., Pia hata yule aliyewapeleka je hakujua wanawapeleka kuendesha magari ya aina gani ?

Nadhani Waziri hapo amesema kabisa tatizo lipo wapi kwa upande huu (NIT) lakini kwa ujumla tatizo ni kubwa zaidi (kwa nyanja zote)
 
View attachment 3332337
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo akisimulia mkasa wa Maderva wa Tanzania walivyokwama kuendesha magari Qatar licha ya kuwa ni wahitimu wa Chuo cha NIT, alisema hayo Mei 7, 2025 alipokutana na Wahariri wa Vyombo vya Habari, Dar es Salaam.


==================================​

WAZIRI KOMBO AKUTANA NA WAHARIRI DAR, AELEZA MWELEKEO MPYA WA SERA YA MAMBO YA NJE

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo, amekutana na Wahariri wa vyombo vya Habari na kuelezea mwelekeo mpya wa Sera ya Mambo ya Nje Toleo la Mwaka 2024, ambayo ni muendelezo wa sera ya mwaka 2001 na kuongeza kuwa maboresho hayo, yamelenga kuiwezesha Tanzania kukabiliana na changamoto za wakati uliopo na wakati ujao katika nyanja za kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Akizungumza katika mkutano na wahariri wa vyombo vya habari uliofanyika jijini Dar es Salaam, Balozi Kombo ameeleza kuwa maboresho hayo yamelenga kulinda maslahi ya taifa kwa msingi wa uhuru, haki za binadamu, demokrasia, ujirani mwema, na diplomasia ya uchumi na kuongeza kuwa maboresho hayo yamejikita kuimarisha ushirikiano wa kikanda na kimataifa, kushirikisha diaspora, kukuza matumizi ya lugha ya Kiswahili kama bidhaa ya taifa, kuingiza masuala ya mazingira, jinsia, vijana, na uchumi wa buluu.

Amebainisha kuwa mafanikio ya utekelezaji wa sera ya mambo ya nje ambayo aliyataja kuwa ni pamoja na kuimarika kwa ujirani mwema na ushirikiano wa kimataifa na kuongeza kuwa kulikuwepo na changamoto kama uhalifu wa mipakani, ukosefu wa mwongozo kwa diaspora, na kutotumika vya kutosha kwa Kiswahili.

Amesema Sera ya Mambo ya Nje toleo la mwaka 2024 itazinduliwa rasmi tarehe 19 Mei 2025 na utekelezaji wake unahusisha wadau mbalimbali, ukiwemo mkakati mahsusi wa kushirikisha Watanzania waishio nje, kukuza utalii, kuongeza masoko ya bidhaa, na kuimarisha ushawishi wa Tanzania kimataifa.

Amesema utekelezaji wa Sera ya Mambo ya Nje ya mwaka 2001 imeleta manufaa kwa nchi na kutaja manufaa hayo kuwa ni Pamoja na kuimarika kwa ujirani mwema, kuimarika kwa ushirikiano wa kikanda na kimataifa, kushika nafasi za uongozi katika taasisi za kimataifa, na Tanzania kuwa mwenyeji wa taasisi za kikanda na kimataifa.

Amesema maboresho hayo yamelenga kuongeza uzingatiaji wa mila na Katiba, kuweka mfumo wa uratibu wa mikataba, kushirikisha diaspora wa Tanzania, kutumia Kiswahili kama bidhaa, na kuingiza masuala ya uchumi wa buluu, mazingira, jinsia na vijana.
Waziri kaongea ukweli na uhalisia. Suluhisho ni Vyuo kuwekeza kwenye Technolojia ili kuendana na wakati.

GCC Countries kwa dereva yoyote hata wa gari ndogo lazima afanye tena mafunzo na mtihani ili apewe leseni ya nchi hiyo. Inasaidia kumuandaa dereva kuweza kutumia njia na sheria za barabarani, Hivyo umakini unatakiwa wa kuibadili akili kujua kuwa hapa kwetu tunaendesha kutumia upande wa kushoto na wao wanatumia upande wa kulia. Mtihani wao wa Leseni ya Udereva unafanya mara nne. 1. Traffic Sign. 2. Drum Test 3. Slope Test 4. Road Test. Na yote lazima ufaulu. Baadhi ya nchi za GCC wanakupa leseni ya uangalizi ya mwaka mmoja ambayo dereva unatakiwa usifanye makosa barabarani, ukifanya unarudi kusoma tena.

Waziri katupa fundisho kuwa sio madereva tu hata wafanyakazi wengine kabla ya kuingia kwenye soko la ajira basi tujitahidi kujua nchi unayokwenda inahitaji ujuzi na maarifa gani kulingana na Technolojia ya sasa.
 
Madereva wa malori wapatao 75 wamerejeshwa nchini kutokea nchini Qatar baada ya kufeli majaribio ya kuendesha malori yaliyotengenezwa kwa teknolojia ya kisasa.

Hii inatokana na ukweli kwamba shughuli ya uendeshaji magari makubwa nchini Tanzania hufanywa zaidi na watu waliopata elimu ya msingi pekee.


 
Wamezoea kuenda scania 113 chuma za kufeli breki, akipotea njia anashuka kuulizia njia , gari za GPS atawezea wapi.
 
Wamezoea kuenda scania 113 chuma za kufeli breki, akipotea njia anashuka kuulizia njia , gari za GPS atawezea wapi.
Mkuu, na wewe una amini kwamba hizo Scania 113 huaga zina feli break? Usidanganywe na madereva, waongo
 
Mkuu, na wewe una amini kwamba hizo Scania 113 huaga zina feli break? Usidanganywe na madereva, waongo
Nafanya biashara ya logistics kwahiyo naelewa kuliko madereva wanavyoelewa, hizo 113 tatizo lake kubwa ni kufeli breki
 
Nafanya biashara ya logistics kwahiyo naelewa kuliko madereva wanavyoelewa, hizo 113 tatizo lake kubwa ni kufeli breki
Majority ya ajali nyingi kaka za mabasi or malori, chunguza vizuri; break hazi fail zenyewe, zinasababishwa na poor driving ya madereva wetu; they don't select proper gear at the right places; kwenye mteremko mkali, dereva anataka kuweka neutral ili abane matumizi ya mafuta, or gear aliokua anatembelea kwenye tambarare say No 3 hadi 4 or 5 halafu gari lina mzigo, gari inaanza ku accelerate kwa gravity, ukikanyaga break zita fail cause gear inaipa support break always. Now talk to your drivers waache kuiba mafuta, waendeshe gari sawa sawa na design, neutral sio proper, neutral tembelea gari ndogo na iwe haina mzigo, likiwa na mzigo nalo Lita fail break tu
 
Madereva wa Mabus wangefaulu Ukizingatia Bus kama Tahmeed anatumia Scania za kisasa full automatic gear burton tu... Volvo Lorry zile za Bakhera nakumbuka zilikuwa Auto ziendazo DRC
 
Kwanini madereva wenyewe hawajahojiwa tuwasikie wanasemaje?

mbona sijasikia wakifeli kuendesha Trucks kule USA ama Canada?

This is a pure scam and news hype

huko Us na Canada mpaka ukapata hiyo ajira ni tayari umeshakidhi vigezo vya huko kwao, fahamu hizo ajira hazitoki Canada zikaja bongo direct, ni tofauti kabisa na hii kesi.
 
Magari ya huko yanatofauti gani na ya bongo au ni lugha gongana.

Isijekuwa walibebwa UVCCM na vyeti vya "Baba kanituma".

mkuu tatizo sio gari, moja ya tatizo kubwa la wabongo ni nidhamu kwenye barabara
 
Waziri katupa fundisho kuwa sio madereva tu hata wafanyakazi wengine kabla ya kuingia kwenye soko la ajira basi tujitahidi kujua nchi unayokwenda inahitaji ujuzi na maarifa gani kulingana na Technolojia ya sasa.
Uko sahihi lazina kujua matarajio ya mwajiri kule uendako
 
Back
Top Bottom