Waziri Kombo awapa siri 3 za mafanikio wahitimu wa Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim

Waziri Kombo awapa siri 3 za mafanikio wahitimu wa Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,278
Reaction score
797
Waziri Kombo awapa siri 3 za mafanikio wahitimu wa Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo (Mb.) amewatunuku vyeti wahitimu 893 wa ngazi mbalimbali za masomo katika Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim na kuwausia mambo muhimu yatakayowasaidia katika maisha baada ya kuhitimu.
mini_magick20241214-44665-ubmg5p.jpg

Akihutubia wakati wa Mahafali hayo ya 27, Waziri Kombo amewaeleza wahitimu kuwa yapo mambo ambayo endapo watayafuata wataweza kufanikiwa katika sekta yoyote watakayobahatika kufanya kazi. Mambo hayo ni pamoja na; kuwa na dhamira thabiti ‘determination’ katika utekelezaji wa majukumu, kuwa na shauku ‘passion’ na majukumu yao pamoja na kujidhatiti katika utekelezaji wa majukumu ili kuyakamilisha kwa ufanisi na weledi.
mini_magick20241214-44665-skdfv8.jpg

Waziri Kombo amewataka pia kuwa jasiri katika kujieleza kwani wana nafasi nzuri ya kuwa mabalozi wazuri wa Tanzania ndani na nje ya nchi. Amewataka wawe na ujuzi wa kubishana kwa hoja kwani ni moja ya mambo muhimu katika Uhusiano wa Kimataifa na Diplomasia.

“Kubishana si utovu wa nidhamu. Kubishana kwa hoja ni jambo muhimu sana,” amesema Waziri Kombo.
mini_magick20241214-44665-j13iek.jpg

Ameeleza kuwa Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim sasa kinashirikiana na chuo cha diplomasia kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu kijulikanacho kama ‘Anwar Gargash Diplomatic Academy’ kwa lengo la kuanza kubadilishana wanafunzi na ujuzi katika mafunzo ya diplomasia.
mini_magick20241214-44665-cj0prz.jpg

Wahitimu wametakwa pia kujielimisha na kuzifahamu vyema ajenda zote za nchi ikiwemo ile ya Jenga Kesho iliyo Bora katika Kilimo, Ajenda 2050 inayolenga kufikia maendeleo endelevu ya kiuchumi na kijamii na hadhi ya kipato cha juu ifikapo 2050, Ajenda ya Nishati Safi ya Kupikia na vipaumbele mbalimbali vya nchi kwa kutumia elimu waliyoipata kama sehemu ya kutatua changamoto mbalimbali za kitaifa.
mini_magick20241214-44665-deft4e.jpg
 

Attachments

  • mini_magick20241214-44665-h105cm.jpg
    mini_magick20241214-44665-h105cm.jpg
    85.2 KB · Views: 4
  • mini_magick20241214-44665-zyjbcw.jpg
    mini_magick20241214-44665-zyjbcw.jpg
    66.7 KB · Views: 4
  • mini_magick20241214-44665-1p9vz3.jpg
    mini_magick20241214-44665-1p9vz3.jpg
    124.8 KB · Views: 4
  • mini_magick20241214-44665-w8i55v.jpg
    mini_magick20241214-44665-w8i55v.jpg
    126.8 KB · Views: 3
  • mini_magick20241214-44665-kwg4km.jpg
    mini_magick20241214-44665-kwg4km.jpg
    158.5 KB · Views: 3
Back
Top Bottom