Waziri Kombo Awasilisha Ujumbe Maalum wa Rais Samia kwa Mwanamfalme wa Saudi Arabia

Waziri Kombo Awasilisha Ujumbe Maalum wa Rais Samia kwa Mwanamfalme wa Saudi Arabia

Habari za Zanzibar

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2024
Posts
651
Reaction score
433
Waziri Kombo Awasilisha Ujumbe Maalum wa Rais Samia kwa Mwanamfalme wa Saudi Arabia.
============
Waziri Kombo Awasilisha Ujumbe Maalum wa Rais Samia kwa Mwanamfalme wa Saudi Arabia
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb) akiambatana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Profesa Palamagamba Kabudi (Mb) amewasilisha ujumbe maalum kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Mwanamfalme na Waziri Mkuu wa Saudi Arabia Mtukufu Mohammed bin Salman Al Saud.

Ujumbe huo umepokelewa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufalme wa Saudi Arabia na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufalme huo, Mheshimiwa Waleed bin Abdulkarim El Khereiji.

Akipokea ujumbe huo, Mheshimiwa Waleed Abdulkarim El Khereiji aliongelea kutambua na kuthami uhusiano wa muda mrefu na imara wa kidiplomasia, kibiashara na kiutamaduni uliopo kati ya Ufalme wa Saudi Arabia na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aidha, aliahidi kuwa Ufalme wa Saudi Arabia utaendelea kushirikiana kwa karibu na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuimarisha zaidi uhusiano huo, hususan katika maeneo ya vijana, utamaduni, biashara, uwekezaji, utalii, elimu, ajira na maeneo mengine yaliyoafikiwa na nchi hizo mbili.

Alieleza dhamira ya Ufalme wa Saudi Arabia kuunga mkono jitihada za uwezeshaji wa vijana zilizowekwa na Serikali ya Tanzania na kuwasilishwa na Waziri Kombo.
Imetolewa na:

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

IMG-20251224-WA0026.jpg
 
Back
Top Bottom