Waziri Lugola: Aliyekuwa Mkurugenzi NIDA, Dickson Maimu na Jack Gotham wasipoitikia wito ‘watapata tabu sana’

Waziri Lugola: Aliyekuwa Mkurugenzi NIDA, Dickson Maimu na Jack Gotham wasipoitikia wito ‘watapata tabu sana’

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,722
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola ameipa wiki mbili kampuni ya Kimataifa ya Iris Corporation Berhard impe majibu ya kuwa italeta mtambo wa kutengeneza kadi ghafi au Dola za Marekani Milioni 14 sawa na zaidi ya shilingi bilioni 32 za Tanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa Wizara, Dodoma leo,baada ya kikao na Menejimenti ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA)na viongozi wa Kampuni hiyo, Waziri Lugola alisema kampuni hiyo haiwezi ikacheza na fedha za Watanzania na walipa kodi.

Lugola aliongeza kuwa lazima fedha hizo au mtambo huo upatikane kwa kuwa Serikali ya Awamu ya Tano haitakubaliana na mchezo mchafu wa aina yoyote, na pia yeye kama Waziri wa Wizara hiyo anaendelea kutekeleza maagizo ya Rais Dkt John Magufuli. “Tumezungumza nao na tumekubaliana

Aidha, Waziri Lugola amewataka wamiliki wa kampuni zilizolipwa kifisadi fedha za Mradi wa mtambo wa NIDA kujisalimisha jijini Dodoma Agosti 3 mwaka huu wakiwa na mtambo huo vinginevyo warejeshe fedha zilizotumika.

Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amesisitiza kuwa kutokana na wito alioutoa kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa NIDA, Dickson Maimu pamoja na Jack Gotham kufika ofisini kwake, wasifanye jaribio la kutokuitikia wito huo, kwani wakifanya hivyo watapata tabu sana.

Di95rm6WwAIZR5O.jpg
 
Maagizo mengi, ngoja tusubirie mrejesho.

Tafadhari tusikimbiane wala kutishana pale mrejesho utakapo hitajika.
 
hizo njemba zilizo nyoa kipara hapo niakina nani? mbona kama....
 
kama vipi Lugola waamrishe na takukuru wachunguze zilipo 1.5T, umeteuliwa juzi tu hivyo "jiwe" hawezi kukutumbia maana itaonekana yeye ndio mwenye "issues" na sio nyie mawaziri
 
Lugola naye kazidi kwa matamko yake sasa. Kila siku anakuja na mpya. Ya awali ameshayatekeleza?

Hana tofauti na Aggrey Mwanri RC wa Tabora ambaye akifika site hufoka mno lakini utekelezaji zero.

Lugola mpaka sasa amerukia rukia mambo mengi lakini sioni anachofanikiwa zaidi ya kutoa masaa kadhaa lakini baada ya hapo hurukia mengine.
 
Kwani Yule mbwa wa Bandarini hajapatikana .....!!!?
 
Back
Top Bottom