Waziri Lugola: Wizara haihusiki na kupotea kwa Mwandishi wa Kampuni ya Mwananchi Communication Limited, Azory Gwanda

Kwa hiyo mtu akitoweka kwa namna hiyo na familia wakaripoti polisi, si kazi ya polisi kusaidia kumtafuta? kazi ya polisi ni nini sasa!! hadi wapate ushahidi kuwa ametekwa ndio wamtafute?
 
Ndo hivo mkuu!kawaida ni kama sheria, hatujawah kuwa na utaratibu wa polis kutafuta waliopotea Bali ni kutoa taarifa polisi na ndugu au wahusika wenyewe kuendelea kumtafuta ndugu yao.Ila kama ni swala la kutekwa hapa polisi inatakiwa ipambane kuhakikisha wanajua nani kafanya hivo.Kupotea sio uhalifu kama kutekwa na ndo nafikir ni sababu kwanini police huwa hawaangaiki kutafuta watu waliopotea zaid huwa naona kwenye magazeti,TV na sehem mbalimbali watu wakiwatafuta ndugu zao.Kwa kesi ya Azory kama kaondoka nyumbani na haijulikani kaenda wapi au katekwa sioni hoja za mcng za kutaka ufafanuzi kutoka serikalini.Kama alitekwa basi serikali inatakiwa ije na majibu nani wamemteka.Niulize swali Azory katekwa au kapotea?
 
Kwa hiyo mlitaka Waziri aseme mnayotaka nyie kuyasikia? ameongea fact kuwa mtu katoka kwake akiwa na suti yake, katelekeza familia kakimbia. Mnataka wizara ifanye nini sasa? Kuweni na akili mapoyoyo nyie
Umeamua kujitoa ufahamu kwa makusudi
 
Lini ulisikia polisi wanafanya kazi ya kuwatafuta waliopotea? Mara kibao wanawatangaza kwenye ITV waliopotea, Je ushawah ona polisi wanawatafuta?Huu utaratibu wa polis kutafuta wanaopotea umeanza Lini?Mimi mwenyewe ni mhanga wa hili,mdogo wangu alitoweka tu nyumbani tukatoa taarifa polisi basi na sisi ndugu kuendelea kumtafuta sio polis kumtafuta.Huu ni utaratibu ambao upo na unajulikana,huku kwa Azory mnaleta siasa UCHWARA kutaka kufanya hili ni jukum la polis kumtafuta aliyepotea.Pita huko mitaani kuna mabango kibao ya watu wakiwatafuta ndugu zao na hili halijaanza awam hii,ni miaka nenda rudi iko hivo.Mngekua na hoja za mcng kama mngesema katekwa coz Huu sasa ni uharifu na hapa polisi ilitakiwa iwajibike kuhakikisha inagundua ni akina nani wamefanya Huu uharifu.Sio kazi ya serikali kutafuta waliopotea
 
Jeshi la polisi kazi yake ni nini??

Na jeshi la polisi lipo chini ya wizara gani?
Elewa hoja,huyo hajapotea na hilo tukio sio la kiuharifu.serikali haiwez deal na mambo binafsi ya watu.Ungesema katekwa sawa.
 
Taarifa ya kupotea ndugu yako ulitoa Polisi, na polisi iko chini ya wizara gani? Kama hivyo vyombo havihusiki kwa nini tunaripoti huko?
Nilitoa taarifa sio kwamba wanisaidie kumtafuta,inaweza kapotea na akapatikana sehem kauawa au kajinyonga so hii taarifa inaweza kusaidia hata ktk upelelezi lkn usipotoa taarifa na huyo aliyepotea akapatikana sehem na yuko ktk mattz basi ndugu kuna namna mtawajibika tu.So hatuendi polisi kutoa taarifa kwa lengo la polis wawajibike kumtafuta.
 
Kwa hiyo mtu akitoweka kwa namna hiyo na familia wakaripoti polisi, si kazi ya polisi kusaidia kumtafuta? kazi ya polisi ni nini sasa!! hadi wapate ushahidi kuwa ametekwa ndio wamtafute?
Yah sio kazi ya polisi kumtafuta.Ila kama taarifa ni kuwa katekwa hapa polisi lzm wawajibike kuwatafuta watekaji.
 
Yah sio kazi ya polisi kumtafuta.Ila kama taarifa ni kuwa katekwa hapa polisi lzm wawajibike kuwatafuta watekaji.
Utajuaje kama katekwa au kaamua kuondoka mwenyewe bila ya uchunguzi. Nini kinafanya polisi wajue mtu katekwa. Niikiitwa kwenye dili na wafanyabiashara wenzangu, then wakanigeuka kunipoteza kwa sababu ya tofauti zetu za kibiashara polisi hawatofatilia kwa kuwa niliondoka mwenyewe nyumbani?
 
Taarifa iliyopo ni kapotea
 
Kwa hiyo mtu akitoweka kwa namna hiyo na familia wakaripoti polisi, si kazi ya polisi kusaidia kumtafuta? kazi ya polisi ni nini sasa!! hadi wapate ushahidi kuwa ametekwa ndio wamtafute?
Wengi wanatoweka majumbani kwao kwasababu moja au nyingine si jukumu la polisi kufuatilia mtu aliyetoweka nyumbani kwake hapo elewa vizuri sheria za nchi.Wengi tu wanaasi familia zao na kukimbilia sehemu zingine kutafuta maisha.Wengi wapo migodini na familia zao hazijui na wengine hata kumaliza matanga kumbe watu wako hai sehemu zingine.Polisi inashughulika na uhalifu.
 
Watanzania tumemkosea nini mungu
 
...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…