Waziri Lugola: Wizara haihusiki na kupotea kwa Mwandishi wa Kampuni ya Mwananchi Communication Limited, Azory Gwanda

Waziri Lugola: Wizara haihusiki na kupotea kwa Mwandishi wa Kampuni ya Mwananchi Communication Limited, Azory Gwanda

Tehehe [emoji16][emoji16] hehe!nimependa hilo jibu kwa kweli.[emoji106][emoji106][emoji106]
 
Kuna shda wapi jamani naona km tunaenda wrong direction kwa speed kubwa
Tena huyu ndio hamna kitu kabisa!!kwani yeye anataka kujifanya kuiga akili za jiwe!!na kuwa ndio soln ya matatizo yote kwnye wizara,akikutana na akili za yule mzee wa WATAPATA TABU SANA!!ndio itakuwa balaa
 
Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amesema wizara hiyo haihusiki na kupotea kwa mwandishi wa habari wa kampuni ya Mwananchi Communication Limited (Ltd), Azory Gwanda.

Kangi ametoa kauli hiyo, leo Ijumaa Julai 6, 2018 wakati wa mkutano wake na wanahabari uliofanyika Ofisi ndogo ya wizara hiyo jijini Dar es Salaam.
Waziri huyo ameeleza hayo baada ya kuulizwa swali na mwandishi wa habari aliyetaka kujua mkakati wa Lugola kuhusu kupotea kwa Gwanda tangu Novemba mwaka jana.

Swali: Mheshimiwa waziri hivi karibuni kumekuwa matukio ambayo sisi waandishi wa habari yanatusumbua mojawapo ni kupotea kwa mwanahabari mwenzetu, Gwanda ambaye bado hajaonekana tangu atoweke Novemba mwaka jana.

Polisi wanasema bado hawajachunguza kwa kina. Nini kinachoendelea, hili unalizungumziaje ili waandishi wa habari tufanye kazi katika mazingira salama bila kubughudhiwa.

Lugola: Zipo hizo habari. Mtu yupo nyumbani kwake halafu ametoweka. Sisi mambo ya ndani hatuingilii uhuru wa mtu kutoweka nyumbani kwake. Kila mtu ana uhuru kwa mujibu wa Katiba ya nchi anaweza kutoka sehemu moja kwenda nyingine bila kuvunja sheria.

Waziri Lugola alisema kama Gwanda alitoweka wakati akiwa nyumbani, wao hawahusiki bali wanahusika na mtu aliyetendewa uhalifu ikiwamo kutekwa, akisema katika tukio kama hilo vyombo vya dola humtafuta mtekaji.

“Hawa ambao wanatoweka kwao tu, wanakuwa na sababu nyingi. Kuna wengine maisha yakiwashinda anaamua kwenda kwingine,” alisema.

Lugola alieleza uzoefu wake alipotembelea migodi wakati akiwa Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).

"Kwenye migodi nilikutana na watu ambao kwao walishaweka matanga kwa kujua wameshakufa. Kwao hawaonekani, lakini kumbe wametoweka," alisema Lugola

Lugola ameeleza kuwa hicho ndicho anachoweza kusema kwa sasa kuhusu kutoweka kwa Gwanda.

Jeshi la Polisi, ambalo jukumu lake kubwa ni kulinda watu na mali zao, liko chini ya Wiuzara ya Mambo ya Ndani.

Hii awamu ina viongozi wa ajabu sana haijapata kutokea. Sasa kama hawahusiki na watu kutoweka wamemkamatia nn Abdul Nondo na wamempelekea nn mahakamani? Maana kwa majibu yake wizara haihusiki sasa kwann kwa Nondo wamehusika?
 
Sio hoja ya mcng kujua kuandika majina ya watu,ebu niambie ni lini wizara iliwajibika kwa kupotea kwa mtu?Nilikua na ndugu yangu alikua anaondoka tu nyumbani na haieleweki kaenda wapi.Kilichokua kinafanyika ni kutoa tu taarifa kuna ndugu yetu kapotea yuko hivi na hivi,hakuna cha kusema polisi wakamtafute wala nn.na iko hivo.Watu wengi wakipotea tumeona matangazo yakibandikwa kwa ajili ya kuwatafuta.Ingekua ni habari nyingine kama mngesema katekwa,lkn bado hoja itakuja huyo alikua anafanya kitu gani cha kusababisha atekwe? Nini uhusiano wake na hao waliomteka.
Taarifa ya kupotea ndugu yako ulitoa Polisi, na polisi iko chini ya wizara gani? Kama hivyo vyombo havihusiki kwa nini tunaripoti huko?
 
Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Kangi Lugola amesema watu walioripotiwa kupotea hawajatekwa bali huenda wametoweka kwa sababu ya ugumu wa maisha. Kangi alikuwa akijibu swali kuhusu taarifa za kupotea kwa watu mbalimbali nchini katika mazingira ya kutatanisha akiwemo mwandishi wa gazeti la Mwananchi Azory Gwanda na msaidizi wa Mwenyekiti wa Chadema Ben Saanane. Lugola amesema serikali haiwezi kuingilia sana maisha ya watu binafsi kwa sababu huenda wametoweka kwenda kutafuta maisha. Amesema hii si mara ya kwanza watu kutoweka katika jamii zao kwenda kutafuta maisha mahali kwingine na wanapofanikiwa hurejea.!

Nini maoni yako?
 
huyo ndiyo Ninja,mtegemee mabaya zaidi naye si alikuwa polisi Nchi yangu Tanzania do!!!
 
Kwa hiyo mlitaka Waziri aseme mnayotaka nyie kuyasikia? ameongea fact kuwa mtu katoka kwake akiwa na suti yake, katelekeza familia kakimbia. Mnataka wizara ifanye nini sasa? Kuweni na akili mapoyoyo nyie
 
Majibu kama hayo niyakawaida sana kwa matukio kma hayo kwani uhalisia wa jambo unafahmika
Aisee Faru john junior,unachosema kwa mwenye akili atakuelewa maana yako, lkn asiejua atakulaumu,lkn ukweli ndio huo,uhalisia wa Jambo hili unafahamika,kwa hiyo jibu hilo kutolewa na Waziri wa mambo ya ndani ni kawaida
 
Kwa hiyo mlitaka Waziri aseme mnayotaka nyie kuyasikia? ameongea fact kuwa mtu katoka kwake akiwa na suti yake, katelekeza familia kakimbia. Mnataka wizara ifanye nini sasa? Kuweni na akili mapoyoyo nyie
Nyie mnaofikiria kwa kutumia makalio ni Shida katika hii dunia,yaani jitu linaandika upuuzi humu kama lilivyo lipuuzi.
 
Aisee Faru john junior,unachosema kwa mwenye akili atakuelewa maana yako, lkn asiejua atakulaumu,lkn ukweli ndio huo,uhalisia wa Jambo hili unafahamika,kwa hiyo jibu hilo kutolewa na Waziri wa mambo ya ndani ni kawaida
Da kama ni mwanafunzi basi kila siku chakula cha mchana unakula kwangu kwa jinsi ulivyonielewa umetumia akili za ziada
 
Afu ndio nasikia alikua polisi huyu
Kwani hajui unaweza tekwa ukiwa kwako ?
Imagine mtu yupo kwake usiku anatumiwa text na mtu anayemfahamu kuwa wakutane getini then asirudi
 
Back
Top Bottom