Malata Junior
JF-Expert Member
- Nov 29, 2011
- 3,104
- 2,550
Tumetoa afadhali tukaweka potelea mbali!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tena huyu ndio hamna kitu kabisa!!kwani yeye anataka kujifanya kuiga akili za jiwe!!na kuwa ndio soln ya matatizo yote kwnye wizara,akikutana na akili za yule mzee wa WATAPATA TABU SANA!!ndio itakuwa balaaKuna shda wapi jamani naona km tunaenda wrong direction kwa speed kubwa
Hii awamu ina viongozi wa ajabu sana haijapata kutokea. Sasa kama hawahusiki na watu kutoweka wamemkamatia nn Abdul Nondo na wamempelekea nn mahakamani? Maana kwa majibu yake wizara haihusiki sasa kwann kwa Nondo wamehusika?Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amesema wizara hiyo haihusiki na kupotea kwa mwandishi wa habari wa kampuni ya Mwananchi Communication Limited (Ltd), Azory Gwanda.
Kangi ametoa kauli hiyo, leo Ijumaa Julai 6, 2018 wakati wa mkutano wake na wanahabari uliofanyika Ofisi ndogo ya wizara hiyo jijini Dar es Salaam.
Waziri huyo ameeleza hayo baada ya kuulizwa swali na mwandishi wa habari aliyetaka kujua mkakati wa Lugola kuhusu kupotea kwa Gwanda tangu Novemba mwaka jana.
Swali: Mheshimiwa waziri hivi karibuni kumekuwa matukio ambayo sisi waandishi wa habari yanatusumbua mojawapo ni kupotea kwa mwanahabari mwenzetu, Gwanda ambaye bado hajaonekana tangu atoweke Novemba mwaka jana.
Polisi wanasema bado hawajachunguza kwa kina. Nini kinachoendelea, hili unalizungumziaje ili waandishi wa habari tufanye kazi katika mazingira salama bila kubughudhiwa.
Lugola: Zipo hizo habari. Mtu yupo nyumbani kwake halafu ametoweka. Sisi mambo ya ndani hatuingilii uhuru wa mtu kutoweka nyumbani kwake. Kila mtu ana uhuru kwa mujibu wa Katiba ya nchi anaweza kutoka sehemu moja kwenda nyingine bila kuvunja sheria.
Waziri Lugola alisema kama Gwanda alitoweka wakati akiwa nyumbani, wao hawahusiki bali wanahusika na mtu aliyetendewa uhalifu ikiwamo kutekwa, akisema katika tukio kama hilo vyombo vya dola humtafuta mtekaji.
“Hawa ambao wanatoweka kwao tu, wanakuwa na sababu nyingi. Kuna wengine maisha yakiwashinda anaamua kwenda kwingine,” alisema.
Lugola alieleza uzoefu wake alipotembelea migodi wakati akiwa Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).
"Kwenye migodi nilikutana na watu ambao kwao walishaweka matanga kwa kujua wameshakufa. Kwao hawaonekani, lakini kumbe wametoweka," alisema Lugola
Lugola ameeleza kuwa hicho ndicho anachoweza kusema kwa sasa kuhusu kutoweka kwa Gwanda.
Jeshi la Polisi, ambalo jukumu lake kubwa ni kulinda watu na mali zao, liko chini ya Wiuzara ya Mambo ya Ndani.
Taarifa ya kupotea ndugu yako ulitoa Polisi, na polisi iko chini ya wizara gani? Kama hivyo vyombo havihusiki kwa nini tunaripoti huko?Sio hoja ya mcng kujua kuandika majina ya watu,ebu niambie ni lini wizara iliwajibika kwa kupotea kwa mtu?Nilikua na ndugu yangu alikua anaondoka tu nyumbani na haieleweki kaenda wapi.Kilichokua kinafanyika ni kutoa tu taarifa kuna ndugu yetu kapotea yuko hivi na hivi,hakuna cha kusema polisi wakamtafute wala nn.na iko hivo.Watu wengi wakipotea tumeona matangazo yakibandikwa kwa ajili ya kuwatafuta.Ingekua ni habari nyingine kama mngesema katekwa,lkn bado hoja itakuja huyo alikua anafanya kitu gani cha kusababisha atekwe? Nini uhusiano wake na hao waliomteka.
Aisee Faru john junior,unachosema kwa mwenye akili atakuelewa maana yako, lkn asiejua atakulaumu,lkn ukweli ndio huo,uhalisia wa Jambo hili unafahamika,kwa hiyo jibu hilo kutolewa na Waziri wa mambo ya ndani ni kawaidaMajibu kama hayo niyakawaida sana kwa matukio kma hayo kwani uhalisia wa jambo unafahmika
Nyie mnaofikiria kwa kutumia makalio ni Shida katika hii dunia,yaani jitu linaandika upuuzi humu kama lilivyo lipuuzi.Kwa hiyo mlitaka Waziri aseme mnayotaka nyie kuyasikia? ameongea fact kuwa mtu katoka kwake akiwa na suti yake, katelekeza familia kakimbia. Mnataka wizara ifanye nini sasa? Kuweni na akili mapoyoyo nyie
Da kama ni mwanafunzi basi kila siku chakula cha mchana unakula kwangu kwa jinsi ulivyonielewa umetumia akili za ziadaAisee Faru john junior,unachosema kwa mwenye akili atakuelewa maana yako, lkn asiejua atakulaumu,lkn ukweli ndio huo,uhalisia wa Jambo hili unafahamika,kwa hiyo jibu hilo kutolewa na Waziri wa mambo ya ndani ni kawaida