Kuandika jina la mtu kwa usahihi ni ishara muhimu ya heshima. Nikushauri tu, uandishi ni kigezo kikubwa cha kupima ueledi na hekima.
Ninarudia tena, kazi ya jeshi la polisi ni kuhakikisha usalama wa kila raia ndani ya mipaka ya Tanzania. Kutokufanikisha wajibu huu, haimaanishi siyo wajibu wao. Ni kama mwalimu asipofundisha au kusahihisha mitihani mara kwa mara halafu hawajibishwi ukasema ni kawaida yake. Hilo ni kosa na halitakiwi kuzoeleka. Kuna taratibu za kuwajibisha serikali na ndio maana tuna Mahakama na Bunge ambazo zinatakiwa kusimamia serikali na taratibu zake. Kama hili halitendeki, basi tukubali tuna ombwe la uongozi. Swali, je tulikabili vipi hilo ombwe, ikiwa lipo?
Tukija kwa mwandishi Azory Gwanda: Ikiwa familia na mwajiri wametoa taarifa ya kutoonekana kwake, Polisi inawajibu wa kumtafuta. Aidha yuko salama au la, ni jambo la kutatua akishapatikana. Ikiwa ametekwa au la, hilo pia ni jukumu la Jeshi la Polisi kufuatilia. Ndio wenye mamlaka, ujuvi na wajibu.