Basi mimi ni mtakatifu ram, mimi huwa tunachangia nusu kwa nusu landlord na mpangaji π π πMara zote Kwenye hii biashara Mpangaji ndiye anamatafuta Dalali kumuomba amtafutie sehemu
Watuache kabisa sisi ma landlords
Namuuliza Dalali Kiongozi.
Kumbe sheria isipokuwepo inahalalisha dhambi kutamalaki? Hakunaga "Affirmative Action?"
Basi mimi ni mtakatifu ram, mimi huwa tunachangia nusu kwa nusu landlord na mpangaji π π π
Malipo makubwa kwa madalali yanaleta madhara ya watu kukosa nyumba au chumba, na wamiliki kukosa wapangaji.Ila mpangaji ndio humtafuta dalali ili apate huduma yake na wakati mwengine mwenye nyumba hata hamjui huyo dalali, sasa kwa mazingira hayo iweje mwenye nyumba ndio amlipe dalali?
Hili tusi litakuwa limetoka kwa dalali!70k ndiyo nini wewe fara?
Hawana uwezo wa kushughulikia mambo nyeti zaidi ya kurukia haya madogo. Hili swala linaumiza watafuta vyumba, lakini si la ngazi ya kushughulikia na waziri. Matokeo ndio miaka 60 ya uhuru mkuu wa nchi anaongelea madawati, madarasa, vyoo vya shule, visima vya maji, mikopo ya wanafunzi heslb nk.Nilikua namaanisha suala la udalali angeongelea hata mkuu wa wilaya au mtendaji ili waziri aangalie yale nyeti zaidi
Zalongwa mbali zatendwa mbaliHatimae wameuona huu ujambazi!! Afadhali.
Tatizo ni matamshi ambayo wakati mwingi hayana msingi wa kisheria. Matokeo ni washikwao inakuwa ni ulaji kwa polisi kwani hayapelekwi mahakamani. Rejea katazo la Magufuli kufungua bar mchana, sikuwahi sikia aliepelekwa mahakamani.Kwani lile la Wapangaji wasilipishwe kodi ya zaidi ya mwezi mmoja lilishapata ufumbuzi?.
Vyovyote ilivyo tukubaliane kuwa haiko kisheria na sasa tunahitaji utaratibu mzuri utakaolinda wateja wote wa pande mbili. Huduma ya kupanga ni kubwa mno iko kila mahali penye jamii ya watu.Wapangaji ndio huenda kuwaomba madalali wawatafutie nyumba za kupanga Sasa unataka mwenye nyumba amlipe kwa lipi?
Wewe unaenda kuomba huduma ya dalali halafu eti ohh mwenye nyumba amlipe kwa lipi wakati mkataba wa kikazi Ni wewe mtafuta nyumba ya kupanga mumeingia na dalali wako uliyemkuta kijiweni au popote kuwa nitafutie nyumba.Wewe ndio umlipe kwa hiyo huduma aliyokupa
IIeleweke wazi contract ya kikazi ya kutafuta nyumba Ni yako wewe na dalali wako sio mwenye nyumba
Waziri alivyoliweka haliko sawa kisheria .Watu wanaenda wenyewe kwa madalali kwa hiari yao bila shuruti na kuingia mikataba nao ya kutafuta nyumba at a fee of course ambayo Ni Kodi ya mwezi mmoja