Waziri Lukuvi apiga marufuku madalali kulipwa posho ya mwezi mmoja na wapangaji. Asema ni ujambazi

Waziri Lukuvi apiga marufuku madalali kulipwa posho ya mwezi mmoja na wapangaji. Asema ni ujambazi

Hela ya udalali inauma asee, yaani unatoa 70k hivi hivi kwa jamaa anayepiga stori kitaa na umeisotea asee.

Hatukatai madalali wana msaada ila wachukue asilimia flani.
Sasa Wewe mpangaji ndio una shida ya chumba unamtafuta dalali akutafutie chumba!anashinda anazurula anatumia gharama,simu,nauli,Ili akupatie chumba sehemu unayotaka,ni lazima alipwe.

Dalali ndio anatafuta chumba kwa ajiri ya mpangaji,au anatafuta mpangaji kwa ajiri ya mwenye nyumba.
Lazima alipwe na anayefanyiwa kazi.
 
Si kweli bali hii kazi ya udalali ni sawa na kubet tu, hebu fikiria kwamba et kisa unajua kwamba nyumba fulani kuna chumba kinapangishwa basi kiasi cha kumchukua mtu na kumpeleka tu et unapata kodi ya mwezi mzima kwa kazi kubwa ipi hapo?

Nakubali umuhimu wao madalali ila sio huo mfumo waliyouweka wa kutaka kodi ya mwezi mzima.
Nilikua namaanisha suala la udalali angeongelea hata mkuu wa wilaya au mtendaji ili waziri aangalie yale nyeti zaidi
 
Sasa mwenye nyumba hataki mpangaji aje mwenyewe unamuelewaje
Hao ni wachache ambao hufanya hivyo na ukiona hivyo ujue huyo mwenye nyumba anagawana hiyo hela ya udalali na huyo dalali.
Ndio madalali wengine wanamchukua mpangaji na kumpeleka hadi kwenye nyumba kama hiyo kisha anaishia kumuonesha kwa nje tu yani mpangaji aingie mwenyewe kujifanya anaulizia vyumba hajaja na dalali.
 
Sasa Wewe mpangaji ndio una shida ya chumba unamtafuta dalali akutafutie chumba!anashinda anazurula anatumia gharama,simu,nauli,Ili akupatie chumba sehemu unayotaka,ni lazima alipwe.

Dalali ndio anatafuta chumba kwa ajiri ya mpangaji,au anatafuta mpangaji kwa ajiri ya mwenye nyumba.
Lazima alipwe na anayefanyiwa kazi.

Sikatai kumlipa bali tunataka asilimia flani, Kodi ya mwezi hapana asee.
 
nawanamatumbo balaaaa ,Ila pango Kodi zitapandasana Mana wenyenyumba wataaza siunajua dalali Natakiwa kumlipa
 
Kwani lile la Wapangaji wasilipishwe kodi ya zaidi ya mwezi mmoja lilishapata ufumbuzi?.
 
Moja Lukuvi kapiga vazi mulua Sana,alipenda Sana baba wataifa,

Pili naunga mkono dalali achukue KWA mwenyenyumba ,japo alinichafua Kipindi flani ,ila KWA kauri hii namsamehe bure
 
Back
Top Bottom