Basi mimi ni mtakatifu ram, mimi huwa tunachangia nusu kwa nusu landlord na mpangaji 🙂 🙂 🙂
Kwangu hapana aisee Mimi ninachojali ni kodi yangu tu , ukilinilipa kadri ya makubaliano unahamia .
Dalali utajuana naye wewe mwenyewe ukiweza kumdhulumu sawa .
Kuna Dalali alileta Mpangaji kwangu Dalali mwenyewe hata simjui nadhani alipewa taarifa na madalali wenzake.
Mpangaji akapenda akalipa nikampa funguo akaja kuhamia alikuwa binti.
Siku mbili tatu Dalali ananifata eti nimrudishie yule binti hajamlipa. Atanitafutia mtu mwingine nikamkatalia nikamwambia fedha nishatumia akiweza atafute fedha arudishie yeye apangishe .
Sikumbili tatu nakutana na kale kajamaa kakaniambia yule binti alimpa hela nusu na pia alimpa papuchi so wamemalizana.
Ni kwangu madalali wanajua kabisa sanasana Kama nakujua nimekupa kaziimi mwenyewe umeniletea Mpangaji katoa kodi miezi 6 na kuendelea hata Kama kodi kwa mwezi laki 2 sanasana nampa elfu 10 au 20 ya soda.
Ni madalali wa kitaa siwashobokei kabisa nawapa kazi nawaambia wakichelewa tu natoa kazi mtandaoni hawapati hata shilingi.
Nilishatangaza napangisha sehemu yangu hapa JF na nikapata Mpangaji hakumlipa dalali yeyote .
Sipendi kutumia mitandao kutokana sipendi kujiexpose