Waziri Lukuvi apiga marufuku madalali kulipwa posho ya mwezi mmoja na wapangaji. Asema ni ujambazi

Waziri Lukuvi apiga marufuku madalali kulipwa posho ya mwezi mmoja na wapangaji. Asema ni ujambazi

Wakati mwingine madalali huwa wanazingua sana, anakuonesha nyumba halafu anakwambia hayupo peke yake yupo na wenzie, so lazima utoe pesa yakumtosha na wenzie hata kama hawapo eneo la tukio

Wenye nyumba nao wengine vichomi kama nini, anapangisha nyumba yake mjini, pesa ya udalali umpe dalali aliekupeleka kukuonesha nyumba, halafu nyingine umtumie na ndugu yake alieko kijijini eti nae ni dalali, upuuzi gani huu, nilirudishiwa pesa yangu baada ya kujua huu ujinga
 
Wanaopanga hawana shida kulipa maana si kazi rahisi kupata nyumba.

Sasa kama ni hivo dalali si anaweza kuongea na mwenye nyumba bei iwe juu ,kitu kile kile
Madalali ndo wanaongeza na kupanga bei za nyumba. Bei ikiwa juu wa napata pesa Yao ya mwezi kubwa ziaid
 
Lukuvi anafikiri kutafuta nyumba/chumba ugenini ni kazi rahisi sana

Kwani madalali & serikali iliyoweka tozo kwenye LUKU nani jambazi sugu
 
Waziri wa Ardhi, William Lukuvi amepiga marufuku Madalali kuwadai Wapangaji Fedha ya Mwezi Mmoja, akiita kitendo hicho kuwa ni ujambazi

Amesema, "Kuna baadhi ya Madalali wanapangisha nyumba halafu wanachukua kwa Wapangaji Kodi ya mwezi. Hawa wanaochukua pesa za wapangaji waache mchezo huo kwasababu ni wizi wa mchana kabisa. Wewe umeajiriwa na mwenye nyumba, yeye lazima akulipe wewe"

View attachment 2011900
Kitengo Cha watumishi wa CCM. Watakula wapi? Nilifukiri zile ajira 40, 000 na Hawa wamo kumbe ni majambazi? Stakafulluh!!!!!!!
 
Waziri wa Ardhi, William Lukuvi amepiga marufuku Madalali kuwadai Wapangaji Fedha ya Mwezi Mmoja, akiita kitendo hicho kuwa ni ujambazi

Amesema, "Kuna baadhi ya Madalali wanapangisha nyumba halafu wanachukua kwa Wapangaji Kodi ya mwezi. Hawa wanaochukua pesa za wapangaji waache mchezo huo kwasababu ni wizi wa mchana kabisa. Wewe umeajiriwa na mwenye nyumba, yeye lazima akulipe wewe"

View attachment 2011900
awaache tu, ni ugumu wa maisha, na wao wana familia za kutunza na hawana kipato kingine. bora hao hata kuturahisishia maisha wakati wa kutafuta nyumba wanapatikana, hatuwezi kukwepa ukweli kwamba wana umuhimu wake, na ukisema wawe registered walipe kodi, aisee watu wenyewe hata anapoenda kukuonyesha nyumba unamwona kabisa ni mtu anayeishi maisha magumu anatafuta ya kula tu.
 
Msishangilie hawa watu ni wagumu kuwadhibiti mana mwenye shida ya chumba,kiwanja,nyumba au shamba anakuwa hamjui mwenye mali. So lazima apitie kwa dalali na hapo ndo mzdalali wanapowavimbia.
 
Nchi nyingi zanaofisi kabisa kwenye mtaa au kata. Na kazi zote za kukarabati mahouse girl n.k zinapatikana sehemu Kama hizo.
Sema nchi zilizoendelea mkuu, chumba kimoja cha giza maeneo ya malamba mawili huko , nani atakitangaza kwenye classified magazine au website? Hapo ndo madalali wanaingilia kati
 
Sikujua Kumbe bado nchi iko gizani halafu bado wanasema Jiwe alikusanya kodi hivi kodi kiasi gani imepotea kwa hawa watu wanaofanya udalali??

Kuna haja ya kuwa na website za rental houses mtu akitaka anaingia na kulipa akiridhika hij ni rahisi na salama na kila kitu kiko traced!

Happ kodi itaonekana na kukatwa kodi na hizo commision za udalali zitakatwa kodi pia
Kabisa tena ziwe na Rating kabisa .maana kuna nyumba zingine hovyo kabisa.Una weka rating ya maana kuwasanuwa wengine
 
Msishangilie hawa watu ni wagumu kuwadhibiti mana mwenye shida ya chumba,kiwanja,nyumba au shamba anakuwa hamjui mwenye mali. So lazima apitie kwa dalali na hapo ndo mzdalali wanapowavimbia.
Kama mtu anataka chumba,nyumba inabd sasa

Ye mwenyewe apige mguu na kuulizia nyumba 1

Baada ya nyingine kama inapangishwa

Ova
 
Back
Top Bottom