Waziri Lukuvi apiga marufuku madalali kulipwa posho ya mwezi mmoja na wapangaji. Asema ni ujambazi

Waziri Lukuvi apiga marufuku madalali kulipwa posho ya mwezi mmoja na wapangaji. Asema ni ujambazi

Dawa ni kufungua Website wenye Nyumba wawe wanatangaza na sisi tunaingia na kukodi
Hapo mtatapeliwa mpaka mkumbuke kuwa heri kulipa pesa ya mwezi kwa dalali kuliko hayo.

Maana Nyumba/chumba hujaiona na uambiwe utaetanguliza ndio atapata. Mtakimbizana kutanguliza bila kumuona mwenye nyumba au mkaonyeshwa mwenye nyumba feke.
 
Nchi nyingi zanaofisi kabisa kwenye mtaa au kata. Na kazi zote za kukarabati mahouse girl n.k zinapatikana sehemu Kama hizo.
Tatizo bongo kila kitu ni deal, yaani wale ma agent wa kutafuta wadada wa kazi wengi ni wapigaji hakuna uaminifu
 
Wakiamua hawashindwi.
Mkuu tatizo la serikali yetu ni kuanzisha vita isivyoviweza.

Namna ya madalai wa vyumba wanavyofanya kazi zao inahuisana sana na umasikini wa mtanzania , imagine Karne hii bado kuna watu wanatafuta kupanga vyumba vya giza !!!

Sio kwamba umeme hawaupendi , la bali hawana uwezo wa kumudu gharama zake . Funny enough kuna wawekezaji wa nyumba za aina hizo , anajenga akijua demands za wateja hao zipo, na connection inatoka kwa dalali,
Katika mazingira kama hayo dalali hakwepeki
 
Waziri alete Sheria inayoipa Real Esate Regulatory Authority kumanage hizi issues na sio kupiga blah blah…….hawataki kupitisha sheria sababu wao nao ni wapangishaji wakubwa wanaogopa itakula kwao……
 
Waziri wa Ardhi, William Lukuvi amepiga marufuku Madalali kuwadai Wapangaji Fedha ya Mwezi Mmoja, akiita kitendo hicho kuwa ni ujambazi

Amesema, "Kuna baadhi ya Madalali wanapangisha nyumba halafu wanachukua kwa Wapangaji Kodi ya mwezi. Hawa wanaochukua pesa za wapangaji waache mchezo huo kwasababu ni wizi wa mchana kabisa. Wewe umeajiriwa na mwenye nyumba, yeye lazima akulipe wewe"

View attachment 2011900

Non Sense ,matamko kibao halafu hamyasimamii ,mlishawahi kusema wenye nyumba hakuna kutaka kodi ya miezi 6 au mwaka bali walipwe mwezi kwa mwezi lakini hiyo issue haitekelezwi.
 
Waziri wa Ardhi, William Lukuvi amepiga marufuku Madalali kuwadai Wapangaji Fedha ya Mwezi Mmoja, akiita kitendo hicho kuwa ni ujambazi

Amesema, "Kuna baadhi ya Madalali wanapangisha nyumba halafu wanachukua kwa Wapangaji Kodi ya mwezi. Hawa wanaochukua pesa za wapangaji waache mchezo huo kwasababu ni wizi wa mchana kabisa. Wewe umeajiriwa na mwenye nyumba, yeye lazima akulipe wewe"

View attachment 2011900
Sasa solution yake ni ipi maana hata ukisena ni wizi je unatusaidia nini??!!
 
Wanaopanga hawana shida kulipa maana si kazi rahisi kupata nyumba.

Sasa kama ni hivo dalali si anaweza kuongea na mwenye nyumba bei iwe juu ,kitu kile kile
Atadaiwa kodi kubwa zaidi[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Matamko ya kisiasa tu hayo,madalali wanaturahisishia kazi na ni lazima wapewe posho kama ilivyo ada.
 
Nilisha fanya utafiti katika hili na nikaishauri wizara ya fedha nini cha kufanya kuweza kupata kodi kupitia madalali lakini Mwigulu aliliweka kapuni na kukomaa na TOZO.

Nilishauri kuwa:-

1.Madalali watumike waliosajitiwa wizara ya fedha na wawe na ofisi zinzotambulika chini ya makampuni yaliyosajiliwa.
2.Wahakikimali wa serikali ambao ndiyo wanaotoa na leseni za udalali kwa kila mkoa ndiyo wawe wafuatiliaji juu ya uhalali wa madalali wa kupangisha nyumba na wahakikishe wana leseni na wajisajiri kwa makamishina wasaidizi wa ardhi wa mikoa.
3.Wamiliki wa nyumba zinazopangishwa waorodheshe nyumba zao kwa makamishina wasaidizi wa ardhi wa mikoa ili kulipia service levy.
4.Madalali waliosajiliwa ndiyo watakuwa na jukumu la kusimamia upangishaji,ulipaji kodi,mikataba,kulipia kodi TRA(with hold tax),n.k. na kurew mikataba kwa kufuata utaratibu uleule wa awali.
5.Madalali watalipwa kamisheni yao kwa asilimia kama ilivyo kisheria na siyo kwa mwezi na pia kuyoka kwa mwenyenyumba na siyo mpangaji

Madalali wote watakaoshindwa kukidhi vigezo washitakiwe kisheri,japo hili limekuwa likizungumzwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na kubaki porojo tu.

Nawasilisha.
 
Nadhani ni muda umefika watu wetu wa IT watengeneze mifumo rahisi ya kupata malala pa kupanga kwa mtandao kama Airbn nk..
 
Back
Top Bottom