Waziri Mabula hatihati kutumbuliwa Uwaziri

Waziri Mabula hatihati kutumbuliwa Uwaziri

Kama ndiye aliyesema viwanja vya 20 kwa 20 visipewe hati, basi na aende zake
 
Huenda uteuzi wa Waziri wa Ardhi, Angelina Mabula ukatenguliwa wakati wowote kuanzia sasa kwa kile kinachodaiwa kuwepo kwa mgongano wa kimaslahi kutokana na uamuzi wake wa kusitisha utoaji wa vibali vya ujenzi wa vituo vya mafuta.

Uamuzi huo umetangazwa leo Alhamisi Novemba 10, 2022 na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Angeline Mabula.

“Lengo ni kutoa nafasi kwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na wizara zinazohusika na utoaji wa vibali kufanya tathmini ya kina kuhusu ujenzi wa vituo vya mafuta nchini,” amesema.

Aidha, Dk Angeline ameagiza kusitishwa kutolewa kwa vibali vipya vya ujenzi vinavyokiuka mipango kabambe ya majiji, manispaa, miji na kusitisha ugawaji wa viwanja kiholela unaosababisha taswira za miji kuharibika.

Habari zaidi zinasema maamuzi hayo yatawagusa watoto wa wakubwa ambao wanadaiwa kwa sehemu kubwa wanajishughulisha na biashara ya mafuta
watz tunafeli wapi?kila kitu kikitokea ni kutumbuliwa.kwa hiyo waache mambo yaende holela kwa kuogopa watoto wa wakubwa!baadaye likitokea janga kutokana na ujenzi holela utasikia waziri ajiuzulu.ifikie mahali sasa viongozi wetu wasiwasikilize sana watu sabau hawana uelekeo.watz ni bendera fuata upepo.huku wapo kule wapo ndo maana hata vyombo vyetu vya habari vinaandika habari kwa kufuata upepo.hata lets say leo jaribu pitia magazeti yetu yote yana stori zinazofanana.
 
Kila kituo kimoja kipya cha Mafuta ni ajira kama ishirini zinatengenezwa, sasa Waziri anataka Vijana waende kwenye Ofisi zake wakae getini kumuomba ajira?
 
Ni hatari sana kiusalama vituo vya mafuta kujengwa karibu karibu, ikitokea ajali ya moto kituo kimoja moto ukishika kituo kingine mji mzima unateketea kwa moto, asante sana waziri Mabula kusitisha vibali kwa kufanya tathmini.
Tunyweni bia
 
Riz1 na baba yake wameguswa kende kwenye hilo zuio. Lazima wa react. Sasa hivi mpaka ndani ndani mitaani Lake Oil wanajenga vituo vya mafuta. Na kwa speed inayokwenda ya ujenzi sidhani kama usalama unazingatiwa. Sasa siku vikija vikabutuka mabomu ya Gongo La Mboto yatakuwa cha mtoto.
 
Vituo vya Mafuta sio pampu peke yake kuna Parking Supermarket Car wash massage parlour kwa madereva wa safari ndefu.

Siasa za kihasidi na kusagiana Kunguni hazifai ni primitive.

Waziri amekurupuka hii sio Awamu ya kukurupuka.
 
Nashangaa barabara ya Bagamoyo, vingine vinatazamana, ni wewe uchague kushoto au kulia. Huenda faida yake ni kubwa sana ndio maana vinafunguliwa kwa mashindano.
 
Huenda uteuzi wa Waziri wa Ardhi, Angelina Mabula ukatenguliwa wakati wowote kuanzia sasa kwa kile kinachodaiwa kuwepo kwa mgongano wa kimaslahi kutokana na uamuzi wake wa kusitisha utoaji wa vibali vya ujenzi wa vituo vya mafuta.

Uamuzi huo umetangazwa leo Alhamisi Novemba 10, 2022 na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Angeline Mabula.

“Lengo ni kutoa nafasi kwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na wizara zinazohusika na utoaji wa vibali kufanya tathmini ya kina kuhusu ujenzi wa vituo vya mafuta nchini,” amesema.

Aidha, Dk Angeline ameagiza kusitishwa kutolewa kwa vibali vipya vya ujenzi vinavyokiuka mipango kabambe ya majiji, manispaa, miji na kusitisha ugawaji wa viwanja kiholela unaosababisha taswira za miji kuharibika.

Habari zaidi zinasema maamuzi hayo yatawagusa watoto wa wakubwa ambao wanadaiwa kwa sehemu kubwa wanajishughulisha na biashara ya mafuta
Msaidizi wake ni mmiliki mwenza wa vituo vya mafuta kadhaa ndio tatizo linapoanzia
 
Uku kwetu Mwanza, kutoka nyegezi stendi mpaka sehemu moja inaitwa buhongwa ndani ya kilomita sita kumejengwa vituo vya mafuta 13 na bado vingine vinajengwa mpaka unajiuliza kuna faida kiasi gani kwenye hii biashara, mbona vituo ni vingi kuliko hata garage za magari...na uwiano wa magari yenyewe...si bure kuna namna ya utakatishaji wa fedha apo.
 
Ningekuwa mimi ningewaacha wavijenge mpaka wachoke baadae wangeflate wenyewe
Unajua kwani kujenga vingi mwisho wa siku haigurentee wateja kuongezeka
Free force za demand zingewafirigisa wangeacha wenyewe bila kuambiwa kama wanojenga hotel za mabas ya mkoani
Tabu huku mitaani, ila main roads haina shida, kingine wanajenga tu bila kuzingatia umbali unaotakiwa kati ya vituo na makazi.
 
But it is too much jamani! kujenga vituo vya mafuta kuna maelekezo yanaongoza lakini kwa miaka ya karibuni imekuwa vinajengwa hadi katika makazi ya watu!
Na hii sababu kubwa ni rushwa wanayopewa wanaotakiwa kuidhinisha vituo hivi ie manispaa, Ewura nk! na huu ndio ukweli!
 
Hawa watu wana nguvu ya kufanya watakavyo. Fikiria kuna mtu anajenga katikati hifadhi ya barabara ya njia nane pale Kimara Stopover hakuna anayemuuliza.
Stopover.jpg
 
Back
Top Bottom