Tetesi: Waziri Maghembe kutumbuliwa

Tetesi: Waziri Maghembe kutumbuliwa

Mzee amechoka apumzike mwenyewe before hajatumbuliwa,Uongo huweza kusemwa na yeyote hasa wanasiasa wa Tanzania,lakini kama yaliyosemwa na kiongozi wa mawaziri ni sahihi.Hakuna cha zaidi isipokuwa maamuzi tu.
 
Alinifukuza chuo huyu akafanya nihamie bara lingine kabisa . Naamini zamu yake nae imefika kuishi kama shetani.

[HASHTAG]#BringBackBenAlive[/HASHTAG].
Du, alikufanyia nini mtu wangu mpaka ukahama Bara? Pole sana.
 
kama huyu faru john alipigwa deal basi wapigaji wamepiga deal kwa kutumia akili nyingi sana..
siku ya kwanza PM anauliza kwa nini alitolewa serengeti?
anajibiwa majibu ya kitaaluma mpaka anaishiwa nguvu.
1.faru john aliondolewa setengeti kwa sababu tulitaka ku control in breeding
2.aliondolewa kwa sababu ya ukorofi wake kitu ambacho kilihatarisha uhai wa faru wengne kwamba alikuwa anawafukuza mpaka wanaenda nje ya conservation area kitu ambacho ni rahisi kuuliwa na majangili..
2.huko gurunet alikufa natural dealth sababu ya umri na upweke kwani aliwekwa ndani ya cadge.
jibu hilo linaua doubt kuwa faru aliuawa kwa kukusudia ila pembe zipo
4.naomba mfukue kabri ili apimwe vinasaba
anajibiwa.mzee faru john hakufa kwa ugonjwa wa maambukizi ila uzee hivo hakuzikwa ili ku suport food chain na ecology kwa wanyama walao mizoga.
hivi kwa sababu hizi nani atashikwa uchawi juu ya faru john.
halafu wahifadhi wanajibu kitaaluma na kwa confidence zote
PM.Kapigwa na butwaa je ?taarifa ya ki intelijensia imenipotosha au wapiga dili wanatumia akili nyingi..
Due! Hatari sana hii
 
Kuna kila dalili kwamba Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe amekalia kuti kavu, tena kavu kwelikweli.

Sakata la kuuzwa kwa faru John na kisha yeye kubariki uuzwaji huo ni udhaifu mkubwa sana na kigezo tosha cha kumfanya aondolewe kwenye nafasi yake ya sasa. Kwa mujibu wa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Majaliwa, inasemekana faru huyo aliuzwa kwa thamani ya Tsh milion 200, ambapo wauzaji walitanguliziwa malipo ya Tsh milioni 100. Waziri mkuu hawezi kusema uongo. Ni dhahiri anazo taarifa za uhakika za kiintelejensia kwamba faru ameuzwa kwa bei hiyo ya kutupwa. Ndio maana wahifadhi wanashindwa kuonyesha kaburi lake lilipo kama kweli mnyama huyo wa porini alikufa.

Sintofahamu hii inakolezwa zaidi na Maghembe mwenyewe aliyediriki kumdanganya Waziri Mkuu, kwa kushirikiana na wezi wenzake, kwamba faru yule 'amekufa' huku akijua kwamba anasema uongo. Kwa sababu hizi, pamoja na sababu nyingine ambazo bado hazijawekwa wazi ili kumtumzia heshima profesa huyu, kuna kila dalili kwamba huenda Rais, Dr Joseph Pombe akatengua uteuzi wake kabla hajamaliza faru wetu.

Ikiwa waziri mwenye dhamana ya kulinda rasilimali zetu, ama kwa kujua au kwa makusudi, ameamua kushirikiana na majangili kufilisi rasilimali zetu kuna haja gani ya kuendelea kukalia kiti cha uwaziri? Kwa dhati kabisa bila unafiki wowote, mimi namuunga mkono Rais Pombe katika utumbuaji huu. Ifike wakati kila mtu aheshimu rasilimali za taifa kwa manufaa ya watanzania wa sasa na vizazi vijavyo.

Mungu mbariki Rais wetu, Mungu wabariki watanzania, Mungu bariki rasilimali zetu za Taifa. Amen.

[HASHTAG]#bringbackourrhinoalive[/HASHTAG]
Usitusumbue shenzi weye, nani kamtuma huyo rais wako kuwapatia uwaziri watu ambao walishawàhi kutumburiwa na serikali zilizopita? Na bado wapo wengi tu na wale madalali ya escrow
 
Umetisha..kama vile ulikua ukimchungulia Faru John all the time
Mkuu inauma sana kuona rasilimali za taifa letu zikimalizwa na majangili kama Maghembe.
 
"....Barani Afrika sio muhimu sana kwa kiongozi kuwa makini, waafrika tumejifunza kudharau mambo muhimu na kushangilia kauli za viongozi hata kama hazina maana..."
Koffi Annan 2014
Africa Journal
 
Inasikitisha kuona serikali ya CCM ikiendelea kulamba matapishi yale yale ya siku zote.
 
Ha ha ha ,anaendaga na siku akienda lazima kick. Anatembea mita 200 anasevu million mia.
Nchi ya kusadikika...Mimi natembea kilomita 5 nasevu mia sita shilingi
Mkuu umenifurahisha , yaani nchi hiii imejaa unafiki wa kiwango cha PhD maana tunafanywa kama cc ndezi. Tunapiga makofi na wao - wanajilipa mapesa mengimengi huku tukifa njaa.
 
Naomba nitaje mawaziri na manaibu waziri ambao hawafai haswa japokuwa wote hawafai:
1. Mwigulu nchemba: huyu kwanza ndiye muuaji wa kwanza na hustoria yake inamuhukumu kuwa yeye ni suspect wa mauaji yote yenye utata yanayotokea kwa wanasia.
2. Prof Jumanne Maghembe: Huyu ni mpiga dili na ni miongoni mwa mawaziri mizigo tangu zamani.
3. Prof Sospeter Muhongo : nikili kuwa huyu ni mbunge wangu na kabila moja na Mimi lakini kama mnavyojua suala la escrow linamuhusu sana na hasa pale alipojibadilisha kuwa dalali wa dili la escrow ofisini kwake.
4. Nape Nauye: Huyu hana dhamira ya kuendeleza michezo, utamaduni na habari bali yupo kufuta haki ya kupata habari kwa watanzania.
5. Hamis Kigwangala; Huyu mwenyewe anapenda masifa kila siku, nk.
 
Alinifukuza chuo huyu akafanya nihamie bara lingine kabisa . Naamini zamu yake nae imefika kuishi kama shetani.

[HASHTAG]#BringBackBenAlive[/HASHTAG].
Mkuu shukuru ulikuwa na uwezo wa kwenda bara jingine, huyu mtu hovyo sana, mwenyewe niliponea chup chup.
 
Mpalakugenda, pori letu la Liparamba Faru wapo lakini siunajua pale Lumeme tumewekewa kibao kinasomeka Akiba la hifadhi la wanyama pori sisi tunatunza tuu ila haaaaa kila naiti Landrover zinaondoka na maliasili yetu Liparamba yangu basi tuu.
 
Back
Top Bottom