Tetesi: Waziri Maghembe kutumbuliwa

Tetesi: Waziri Maghembe kutumbuliwa

Ndio maana mnyama yeyote akipata matatizo lazima Magembe kama waziri apewe taarifa na yeye ndio wa mwisho kuizinisha na kutoa tamko hiyo ndio kazi yake.
Huna Elimu ya juu

Go back to school Dude.
Mnyama yeyote akipata matatizo lazima waziri apewe taarifa?
Sina hakika na suala hili.

swissme
 
Ndio maana mnyama yeyote akipata matatizo lazima Magembe kama waziri apewe taarifa na yeye ndio wa mwisho kuizinisha na kutoa tamko hiyo ndio kazi yake.
Huna Elimu ya juu

Go back to school Dude.

swissme
Du haya bana bibi nyama!!!
 
Wewe unaamini kuwa wanayama wote huko mbugani huwa wanazikwa... tuonyeshe hata kaburi moja.. mnyama akifa anaachwa mzoga wake usaidie kuwa chakula ya wengine na kuendeleza ecology, unadhani fisi na tai wange ishi vipi kama mizoga inazikwa. Hakuna kaburu la John Faru.
Siku ya sherehe ya uhuru nani aliyesema FARU amezikwa?
Wakat PM anakabidhiwa pembe za John ndo aliambiwa amezikwa sasa kinachozikwa kinatupwa au kufukiwa?
 
Kuna kila dalili kwamba Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe amekalia kuti kavu, tena kavu kwelikweli.

Sakata la kuuzwa kwa faru John na kisha yeye kubariki uuzwaji huo ni udhaifu mkubwa sana na kigezo tosha cha kumfanya aondolewe kwenye nafasi yake ya sasa. Kwa mujibu wa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Majaliwa, inasemekana faru huyo aliuzwa kwa thamani ya Tsh milion 200, ambapo wauzaji walitanguliziwa malipo ya Tsh milioni 100. Waziri mkuu hawezi kusema uongo. Ni dhahiri anazo taarifa za uhakika za kiintelejensia kwamba faru ameuzwa kwa bei hiyo ya kutupwa. Ndio maana wahifadhi wanashindwa kuonyesha kaburi lake lilipo kama kweli mnyama huyo wa porini alikufa.

Sintofahamu hii inakolezwa zaidi na Maghembe mwenyewe aliyediriki kumdanganya Waziri Mkuu, kwa kushirikiana na wezi wenzake, kwamba faru yule 'amekufa' huku akijua kwamba anasema uongo. Kwa sababu hizi, pamoja na sababu nyingine ambazo bado hazijawekwa wazi ili kumtumzia heshima profesa huyu, kuna kila dalili kwamba huenda Rais, Dr Joseph Pombe akatengua uteuzi wake kabla hajamaliza faru wetu.

Ikiwa waziri mwenye dhamana ya kulinda rasilimali zetu, ama kwa kujua au kwa makusudi, ameamua kushirikiana na majangili kufilisi rasilimali zetu kuna haja gani ya kuendelea kukalia kiti cha uwaziri? Kwa dhati kabisa bila unafiki wowote, mimi namuunga mkono Rais Pombe katika utumbuaji huu. Ifike wakati kila mtu aheshimu rasilimali za taifa kwa manufaa ya watanzania wa sasa na vizazi vijavyo.

Mungu mbariki Rais wetu, Mungu wabariki watanzania, Mungu bariki rasilimali zetu za Taifa. Amen.

Ben Saanane ameshapatikana? Faru John naona ana maana sana nchini Zaidi ya Raia sio
 
Mbona hata yeye Majaliwa alidanganya kuhusu fedha za maafa? Naye atumbuliwe maana ni muongo! Mbona hata BWANA YULE alidanganya kuhusu mambo ya dawa?Wanaolipwa milioni 40? Tena BWANA YULE amedanganya sana tangia aingie mjengoni!!
 
Hadithi nyingine zinachosha na kuendekeza majungu tu, kama ameuzwa Mil 200 na bado mil 100, yatosha kabisa mtu aliye na taarifa hizi kujua aliuziwa nani na huyu Faru yupo wapi. Inasikitisha sana kuona tukifanya kazi na kupoteza muda kwa kuendekeza majungu. Sielewi kabisa tunadiscuss nini kwa muda mrefu wakati nchi ina majanga mengi sana haswa usalama wa raia. Tusichoshane akili, aliyesema ameuzwa na kueleza kiasi cha pesa aende akawaoneshe alipouzwa na waziri Mkuu aje atuoneshe Faru akiwa hai kama anaamini ni Ukweli. Full Stop Tusipoangalia tutajenga mizizi ya kufanya kazi kwa majungu na uongo. Tuache kufuatana fuata
 
Kuna kila dalili kwamba Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe amekalia kuti kavu, tena kavu kwelikweli.

Sakata la kuuzwa kwa faru John na kisha yeye kubariki uuzwaji huo ni udhaifu mkubwa sana na kigezo tosha cha kumfanya aondolewe kwenye nafasi yake ya sasa. Kwa mujibu wa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Majaliwa, inasemekana faru huyo aliuzwa kwa thamani ya Tsh milion 200, ambapo wauzaji walitanguliziwa malipo ya Tsh milioni 100. Waziri mkuu hawezi kusema uongo. Ni dhahiri anazo taarifa za uhakika za kiintelejensia kwamba faru ameuzwa kwa bei hiyo ya kutupwa. Ndio maana wahifadhi wanashindwa kuonyesha kaburi lake lilipo kama kweli mnyama huyo wa porini alikufa.

Sintofahamu hii inakolezwa zaidi na Maghembe mwenyewe aliyediriki kumdanganya Waziri Mkuu, kwa kushirikiana na wezi wenzake, kwamba faru yule 'amekufa' huku akijua kwamba anasema uongo. Kwa sababu hizi, pamoja na sababu nyingine ambazo bado hazijawekwa wazi ili kumtumzia heshima profesa huyu, kuna kila dalili kwamba huenda Rais, Dr Joseph Pombe akatengua uteuzi wake kabla hajamaliza faru wetu.

Ikiwa waziri mwenye dhamana ya kulinda rasilimali zetu, ama kwa kujua au kwa makusudi, ameamua kushirikiana na majangili kufilisi rasilimali zetu kuna haja gani ya kuendelea kukalia kiti cha uwaziri? Kwa dhati kabisa bila unafiki wowote, mimi namuunga mkono Rais Pombe katika utumbuaji huu. Ifike wakati kila mtu aheshimu rasilimali za taifa kwa manufaa ya watanzania wa sasa na vizazi vijavyo.

Mungu mbariki Rais wetu, Mungu wabariki watanzania, Mungu bariki rasilimali zetu za Taifa. Amen.

[HASHTAG]#bringbackourrhinoalive[/HASHTAG]
Kwaninii kilaaa wazirii anataka kumaliza faruuwetuu wanamajini ama??
 
Kwani huyo faru John aliuzwa mwaka gani
Inasemekana aliuzwa tangu mwaka jana kwa thamani ya Tsh milioni 200 lakini Waziri Maghembe na wasaidizi wake wakadanganya kwamba amekufa kumbe si kweli. Wamekuja kuumbuka baada ya kushindwa kumuonyesha Waziri Mkuu lilipo kaburi la mnyamapori huyo.
 
Inasemekana aliuzwa tangu mwaka jana kwa thamani ya Tsh milioni 200 lakini Waiziri Maghembe na wasaidizi wake wakadanganya kwamba amekufa kumbe si kweli. Wamekuja kuumbuka baada ya kushindwa kumuonyesha Waziri Mkuu lilipo kaburi la mnyamapori huyo.
Mwaka Jana Mh Maghembe alikuwa waziri wa utalii Kwani?
 
Hivi huyo faru mwenyewe alihamishiwa Kenya? Kama alipelekwa ndani ya hifadhi zetu tatizo liko wapi? Walikuwa wanamfunga kamba huyo joni? Hebu watu waache ujinga wajikite kuletea watu maendeleo bwana! By the way, hivi Ben ameshapatikana?
 
Sidhani kama Prof Maghembe anahusika moja kwa moja kwenye hili sakata, hivi huo mchakato wa kumhamisha Faru John ulifanyika wakati Prof ni waziri wa maliasili na utalii? au ndo dhana pana ya uwajibikaji?
Mkuu, Maghembe anahusika kwa 101%...wakati faru anapigwa bei yeye alikuwepo na amekuwa mstari wa mbele kumdanganya PM kwamba faru amekufa kumbe wamempiga bei kwa wazungu. Inauma sana.

[HASHTAG]#bringbackourrhinoalive[/HASHTAG]
 
We unadhani kipindi hicho kulikua na TCU na izo standardized cut off point ? Watu walikua vichwa Sana much respect to John john mnyika kamanda wa nguvu.
[HASHTAG]#BringBackBenAlive[/HASHTAG]
Si ulukuwa huna akili ?
 
usiseme waziri mkuu hawezi kudaganya labda useme Kasim Majaliwa hawezi kudanganya uwaziri mkuu ni cheo tulikuwa na waziri mkuu aliyedanganya wakati wa issue ya richmond hapo inabidi turekebishe
 
Back
Top Bottom