Tetesi: Waziri Maghembe kutumbuliwa

Tetesi: Waziri Maghembe kutumbuliwa

Wazir mkuu alisema kuwa serikali imetoa trilion 1 kununua madawa. Magufuli akasema serikali imetoa billion 200 kunuNua dawa. Nani apo ni muongo?
Ww ndiyo muongo, jamaa hao ndiyo serikali utapiga kelele bure subiri cdm yenu mwaka 2200
 
Kumtumbua Maghembe ni uonevu mkubwa. Kama jambo hili la faru john limefanyika ndani ya awamu hii basi waziri mkuu Majaliwa Kasimu Majaliwa ajiuzuru.

Yeye ndiye mtendaji mkuu wa serikali, iweje waziri aliye chini yake auze nyara za umma halafu waziri mkuu ajipe kazi ya kukata mkono wake (waziri)
 
Mimi sijui wanapinga maelezo ya uzi huo wanahitaji nini hasa, wanataka waziri mkuu aseme uongo au wale waliohusika na kupotea kwa faru wachukuliwe hatua
 
Nauliza hiviiiiiiiiii eti ile mahakama ya mafisadi ipo au haipo ? Kama ipo kwanini hawa wasipelekwe huko ?

Bado mafundi wanapaka rangi, kisha viwekwe na vigaye chini, hapo mambo uatakuwa tayari.
 
Kuna kila dalili kwamba Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe amekalia kuti kavu, tena kavu kwelikweli.

Sakata la kuuzwa kwa faru John na kisha yeye kubariki uuzwaji huo ni udhaifu mkubwa sana na kigezo tosha cha kumfanya aondolewe kwenye nafasi yake ya sasa. Kwa mujibu wa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Majaliwa, inasemekana faru huyo aliuzwa kwa thamani ya Tsh milion 200, ambapo wauzaji walitanguliziwa malipo ya Tsh milioni 100. Waziri mkuu hawezi kusema uongo. Ni dhahiri anazo taarifa za uhakika za kiintelejensia kwamba faru ameuzwa kwa bei hiyo ya kutupwa. Ndio maana wahifadhi wanashindwa kuonyesha kaburi lake lilipo kama kweli mnyama huyo wa porini alikufa.

Sintofahamu hii inakolezwa zaidi na Maghembe mwenyewe aliyediriki kumdanganya Waziri Mkuu, kwa kushirikiana na wezi wenzake, kwamba faru yule 'amekufa' huku akijua kwamba anasema uongo. Kwa sababu hizi, pamoja na sababu nyingine ambazo bado hazijawekwa wazi ili kumtumzia heshima profesa huyu, kuna kila dalili kwamba huenda Rais, Dr Joseph Pombe akatengua uteuzi wake kabla hajamaliza faru wetu.

Ikiwa waziri mwenye dhamana ya kulinda rasilimali zetu, ama kwa kujua au kwa makusudi, ameamua kushirikiana na majangili kufilisi rasilimali zetu kuna haja gani ya kuendelea kukalia kiti cha uwaziri? Kwa dhati kabisa bila unafiki wowote, mimi namuunga mkono Rais Pombe katika utumbuaji huu. Ifike wakati kila mtu aheshimu rasilimali za taifa kwa manufaa ya watanzania wa sasa na vizazi vijavyo.

Mungu mbariki Rais wetu, Mungu wabariki watanzania, Mungu bariki rasilimali zetu za Taifa. Amen.

[HASHTAG]#bringbackourrhinoalive[/HASHTAG]
watumbuane tu.maana me nishachoka ikiwezekana rais avunje baraza lote
 
Wewe unaamini kuwa wanayama wote huko mbugani huwa wanazikwa... tuonyeshe hata kaburi moja.. mnyama akifa anaachwa mzoga wake usaidie kuwa chakula ya wengine na kuendeleza ecology, unadhani fisi na tai wange ishi vipi kama mizoga inazikwa. Hakuna kaburu la John Faru.

Angalieni asije akataka na jina la padri alieendesha misa ya kumzika marehemu John......
 
ni malaika nadhani! hehe
Unajua, wakati wa JK, Waziri angeliweza kusema ukweli na akadumu kazini. Leo siyo hivyo. Utatumbuliwa. Lazima useme uongo umpendezeshe. Nasikia????? not confirmed please- nilisoma humu JF kuwa kuna wilaya fulani wanalaza wagonjwa wa kipindupindu katika wodi za kawaida kuogopa kuambiwa kuwa wameshindwa kusimamia usafi DC and therefore risk being fired (kutumbuliwa)- sijui kama ni kweli????
 
Sipo kwenye hoja ya faru kwa kuwa siujui undani wake.lakini napinga maelezo yanayosema waziri mkuu hawezi kusema uongo hali na yeye ni binadamu na mpaka alipofikia kwenye suala la faru ameshawahi kudanganya akiwa jimboni mwake kuwa ajira mpya za walimu hususani wa sayansi zitatoka julai kitu ambacho hakikutokea mpaka leo
 
Hivi Ben na faru yohana nani was maana
Kila kitu kinaangaliwa katika context yake Beni ni wa muhimu serekali lazima iwajibike kumtafuta kupitia vyombo vyake vya kipelelezi polisi ....kwa upande mwingine vita ya kupambana na ujangili ni muhimu lazima iendelee ...kwa hiyo udadisi wa faru john ni muhimu sana
 
Sina uhakika na jambo hili lakini jana nilisikiliza maelezo ya ni namna gani mnyama ambae hakufa kwa magonjwa yasiyoambukiza, dispoasal yake haiwezi kuwa kwa kuzikwa!

Haijalishi kama Faru John amekufa kweli or not; lakini ikiwa PM hakuambiwa Faru John alikufa kwa maradhi ya kuambukiza basi ile kuagiza kaburi lifukuliwe peke yake inatosha kuonesha huwa anaropoka bila kutafiti kidogo! Endapo angetumia dakika 5 tu kutafiti basi angejuwa aina ya "kifo" cha John haikutakiwa kuzikwa na hivyo badala ya kuagiza kaburi kufukuliwa angeagiza kuoneshwa ni wapi mzoga wa John ulitelekezwa! Na kwa mtindo huu si ajabu hatimae akaagiza "nendeni Gurunet mkaangalie masalio ya Faru John hapo alipotelekezwa" Hatimae ataletewa jibu Fisi wamekula hadi mifupa kwahiyo hamna hamna masalio!"
information ya kwamba faru alizikwa ameipata kwenye report waliompelekea. wao ndo waliosema wamemzika. sasa waseme walipomzika watu wafanye vipimo tujue mbichi na mbivu.
 
Maendeleo ya kweli yanapatikana kwa kufanya kazi kwa bidii , nidhamu ya mtumizi na heshima kwa maslimali zako na zataifa zaidi ya hapo ni kupiga mbizi kwenye mchanga tu na bahati mbaya wezi wa nchi hii ni wasomi sasa unajiuliza watu wenye kutakiwa kutupeleka kwenye nchi ya ahadi ndio wafalme wa Egypt
 
Back
Top Bottom