DogoWaNjombe
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 3,284
- 7,708
Akiwa katika ziara hiyo Waziri Kombo atashiriki katika matukio mbalimbali ya kimkakati ikiwemo; Mkutano wa 5 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi za Afrika na Singapore (5th Singapore-Africa Ministerial Exchange Visit - SAMEV); Kongamano la 8 la Biashara kati ya Afrika na Singapore (8th Africa Singapore Business Forum -ASBF), kushiriki kongamano la Wafanyabiashara wa Tanzania na Singapore na kufanya mazungumzo ya uwili na viongozi mbalimbali wa ngazi za juu Serikali ya Singapore na sekta binafsi.
Waziri Kombo katika ziara hiyo ambayo imebeba dhima ya utekelezaji wa diplomasia ya uchumi ameambatana na ujumbe wa Wafanyabiashara, ikikusudia kuongeza wigo wa fursa za kiuchumi huku ikitilia mkazo zaidi katika nyanja za biashara na uwekezaji, uchumi wa bluu, teknolojia, nishati jadidifu, utalii na kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia.
Takwimu kutoka Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) zinaeleza kuwa kuanzia mwaka 1997 hadi Julai 2025, jumla ya miradi 36 yenye thamani ya Dola za Marekani milioni 535.13 imesajiliwa hapa nchini kutoka Singapore, ikikadiriwa kutengeneza ajira 3,228. Sehemu kubwa ya uwekezaji huo umejikita katika sekta ya viwanda, ikiwa na jumla ya miradi 21 kati ya 36.