Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,621
- 8,411
Serikali ya Tanzania yasema haina ushahidi wa kutosha kuzitia hatiani shule za Feza zinazodaiwa kumilikiwa na raia wa Uturuki anayetuhumiwa kujihusisha na jaribio la kupindua Serikali ya Uturuki.
Serikali ya Uturuki inadai wamiliki wa shule hizo na baadhi ya wafanyabiashara wanafadhili ugaidi kwa kushirikiana na Imamu Fethullah Gulen anayeishi nchini Marekani ambaye ndio inadaiwa yuko nyuma ya jaribio la Mapinduzi.
= > Serikali ya Uturuki yatakiwa kuwasilisha taarifa zenye ushahidi wa kutosha juu ya hili.
= > Aidha, Ubalozi wa Uturuki Tanzania umedai kuwa baadhi ya walimu wa shule za FEZA ambao ni raia wa Uturuki wamekuwa wakitumia mbinu za kigaidi kufundisha wanafunzi.
Feza wamekanusha kuhusika

Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Augustino Mahiga amesema serikali ya Uturuki kupitia balozi wake hapa nchini imedai wamiliki wa shule za Feza Tanzania walifadhili jaribio la mapinduzi Uturuki
Serikali hiyo inadai mapinduzi hayo hayakuanzia jeshini tu bali yameanzia kwenye vyuo na shule mbalimbali Uturuki na nje ya uturuki
Ubalozi wa Uturuki umesema wamiliki wa shule hizo hapa nchini wanahusika na kufadhili mapinduzi hayo huko Uturuki na ada inayokusanywa kutoka kwenye shule hizo ilitumika kufadhili mapinduzi hayo na ni magaidi
Balozi Mahiga amesema wametaka ushahidi zaidi kutoka serikali ya Uturuki kuhusu madai hayo
Walimu wa shule ya Feza wamedai wao hawahusiki kabisa na mapinduzi hayo na shule zao hazijihusishi na mambo ya siasa na zinamilikiwa na watanzania