Waziri Makamba akutana kwa mazungumzo na Waziri wa Viwanda na Teknolojia ya Juu wa Serikali ya UAE

Hizi habari zipo tokea Juzi hapa? Nikadhani kuna jipya kumbe ni yale yale ya kutafuta furusa za upigaji?
Mkuu Mimi nimeziweka hapa ili kukazia bandiko lang la Jana kuhusu huo uteuzi mpya wa mawaziri wa Mh Samia
Unaweza kulisoma tena
[emoji116]

Mabadiliko Mawaziri tuliingizwa Kingi
 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) amekutana na kuzungumza na Waziri wa Viwanda na Tekinolojia ya Juu wa Serikali ya Umoja wa Falme za Kiarabu, Mhe. Sultan Ahmed Al Jaber Jijini Nairobi, Kenya.

Waziri Makamba amekutana na Mhe. Al Jaber pembezoni mwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi unaofanyika Nairobi, Kenya.

Pamoja na mambo mengine, Mhe. Waziri Makamba ameihakikishia UAE kuwa Tanzania itashiriki Mkutano wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP 28) mwezi Disemba 2023, ambapo miongoni mwa masuala itakayoyatilia mkazo ni ufadhili wa miradi ya nishati safi ya kupikia kwa akina mama vijijini.

Aidha, Mheshimiwa Waziri Makamba amesisitiza kuwa Tanzania itaungana na nchi za Afrika na nchi nyingine zinazoendelea duniani, kuhimiza Nchi Wanachama, hususan zilizoendelea kutekeleza ahadi za kupunguza hewa ukaa, kuchangia fedha kwa ajili ya Uhimilivu na kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi na upatikanaji wa teknolojia kwa ajili ya jitihada hizo.

Kwa upande wake, Mhe. Sultan Ahmed Al Jaber, aliishukuru Tanzania kwa kuahidi kushiriki Mkutano wa COP 28 na kwamba Umoja wa Falme za Kiarabu umejipanga kuhakikisha Mkutano wa COP 28 unaleta matokeo chanya katika jitihada za kukabiliana na athari za mabadiliko ya Tabianchi Duniani.

Aidha, Mhe. Al Jaber aliahidi kuunga mkono masuala ya kipaumbele ya Tanzania katika Mkutano huo kwa kuzingatia uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na UAE.

Mhe. Al Jaber ni Rais ajaye wa Mkutano wa Cop 28 unaotarajiwa kufanyika Dubai, mwezi Disemba 2023.

#newsupdatemedia2023View attachment 2743874
Pia soma

Mabadiliko Mawaziri tuliingizwa Kingi
Shida yako nini!?..uarabu wa imarati au dini zao!?..angekua mzungu ungehara jamvini!?
 
Kwanini makamba anaingilia wizara nyingine? Inamaana wizara ya mazingira Haina waziri?
 
Bandari haziwezi kuporwa maana zitaendelea kuwepo hapo zilipo hata baada ya miaka elfu ijayo !
Ila kwenye madini ndipo unapoweza kuporwa usipokuwa makini maana baada ya miaka kadhaa utabakiwa na mashimo tupu yaliyojaa nyoka !!
Bandari isiyo nufaisha taifa husika kwa muda husika ili kuineemesga Jamii husika!
Ina tofauti gani na iliyoporwa?
 
Yale mashirika waliouzia wazawa wakayatelekeza sasa yamefika pake.

Huko Ar ilikuwepo general tairi
huko mbeya ikawepo hi soap, mbeya tex, sido vyombo

Vyote vyote wakapewa watu wakafanya ma godown

Sasa je? Huyu mjomba wa Mheshimiwa kuna kitu atafanya au atanunua viwanda na raia?

And why Arabs only?
Arabs wanafanya biashara kwa sasa kwa sababu Wazungu wameamua kwanza waziteketeze pesa zao kwa vita huko Ukraine 🇺🇦 mpaka ajulikane ni nani mbabe wa Dunia !
Akishapatikana wanarudi kuzitawala Nchi zote za Dunia ya tatu wakiwemo na hao Arabs 🙏🙏💰
 
Arabs wanafanya biashara kwa sasa kwa sababu Wazungu wameamua kwanza waziteketeze pesa zao kwa vita huko Ukraine [emoji1255] mpaka ajulikane ni nani mbabe wa Dunia !
Akishapatikana wanarudi kuzitawala Nchi zote za Dunia ya tatu wakiwemo na hao Arabs [emoji120][emoji120][emoji383]
Wataliacha taifa likiwa Hoi bin Taaban!
 
Bandari haziwezi kuporwa maana zitaendelea kuwepo hapo zilipo hata baada ya miaka elfu ijayo !
Ila kwenye madini ndipo unapoweza kuporwa usipokuwa makini maana baada ya miaka kadhaa utabakiwa na mashimo tupu yaliyojaa nyoka !!
Kwanini tuliwaonda wakoloni wakati hata wasingeondoka nchi yetu ingeendelea kuwepo kwa miaka 10000000
 
Arabs wanafanya biashara kwa sasa kwa sababu Wazungu wameamua kwanza waziteketeze pesa zao kwa vita huko Ukraine [emoji1255] mpaka ajulikane ni nani mbabe wa Dunia !
Akishapatikana wanarudi kuzitawala Nchi zote za Dunia ya tatu wakiwemo na hao Arabs [emoji120][emoji120][emoji383]
Suala hapa ni kwamba muda si mrefu Mafuta yatakuwa sio issue Duniani kutokana na aidha akiba kuisha huko Ardhini au Pia kutokana na ujio wa matumizi ya Umeme zaidi kwenye vyombo vya moto badala ya Mafuta.
Waarabu wanaona mbali na kuwahi hizi fursa kupitia viongozi walafi na wasiojitambua wa kiafrika.
 
Bandari haziwezi kuporwa maana zitaendelea kuwepo hapo zilipo hata baada ya miaka elfu ijayo !
Ila kwenye madini ndipo unapoweza kuporwa usipokuwa makini maana baada ya miaka kadhaa utabakiwa na mashimo tupu yaliyojaa nyoka !!
Kama kuna mtu mwingine amezichukuwa kwa utapeli na kuzitumia kwa manufaa yake ni nini hicho
 
"Aidha, Mhe. Al Jaber aliahidi kuunga mkono masuala ya kipaumbele ya Tanzania katika Mkutano huo kwa kuzingatia uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na UAE."

Hayo Mahusiano Mazuri ni yapi hapa nchini,Ilhali kuja kwao ndiyo kumechochea kuni za Ufisadi nchini?
 
Back
Top Bottom