Waziri Makamba akutana kwa mazungumzo na Waziri wa Viwanda na Teknolojia ya Juu wa Serikali ya UAE

Waziri Makamba akutana kwa mazungumzo na Waziri wa Viwanda na Teknolojia ya Juu wa Serikali ya UAE

[emoji16][emoji120]
Haya hapa
[emoji116]

Mabadiliko Mawaziri tuliingizwa Kingi
 
Takataka tu

Mabadiliko Mawaziri tuliingizwa Kingi
 
Wewe umemezwa kwenye kanzu.
Makamba hapaswi kuingilia majukumu ya wizara ambayo sio yake!
That's the Point hayo ya uarabu na kanzu zako wewe endelea nazo.
Naona unajua majukumu yake kuliko yeye,kwamba kaamua tu kuonana na Waziri wa nchi nyingine bila kutumwa,kazi za Waziri wa mambo ya nje ni zipi!?
 
Mkisha maliza kuuza hii nchi mtugawie hata mil' moja moja na sisi wananchi sio mnajilimbikizia wenyewe tu
 
Kama kuna mtu mwingine amezichukuwa kwa utapeli na kuzitumia kwa manufaa yake ni nini hicho
Uporaji ! Lakini kama amezichukua na baadaye zikaleta faida kubwa kuliko miaka yote iliyopita ??!!
 
hio picha imenitafakarisha sana...hao waarabu wanatuona ngombe kama ngombe nyingine machungani....yaani hatuna utamaduni kiasi kwamba tunaweka vazi rasmi kuwa suti na tai kama mwingereza au mzungu....hivi tungeamua kuenzi lubega zetu si zingekuwa official kama kanzu...(inje ya mada nawaza kwa sauti)
 
Uporaji ! Lakini kama amezichukua na baadaye zikaleta faida kubwa kuliko miaka yote iliyopita ??!!
Kwanza haziwezi kuleta faida kubwa kwa sababu mwenyewe hakushirikishwa! Kwa hiyo huyo ni mwizi au tapeli!
 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) amekutana na kuzungumza na Waziri wa Viwanda na Tekinolojia ya Juu wa Serikali ya Umoja wa Falme za Kiarabu, Mhe. Sultan Ahmed Al Jaber Jijini Nairobi, Kenya.

Waziri Makamba amekutana na Mhe. Al Jaber pembezoni mwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi unaofanyika Nairobi, Kenya.

Pamoja na mambo mengine, Mhe. Waziri Makamba ameihakikishia UAE kuwa Tanzania itashiriki Mkutano wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP 28) mwezi Disemba 2023, ambapo miongoni mwa masuala itakayoyatilia mkazo ni ufadhili wa miradi ya nishati safi ya kupikia kwa akina mama vijijini.

Aidha, Mheshimiwa Waziri Makamba amesisitiza kuwa Tanzania itaungana na nchi za Afrika na nchi nyingine zinazoendelea duniani, kuhimiza Nchi Wanachama, hususan zilizoendelea kutekeleza ahadi za kupunguza hewa ukaa, kuchangia fedha kwa ajili ya Uhimilivu na kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi na upatikanaji wa teknolojia kwa ajili ya jitihada hizo.

Kwa upande wake, Mhe. Sultan Ahmed Al Jaber, aliishukuru Tanzania kwa kuahidi kushiriki Mkutano wa COP 28 na kwamba Umoja wa Falme za Kiarabu umejipanga kuhakikisha Mkutano wa COP 28 unaleta matokeo chanya katika jitihada za kukabiliana na athari za mabadiliko ya Tabianchi Duniani.

Aidha, Mhe. Al Jaber aliahidi kuunga mkono masuala ya kipaumbele ya Tanzania katika Mkutano huo kwa kuzingatia uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na UAE.

Mhe. Al Jaber ni Rais ajaye wa Mkutano wa Cop 28 unaotarajiwa kufanyika Dubai, mwezi Disemba 2023.

#newsupdatemedia2023View attachment 2743874
Pia soma

Mabadiliko Mawaziri tuliingizwa Kingi
Hakuna kitu hapo.
 
Warabu wa dubai wamemlisha nini huyu mama mbona kama anakuwa dhaifu sana kwa hawa jamaa! Yaani hachomoi kwa chochote aisee..
 
Pesa mingi kwa faida ya nani? Kwa kuwa bandari ni mali ya DPW!
Hakuna kitu kama hicho !! Bandari ni mali za Nchi wale Dipiwedi ni wawekezaji tu kama wengine waliokuwepo kabla yao !
TICTS and the likes 😅🙏

Maubaguzi hayafai bandugu 🙏🙏🙏
 
Back
Top Bottom