Mabadiliko yaliyofanywa na Rais Samia kwenye baraza la Mawaziri.Ni kiini macho. Uhalisia ni kwamba Rais Samia alikusudia na anaendelea kujisimika na kujiimarisha kwa mbinu zozote zile ili kujiwekea mazingira ya ushindi wa urais 2025. Hili kumuweka mkwewe kwenye Tamisemi ni mpango rasmi...

Wewe umemezwa kwenye kanzu.
Makamba hapaswi kuingilia majukumu ya wizara ambayo sio yake!
That's the Point hayo ya uarabu na kanzu zako wewe endelea nazo.
hio picha imenitafakarisha sana...hao waarabu wanatuona ngombe kama ngombe nyingine machungani....yaani hatuna utamaduni kiasi kwamba tunaweka vazi rasmi kuwa suti na tai kama mwingereza au mzungu....hivi tungeamua kuenzi lubega zetu si zingekuwa official kama kanzu...(inje ya mada nawaza kwa sauti)
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) amekutana na kuzungumza na Waziri wa Viwanda na Tekinolojia ya Juu wa Serikali ya Umoja wa Falme za Kiarabu, Mhe. Sultan Ahmed Al Jaber Jijini Nairobi, Kenya.
Waziri Makamba amekutana na Mhe. Al Jaber pembezoni mwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi unaofanyika Nairobi, Kenya.
Pamoja na mambo mengine, Mhe. Waziri Makamba ameihakikishia UAE kuwa Tanzania itashiriki Mkutano wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP 28) mwezi Disemba 2023, ambapo miongoni mwa masuala itakayoyatilia mkazo ni ufadhili wa miradi ya nishati safi ya kupikia kwa akina mama vijijini.
Aidha, Mheshimiwa Waziri Makamba amesisitiza kuwa Tanzania itaungana na nchi za Afrika na nchi nyingine zinazoendelea duniani, kuhimiza Nchi Wanachama, hususan zilizoendelea kutekeleza ahadi za kupunguza hewa ukaa, kuchangia fedha kwa ajili ya Uhimilivu na kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi na upatikanaji wa teknolojia kwa ajili ya jitihada hizo.
Kwa upande wake, Mhe. Sultan Ahmed Al Jaber, aliishukuru Tanzania kwa kuahidi kushiriki Mkutano wa COP 28 na kwamba Umoja wa Falme za Kiarabu umejipanga kuhakikisha Mkutano wa COP 28 unaleta matokeo chanya katika jitihada za kukabiliana na athari za mabadiliko ya Tabianchi Duniani.
Aidha, Mhe. Al Jaber aliahidi kuunga mkono masuala ya kipaumbele ya Tanzania katika Mkutano huo kwa kuzingatia uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na UAE.
Mhe. Al Jaber ni Rais ajaye wa Mkutano wa Cop 28 unaotarajiwa kufanyika Dubai, mwezi Disemba 2023.
Mabadiliko yaliyofanywa na Rais Samia kwenye baraza la Mawaziri.Ni kiini macho. Uhalisia ni kwamba Rais Samia alikusudia na anaendelea kujisimika na kujiimarisha kwa mbinu zozote zile ili kujiwekea mazingira ya ushindi wa urais 2025. Hili kumuweka mkwewe kwenye Tamisemi ni mpango rasmi...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.