Mbona mnahangaika sana kumsafisha mtu ambaye alikwishatumbukia kwenye dimbwi la OIL CHAFU?Waziri wa Nishati ndugu January Makamba amewahakikishia watanzania kuwa hakuna uhaba wa mafuta, akitoa ufafanuzi baada ya mkurugenzi Mkuu wa TPDC ndugu James Mataragio kukaririwa vibaya juu ya kauli ya uhaba wa mafuta
Waziri Makamba amefafanua kuwa
Dizeli iliyopo kwenye matenki nchini hadi leo asubuhi ni lita milioni 90.7. Meli inayoitwa SLOANE SQUARE muda huu inashusha lita milioni 60.9 hivyo kupelekea mafuta ya dizeli kuongezeka na kuwa lita 151,694,926 yanayotosheleza kwa siku 24.
Petroli iliyopo kwenye matenki nchini hadi leo asubuhi ni lita 100,345,631. Meli iitwayo JAMES COOK inashusha lita 22,493,188; meli iitwayo JAG PUNIT iko njiani na lita 30,579,019 hivyo kupeleka mafuta ya petroli kuongezeka na kuwa lita 153,417,838 yanayotosheleza kwa siku 34
mafuta ya taa ndani ya siku tano zilizopita, nchini kulikuwa na lita 3,978,276 zinazotosheleza kwa mahitaji ya siku 46.
Hivyo mafisadi waliotaka kutumia kauli ya ya Mataragio kama kigezo cha kushawishi EWURA ipandishe bei ya mafuta wamegonga mwamba.
Heko Waziri Januari Makamba
Heko Mama Samia
Heko Tanzania
KAZI IENDELEE
Makamba ni janga la kitaifaMbona mnahangaika sana kumsafisha mtu ambaye alikwishatumbukia kwenye dimbwi la OIL CHAFU?
Kwa hiyo Makamba ndio amerudisha lile kundi lake la kampeni mtandaoni lililokuwa likipiga kura hewa kuchuana na team Membe na team Ngeleja?
Hadi awamu iliyopita tulimwamini Rais kwaio hata makamba tunamwamini ndio Mtendaji wa mwisho kwenye wizara hioUnaacha kumuamini msimamizi wa maghala ya mafuta unamuamini mpewa ripoti..kweli uchawa ukizidi unakuwa funza.
Waandishi wanamgombanisha waziri na Mtendaji mkuuAlichokisema James ndio alichokisema Makamba baada ya kutoka Uarabuni. Waandishi wa habari wamemnukuu vibaya James.
Usilolijua ni sawa na usiku wa gizaMakamba ni janga la kitaifa
Tumpe nafasi achape kazi atatuletea makubwaTumpe nafasi huyu makamba afanye kazi tumuamini ili tuone uwezo wake tusiwe na haraka kumponda bila uhalali.
Si ao waliochapisha habari za kupanda kwa mafuta ili nchi itikisikeNani fisadi? Kama sisi wewe mwenyewe?
Mwache jamaa achape kazi🏃♂️🏃♂️🏃♂️
View attachment 2008296
Kazi imeanza mmeshaanza kuhujuma hadi mafuta jamani nchi kama viel amna kiongozi madili kila mahala yameshaamza kutengenezwaWaziri wa Nishati, January Makamba amesema haya...
“Hakuna uhaba wa mafuta nchini. Hakuna sababu ya kuwa na taharuki. Utaratibu wa kuingiza mafuta unahakikisha kwamba mahitaji yapo wakati wote. Serikali inaendelea kuchukua hatua kuongeza uhakika wa upatikanaji na unafuu wa bei”.
“Kauli ya uhakika ni ya Serikali. Mkurugenzi wa TPDC atatoa taarifa kuhusu taarifa yake hii manake aliitoa kwenye semina ya wanahabari lakini ni gazeti moja tu ndio limeandika. Pia atakuja ofisini kutoa maelezo kabla hatujachukua hatua za ziada”.
Pia soma > TPDC: Mafuta yaliyopo yatosha siku 15
Tatizo wala sio vita,Aisee! Ndani ya siku 15,!
Hivi ikitokea vita hizo Meli zikawa blocked watz watapona kweli?