Waziri Makamba: Hakuna uhaba wa mafuta nchini, amtaka Mkurugenzi wa TPDC akajieleze kabla hawajachukua hatua

Waziri Makamba: Hakuna uhaba wa mafuta nchini, amtaka Mkurugenzi wa TPDC akajieleze kabla hawajachukua hatua

Waziri wa Nishati ndugu January Makamba amewahakikishia watanzania kuwa hakuna uhaba wa mafuta, akitoa ufafanuzi baada ya mkurugenzi Mkuu wa TPDC ndugu James Mataragio kukaririwa vibaya juu ya kauli ya uhaba wa mafuta

Waziri Makamba amefafanua kuwa
Dizeli iliyopo kwenye matenki nchini hadi leo asubuhi ni lita milioni 90.7. Meli inayoitwa SLOANE SQUARE muda huu inashusha lita milioni 60.9 hivyo kupelekea mafuta ya dizeli kuongezeka na kuwa lita 151,694,926 yanayotosheleza kwa siku 24.

Petroli iliyopo kwenye matenki nchini hadi leo asubuhi ni lita 100,345,631. Meli iitwayo JAMES COOK inashusha lita 22,493,188; meli iitwayo JAG PUNIT iko njiani na lita 30,579,019 hivyo kupeleka mafuta ya petroli kuongezeka na kuwa lita 153,417,838 yanayotosheleza kwa siku 34

mafuta ya taa ndani ya siku tano zilizopita, nchini kulikuwa na lita 3,978,276 zinazotosheleza kwa mahitaji ya siku 46.

Hivyo mafisadi waliotaka kutumia kauli ya ya Mataragio kama kigezo cha kushawishi EWURA ipandishe bei ya mafuta wamegonga mwamba.

Heko Waziri Januari Makamba
Heko Mama Samia
Heko Tanzania
KAZI IENDELEE
Mbona mnahangaika sana kumsafisha mtu ambaye alikwishatumbukia kwenye dimbwi la OIL CHAFU?

Kwa hiyo Makamba ndio amerudisha lile kundi lake la kampeni mtandaoni lililokuwa likipiga kura hewa kuchuana na team Membe na team Ngeleja?
 
Alichokisema James ndio alichokisema Makamba baada ya kutoka Uarabuni. Waandishi wa habari wamemnukuu vibaya James.
 
Mbona mnahangaika sana kumsafisha mtu ambaye alikwishatumbukia kwenye dimbwi la OIL CHAFU?

Kwa hiyo Makamba ndio amerudisha lile kundi lake la kampeni mtandaoni lililokuwa likipiga kura hewa kuchuana na team Membe na team Ngeleja?
Makamba ni janga la kitaifa
 
Unaacha kumuamini msimamizi wa maghala ya mafuta unamuamini mpewa ripoti..kweli uchawa ukizidi unakuwa funza.
Hadi awamu iliyopita tulimwamini Rais kwaio hata makamba tunamwamini ndio Mtendaji wa mwisho kwenye wizara hio
 
Alichokisema James ndio alichokisema Makamba baada ya kutoka Uarabuni. Waandishi wa habari wamemnukuu vibaya James.
Waandishi wanamgombanisha waziri na Mtendaji mkuu
Halafu walilkosa tenda tanesco anachukua jama advantage ya kunchafua Waziri wakati mambo yanaeleweka
 
Makamba endelea kuchapa kazi baba
Maendeleo kwa vitendo weka mipango kazi iendelee
 
Makamba fanya kazi, wanaokupinga na kukuponda watakuelewa tuu mbele ya safari.
 
Tumpe nafasi huyu makamba afanye kazi tumuamini ili tuone uwezo wake tusiwe na haraka kumponda bila uhalali.
 
Tumpe nafasi huyu makamba afanye kazi tumuamini ili tuone uwezo wake tusiwe na haraka kumponda bila uhalali.
Tumpe nafasi achape kazi atatuletea makubwa
Rais Samia ni mtu makini na anajua uwezo wa Makamba
 
🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
1459200653746708485.png
 
Waziri wa Nishati, January Makamba amesema haya...

“Hakuna uhaba wa mafuta nchini. Hakuna sababu ya kuwa na taharuki. Utaratibu wa kuingiza mafuta unahakikisha kwamba mahitaji yapo wakati wote. Serikali inaendelea kuchukua hatua kuongeza uhakika wa upatikanaji na unafuu wa bei”.

“Kauli ya uhakika ni ya Serikali. Mkurugenzi wa TPDC atatoa taarifa kuhusu taarifa yake hii manake aliitoa kwenye semina ya wanahabari lakini ni gazeti moja tu ndio limeandika. Pia atakuja ofisini kutoa maelezo kabla hatujachukua hatua za ziada”.

Pia soma > TPDC: Mafuta yaliyopo yatosha siku 15
Kazi imeanza mmeshaanza kuhujuma hadi mafuta jamani nchi kama viel amna kiongozi madili kila mahala yameshaamza kutengenezwa
 
Aisee! Ndani ya siku 15,!

Hivi ikitokea vita hizo Meli zikawa blocked watz watapona kweli?
Tatizo wala sio vita,

Kama ukiangalia hizo screenshot, utaona kuna maneno "Vessel is Out of Range"! Sometimes, meli zinazopita Ghuba ya Eden na hata Indian Ocean from the Horn of Africa, huwa wana-switch off Automatic Identification System!!

Hiyo AIS huwa inatambulisha identity na location za meli zinapokuwa baharini! Sasa kwavile Ghuba ya Eden na Indian Ocean ni high risk area kutokana na uwezekano wa kuwepo pirates, ndipo wanazima hizo AIS ili wasiwe tracked.

So, risk sio vita bali piracy!
 
Back
Top Bottom