Waziri Makamba: Hakuna uhaba wa mafuta nchini, amtaka Mkurugenzi wa TPDC akajieleze kabla hawajachukua hatua

Waziri Makamba: Hakuna uhaba wa mafuta nchini, amtaka Mkurugenzi wa TPDC akajieleze kabla hawajachukua hatua

Mimi nadhani alitaka kuweka worse case scenario kwamba ikitokea meli haijafika ila alikosea sababu bulk system ndio wanajukumu hilo kuhakikisha wale walioshinda tender wanaleta kwa wakati na hii imekuwa toka 2012 sasa mkurugenzi wa TPDC hii sio kazi yake kusemea serikali nadhani ameshajuwa kuna chance TPDC wakarudishiwa wao wawe kama waagizaji pekee kitu ambacho hakitatokea wameshanusa ulaji sasa wamefufuka. Kwa kauli hii mkuregenzi wa TPDC kaingilia mamlaka sio yake kabisa maana hata yeye na kampuni yake wameshinda tender kwa kushindana na wengine hawakupewa tu kama zawadi. Waziri yuko sahihi jamaa kachemka ila naamini hakuwa na nia mbaya ila hakuliweka sawa na vile waandishi wetu hawa wanadaka moja baya tu.

Kuna Vitu umeongea sahihi vingine kama Unatak kupotosha...
Tpdc watanunua Mojoa kwa moja toka Visimani,Hivyo hakuna Mtu kati,Na Bei itakuwa chini,Sasa haya Makampuni yakikuwa yakiagiza Bei inakuwa juu tuuu hata Kama Bei kule wanakununulia Iko chini”
Mwisho wa Kunukuu
 
Hakuna mafuta yanauzwa visimani, kuna watu wana produce crude wanauza crude tu na wako wana refine products ni biashara nyingine kabisa sasa huwa nashangaa hizi kauli za kupotosha watu tunanunua visimani moja kwa moja. Ungeniambia kuwa tanzania wana refinery hapo ningekuelewa maana ungenunua crude direct lakini ku refine crude upate products ni gharama pia kuna process ndefu na ya gharama. Hapo unamaanisha kununua refinery direct labda ila kumbuka hakuna biashara ya direct wako mawakala ndio kazi yao kwa hiyo hakuna ukweli wowote tunanunua direct mafuta yanapanda dunia nzima. Wao wana kodi zaidi ya 10 unategemea nini? Huwezi ku control bei ya mafuta ni soko linaamua tatizo liko katika system ya uagizaji mafuta nchini limekaa kijamaa zaidi sio kiushindani. Mzigo mnaleta nyinyi na bulk system yenu bei elekezi inatolewa na serikali kulaumu una mlaumu mfanya biashara wakati bei mmepanga nyinyi na huwa wanasema bei itakuwa hivi sababu bei imepanda duniani.
 
Kuna tofauti gani alichosema yeye mwenyewe waziri alipotoka kuzurura uarabuni na alichosema mkurugenzi wa TPDC.

Wote wametoa scenario ambayo ni risk kwa upatikanaji wa mafuta, na hata thread yenyewe aijapindisha kitu imeongelea scenario.

Sasa tena kama vilaza wa JF awakuelewa mkurugenzi anaongelea nini na kudandia kuna uhaba wa mafuta ilo ni kosa la mkurugenzi kweli, kuna hiyo taharuki kweli mtaani au waziri anatafuta sifa.

Ameshaboronga TANESCO na sasa anataka kwenda kuongeza matatizo TPDC.

Halafu mafuta ayashuki on the same day kwenye pump kama yanavyoshuka kwenye soko la dunia. By know he should know purchase orders are placed well in advance ukitaka kununua mafuta.

So mafuta yanayofika leo unakuta yalinunulia kwa bei ya mwezi mmoja au miwili nyuma kama muagizaji anatumia FI-FO kwenye Investory record zake na yeye awezi shusha sababu bei ya dunia imeshuka leo, atauza kwa bei alizonunulia mwezi mmoja au miwili nyuma.

Ndio maana mafuta kwenye pump huwa yanachelewa kushuka sambamba na bei ya soko la dunia.
 
Hakuna mafuta yanauzwa visimani, kuna watu wana produce crude wanauza crude tu na wako wana refine products ni biashara nyingine kabisa sasa huwa nashangaa hizi kauli za kupotosha watu tunanunua visimani moja kwa moja. Ungeniambia kuwa tanzania wana refinery hapo ningekuelewa maana ungenunua crude direct lakini ku refine crude upate products ni gharama pia kuna process ndefu na ya gharama. Hapo unamaanisha kununua refinery direct labda ila kumbuka hakuna biashara ya direct wako mawakala ndio kazi yao kwa hiyo hakuna ukweli wowote tunanunua direct mafuta yanapanda dunia nzima. Wao wana kodi zaidi ya 10 unategemea nini? Huwezi ku control bei ya mafuta ni soko linaamua tatizo liko katika system ya uagizaji mafuta nchini limekaa kijamaa zaidi sio kiushindani. Mzigo mnaleta nyinyi na bulk system yenu bei elekezi inatolewa na serikali kulaumu una mlaumu mfanya biashara wakati bei mmepanga nyinyi na huwa wanasema bei itakuwa hivi sababu bei imepanda duniani.

TPDC: Mafuta yaliyopo yatosha siku 15
 
January Makamba: Hakuna uhaba wa mafuta nchini. Hakuna sababu ya kuwa na taharuki. Utaratibu wa kuingiza mafuta unahakikisha kwamba mahitaji yapo wakati wote. Serikali inaendelea kuchukua hatua kuongeza uhakika wa upatikanaji na unafuu wa bei.

Akijibu swali la mdau alieuliza mkanganyiko kati ya mkurugenzi wa TPDC na kauli yake kujichanganya, Makamba amesema yake ni Kauli ya uhakika ya Serikali. Mkurugenzi wa TPDC atatoa taarifa kuhusu taarifa yake kwasababu aliitoa kwenye semina ya wanahabari lakini ni gazeti moja tu ndio limeandika.

Pia amemtaka mkurugenzi wa TPDC aende ofisini kutoa maelezo kabla hajachukuliwa hatua za ziada.

Aidha, amesema Dizeli iliyopo kwenye matenki nchini hadi leo asubuhi ni lita milioni 90.7. Meli inayoitwa SLOANE SQUARE muda huu inashusha lita milioni 60.9 hivyo kupelekea mafuta ya dizeli kuongezeka na kuwa lita 151,694,926 yanayotosheleza kwa siku 24.

Petroli iliyopo kwenye matenki nchini hadi leo asubuhi ni lita 100,345,631. Meli iitwayo JAMES COOK inashusha lita 22,493,188; meli iitwayo JAG PUNIT iko njiani na lita 30,579,019 hivyo kupeleka mafuta ya petroli kuongezeka na kuwa lita 153,417,838 yanayotosheleza kwa siku 34

Pia soma > TPDC: Mafuta yaliyopo yatosha siku 15

Nadhan James anachokesema ni sahii ila wakina wizara wanaleta siasa watz hatuwez kusonga mbale kwa kuendelea kuwa na watu wale wale wenye mawaz yale wanaobebwa na ccm na hawajachaguliwa na wananchi wapewa tu vyeo tunahitaji katiba mpya
 
Kumbe hata Hamza alikuwa ni mwana cdm?
Huoni wafuasi wa mboe walivyo furahia na kejeli juu baada ya Askari 3 kuuwawa na Gaidi Hamza?

chunguza utaona kuwa kila tukio baya linalo wakumba askari au viongozi au nchi kwa ujumla utakuta wafuasi wa mboe wanafurahia na kukejeli.
hiyo ndio dalili tosha kuwa kazi mbaya ya kupandikiza vitendo vya kihalifu lilifanywa na Mwenyekiti wao.
 
Haka kajamaa kanatufaa sana!!! Mwenda zake alikuwa na zake zi vijamboz!!! yaani alijawa na chuki yule mzee basi tu yaani! mpaka aibu!..... huko ahera ana lalamika eti amewai kufa mapema mweee!!

Mimi; nikamwambia ukaegeee huku huku ndo kuna kufaa!! kwani hukujua??

(NB; Mazungumzo yangu na jiwe yalikuwa mafupi sana, ila ntakuwa nawaletea habari kutoka kuzimu!! kuna watu wengi huko balaa! wanaenda na kurudi, mpaka sasa wanaenda lkn hawapewa kibali na serikali ya kuzimu kuongelea haya isipokuwa mimi tu na jiwe!).......km hivi...endelea

Jiwe ; aaah! mtani sikujua,

Mimi; ndo ujue sasa, ukutane na kina Beni saanane! sasa mwenzako ni kiranja wa huku kuzimu!! unasemaje? kwani umechota maji leo?!

Jiwe; dogo ana niheshimu sana yule! japo nilimfanyizia lkn??? anaanza kulia ''sijui itakuwa mpaka lini! milele au?

Mimi; ukipewa nafasi ya kurudi Bongo vipi! utaweza? au ubaki huku huku!

Jiwe; Daaa!! ntafurahi sana Mtani! yaani nahakikisha zile familia za watoto nilizopiga na wale nilio ua Baba zao!! nawaomba msamaha wa dhati nawalipa fidia!! wasome mpaka wachoke wao!! haya kwakweli mtani siyo maisha mazuri! halafu ntaachana na siasa za kuwatukana Mabeberu!! saabu sikujua! nilidanganywa na kiburi cha uzima! yaani mtani sikujua kabisa!! lkn sasa muda umekwisha si unaona sikupata hata Muda wa kutubu?

Mimi; Kweli kabisa !! sasa ulikuwa unawaza nini? na kanisani ulienda?

Jiwe; Unajua Mtani shetani alinidanganya sana, kweli nikawa na kiburi cha uzima mpaka kanisani! ukienda washauri wasiwe km mimi! naumia sana huku Mtani! Mwambie yule kijana wangu Atubu kwa dhati asije kuwa km mie! sasa haya ni maisha mazuri haya kweli?

Mimi: Nitajaribu lkn sasa kijana mwenyewe yuko mafichoni, sasa!!! Una muonaje Mama anavopiga mzigo!!

Jiwe mfu! yaani heee! yaani Mtani, aendelee tu! ivoivo, yuko vizuri bado, ziara afanye tu, nyie bado ni watega kopo!! lkn kinacho niumiza mbona hakunisaidia tu hata ushauri?? wkt nilimuamini??

Mimi; Kwa nini unasema Nyie!! na wala siyo sisi kwani hututaki tena??

Akaanza kulia !!! akalia sana,.... mpaka askari wa kuzimu wakajaaa pale chemba la kuzimu!! safari ijayo ntawambia hawa askari wa kuzimu walivyo walivyo! wanakula nini huko kuzimu!! wewe utafikaje huko!! na ili usizuiwe kurudi Duniani, unatakiwa uweje!

Onyo; Kuzimu inataka watu kwa hamu kubwa sana, imeachama mdomo Mwaaa!!! km uliwahi kuokoka, au umeokoka kindaki! ndaki! ktk kanisa la kweli!! usijaribu kutuma maombi ya kuja huku! Manake hutarudi Duniani!

Mambo siku hizi ni Rahisi mno!! sababu shetani anajua ana Muda mchache sana wa kupeta!
 
TPDC: Mafuta yaliyopo yatosha siku 15
Hii sio habari mpya toka 2012 hatujawahi kuwa na akiba ya miezi sababu vendor wanabadilika kila mwezi wa kuleta mafuta na meli zinaingia kwa muda yakitoka inakuja meli nyingine inajazia hakuna habari mpya. Labda unataka kusema wanataka kuweka reserve ya nchi kama ni hivyo waweke lakini wanapesa ya kutumbukiza kuweka akiba? msidanganywe na hawa wana siasa nchi hii haijawahi kuwa na zaidi ya akiba ya mwezi.
 
Nilitaka Usome alivyosema Mtaalam Dr.Mataragio Kuwa Watakuwa wananunua Moja Kwa moja,Pia Akazungumza Bei ya Mafuta Imwshuka Mpaka Sifuri,Lakini Huku hayashuki,
Waache wataalam wachukue nafasi yao Mkuu,Kama wewe uko Camel oil sijui oryx kuwa Mpole tuu Kaka[emoji3516][emoji41][emoji2]
Yaani hii Issue naifananisha ya Bwawa la Stiegliers,Wengi wanapenda Mradi Ukamilike tupate Umeme wa Nafuu...Ila wengine wenye maslahi yao binafsi/Ya Wachache wanataka tutumie gas kuzalisha Umeme wakati gas ni ghali! Kama Hawana Pa Kuipeleka Gas Waiuze nje au Viwandani.watuachie Umeme wetu wa maji[emoji39]
Yaani Kuna Watu hawataki Tannesco Ijiendeshe kwa faida aisee[emoji3516][emoji15][emoji15][emoji41][emoji119]
 
Huoni wafuasi wa mboe walivyo furahia na kejeli juu baada ya Askari 3 kuuwawa na Gaidi Hamza?

chunguza utaona kuwa kila tukio baya linalo wakumba askari au viongozi au nchi kwa ujumla utakuta wafuasi wa mboe wanafurahia na kukejeli.
hiyo ndio dalili tosha kuwa kazi mbaya ya kupandikiza vitendo vya kihalifu lilifanywa na Mwenyekiti wao.
Pumbaf chawa wa sukuma gang
 
Zandrano Yuko sahihi machadema ni magaidi mkiongozwa na gaidi mbowe [emoji23][emoji1787]
Hamza naona tayari mshamsahau mwenzenu.
Nasikia wewe ndiye uliyeshika nafasi yake.
 
Kampuni ya simu ya Halotel ni ya January Makamba na JK . Kampuni hii hailipi kodi na imewekeza minara yao kwenye maeneo ya taasisi za serikalu mfano shule za serikali, bure na hawalipi kodi ya pango popote waliopoweka minara. Wizi mkubwa huu
Yaani wasilipe kodi kwa sababu gani
Mnaongea mambo ya barabarani
 
TANZANIA HAKUNA UHABA WA MAFUTA MHE WAZIRI WA NISHATI JANUARY MAKAMBA

Habari Zone Tz

Baada ya kuzushwa taarifa ya kuwepo Kwa uhaba wa mafuta nchini, Waziri wa Nishati Mhe January Makamba ametolea ufafanuzi suala hilo kupitia mtandao wake wa Twitter na kusema

"Hakuna uhaba wa mafuta nchini. Hakuna sababu ya kuwa na taharuki. Utaratibu wa kuingiza mafuta unahakikisha kwamba mahitaji yapo wakati wote. Serikali inaendelea kuchukua hatua kuongeza uhakika wa upatikanaji na unafuu wa bei."

Hakuishia hapo akatoa takwimu za kiasi Cha mafuta kilichopo nchini hadi siku ya Leo

[emoji419] Dizeli iliyopo kwenye matenki nchini hadi leo asubuhi ni lita milioni 90.7. Meli inayoitwa SLOANE SQUARE muda huu inashusha lita milioni 60.9 hivyo kupelekea mafuta ya dizeli kuongezeka na kuwa lita 151,694,926 yanayotosheleza kwa siku 24.

[emoji419] Petroli iliyopo kwenye matenki nchini hadi leo asubuhi ni lita 100,345,631. Meli iitwayo JAMES COOK inashusha lita 22,493,188; meli iitwayo JAG PUNIT iko njiani na lita 30,579,019 hivyo kupeleka mafuta ya petroli kuongezeka na kuwa lita 153,417,838 yanayotosheleza kwa siku 34

[emoji419] mafuta ya taa ndani ya siku tano zilizopita, nchini kulikuwa na lita 3,978,276 zinazotosheleza kwa mahitaji ya siku 46.

More Updates
Instagram: @habarizonetz
Twitter: @HabariZoneTz
Facebook: Fact Site tz
 
Back
Top Bottom