Waziri Makamba jiuzulu, siku 10 za mgao wa umeme kupisha marekebisho zilishaisha ila umeme bado unakatika

Waziri Makamba jiuzulu, siku 10 za mgao wa umeme kupisha marekebisho zilishaisha ila umeme bado unakatika

Wacha nijibu kwa niaba yake;

Mimi naishi dar nipo wilaya ya ilala msongola namba ya simu ni 0783721337 jana kati ya majira ya saa tatu na saa nne asubuhi umeme ulikatika na kurudi saa moja kasoro usiku pia juzi mchana kati ya majira ya saa sita ulikatika na kurudi mchana kama kwenye saa nane hatukuwa na taarifa yoyote,pia maeneo yote jirani kama kivule,kitonga,mvuti na chanika kote tulikosa umeme naomba majibu ya hili tatizo lilikuwa ni nini na kwann mlituaminisha kuwa zile siku kumi mlituaminisha kuwa kukatika kwa umeme kutakuwa ni historia?!!!! TANESCO
Ndugu Mteja

Tunashukuru kwa taarifa, Tumezipokea kwa ufatiliaji na hatua zaidi.

TANESCO Huduma kwa Wateja

Makao Makuu

0748550000
 
Ndugu Mteja

Tunashukuru kwa taarifa, Tumezipokea kwa ufatiliaji na hatua zaidi.

TANESCO Huduma kwa Wateja

Makao Makuu

0748550000

Afadhali hua mko active kidogo hata tunapowatukana mnakua chini kidogo, saa nyingine tumepata hasara unaweka samaki wabichi kwenye friji umeme unakatika bila taarifa ndio hasira hizo
 
Je ni eneo gani?Wilaya na namba ya simu tafadhali
hivi wakubwa mkikaa chini si mnaona mnapigwa kweupee...maana kama majenereta tushanunua mvua za kumwaga matengenezo mshamaliza mwambieni kipara aachie umeme tu aisee
 
Wacheni utapeli wenu, huu umeme umewashinda muda mrefu sana, mnabahatisha tu kama mnavyobahatisha kuongoza nchi.
 
Nimeona kupitia Al jazeera kwamba kutakuwa na hali ya upungufu wa nishati katika maeneo mbalimbali duniani kufuatia vita ya Russia na Ukraine na vikwazo vilivyowekwa.

Tanzania iko duniani ndio nauliza hii katika katika ya umeme wiki hii ni kwa sababu ya vita?

Maendeleo hayana vyama!
Teteteteete we chizi kweli
 
Wacheni utapeli wenu, huu umeme umewashinda muda mrefu sana, mnabahatisha tu kama mnavyobahatisha kuongoza nchi.
Mafuta tuliambiwa wameagiza mzigo wa Dec 2021 tutaanza kuona nafuu March 2022 matokeo yake wamegeuka eti vita ya Rusia na huku haina hata wiki
 
Kiukwel nchi ipo kwenye autopilot tusipoteze muda kuhoji kiukwel wa Mungu makamba hafai hata mjumbe wa nyumba kumi kumi
 
inawezekana makamba akawa waziri mzuri ila ana u much-know mwingi. Haiwezekani waziri anawapa kiburi/jeuri tanesco halafu utegemee umeme uwe wa uhakika
 
Mi najiuliza, kwanini haya yameanza baada ya kuondoka Kalemani, Why?!!
 
Je ni eneo gani?Wilaya na namba ya simu tafadhali
Maeneo mengine mmefunga mita mpya, Lakin kila tukijaza umeme unaambiwa mita namba haitambuliki..Umeme hakuna week ya pili sasa hivi. shirika lenu ni uchafu mtupu hakuna kazi hapo!
 
Mhe. Waziri alituaminisha kuwa utafanyika ukarabati kwa muda wa wiki mbili na umeme utarudi kama uilivyokuwa tangu zamani. Tulifurahi sana kwa kauli ya Mhe. Waziri lakini cha kushangaza mambo yamekuwa tofauti kabisa. Nitoe mfano hapa Mwanza eneo la Mwananchi. Jana umeme ulikatwa mida ya saa moja kamili za usiku na umeme ukarudi kama saa saba za usiku. Ifahamike kuwa kuanzia saa moja usiku ndiyo muda wa kutayarisha mlo wa usiku, kusali, watoto wa shule kufanya mazoezi waliopewa shuleni, n.k. sasa inakuwaje umeme unakatwa muda ambao vitu vya muhimu vinatakiwe vifanyike?. Wakati wa Hayati Mhe. Magufuli umeme ulikuwa haukatiki mbona awamu hii tunaona mambo yakiwa tofauti. Nashauri Mamlaka ya uteuzi uangalie kwa maakini nafasi ya Waziri wa Nishati na Meneja Mkuu wa Tanesco. Kwa maeneo wanapoishi wananchi wa kawaida ni vema umeme ukatwe mchana na siyo usiku.
Kwanini ukatwe mchana,umeme usikatwe kabisa...tulisahau hizi shida za umeme kukatika hovyo.
 
Nyie Kongowe, Kigamboni mbona hakuna umeme..!?
Wataalamu wetu wa matengenezo watafika Leo kwa utatuzi zaidi

Tahadhari
Usikanyage wala kushika waya uliokatika au kulala chini.

Wasiliana nasi kupitia kupitia kituo cha miito ya simu:-0748550000
 
Wee jamaa haupo serious keshasema mwanza,mwananchi hapo si karibia na ofisi zenu. Namba za simu unataka umtumie muamala ama
Je ni eneo gani?Wilaya na namba ya simu tafadhali
 
Back
Top Bottom