Cha kufanya amrudishe eng mramba kuwa managing director jamaa yupo vizuri alitolewa kwa fitina tu za muhongo na magu
Utakuwa ni mnufaika wa Mramba bila shaka. Baada ya Idrisa, hakuna MD wa Tanesco aliyekidhi vigezo.
Mramba ni mwanafunzi wa Mhando, yeye akiwa ndo junior kwenye top layer, Mhando alipenda kumkaimisha nafasi kwakuwa jamaa ni bingwa wa kutoa maandiko ambayo yalikuwa yakikubalika sana wizarani, hivyo Mhando kunuona mwana kuwa ndio wing man wake.
Mhando alijenga safu yake ambayo ni Tangaline, na kila kitu cha shirika kikahamishiwa Tanga. Mramba, unadhani alifanya tofauti?
Akae MD yeyote pale, kama hana hulka za kijiwe, hawezi kufanya vizuri, kulikuwa na safu ya kanda ya ziwa pale, ndio ilikuwa creamy ya shirika, wao ndo wanaamua mwenendo wa shirika. Kamuulize aliyewahi kuwa GM wa mwisho kabla ya 2010, kabla cheo hicho hakijavunjwa, pia kina DMDs watakuambia mchezo ulivyo.
Wanasema chama cha kijani, mrija wake pia uko hapo, muulize Ngeleja alikuwa anafanya nini? Iulize tume ya Warioba, walikuwa wananyonya wese la magari yao kutoka wapi? Waulize walimwengu, zile VX V8 za kijani mawilayani kwaajili ya kampeni kipindi cha Vasco, nani alinunua? Ndivyo wananchi wanavyonong'ona.