Huyu Makamba hana chochote wala lolote zaidi kutembelea nyota ya baba yake na JK. Uwezi kuja na mawazo finyu kwamba dawa ya kufanya tuwe na umeme ni kufukuza wafanyakazi. Hii inaonesha uwezo wake mfupi wa kufikiri na namna ya kutafuta ufumbuzi wa tatizo hana.
Hivyo nijiulize, ni kweli umeme unakatika kwa uzembe wa watumishi au bado Tanzania hatujafikia mahitaji yanayohitajika ya umeme kwa wananchi?
Je umeme huu tulionao ambao si toshelevu kuondoa kero za ukatikaji umeme kila mara ni nini kifanyike ili watanzania wasipate usumbufu huo?
Je, Kuna tatizo gani Tanesco linalofanya kuwe na ukatikaji wa umeme mara kwa mara? Na tatizo linasababishwa na nani?
Nadhani waziri anahitaji kuchukua muda na kutafakari suluhisho la umeme na namna ya kusambaza umeme, na kupata umeme wa nafuu kuliko kuja na hadithi za kufukuzana.
Ndo maana nashangaa hii Tanzania, tunaongozwa na watu wale wale ambao hawajawahi kupata ufumbuzi wa matatizo ya watanzania. Ndiyo maana hatusongi mbele. Si mara ya kwanza huyu Makamba kuwa katika hii wizara. Amekuwa hadi mwenyekiti wa Kamati. Alichowahi fanya ni nini?
Leo Rais anamteuwa tena? Hivi huko Bungeni CCM imeishiwa kabisa? Kitu gani kinamfanya Makamba kuwa special ati kila baraza yumo toka enzi za mzee Kikwete?
Ati watu wanamuona ni Presidential material kweli watanzania tumeishiwa. Tanzania hii ina vijana wengi wenye uwezo mkubwa zaidi ya Makamba.
Hivi Mhe. Rais watu wanaokushauri si warudi enzi za Nyerere walikuwa wanafuatilia watu toka wako shule. Wakiona kichwa wanakichukua. Walifuatilia hata mtaani wakiona kichwa wanakichukua, walifuatilia hata ofisi za serikali wilayani, halmashauri na mikoani ili kuandaa vijana na uongozi wa baadae.
Tuache hii ya kubebana. Naipenda CCM ila nadhani CCM imeshafikia mwisho wa kufikiri, tunahitaji chama ambacho kitaiondoa Tanzania hapa tulipo. Tunahitaji viongozi wenye maono na mikakati mipya. Natamani Mapinduzi!