Waziri Makamba kaanza vibaya, nahofia atafeli kama wenzie

Hahahahaaa. Mkuu inaonekana alikukera sana hiyo 2015. Eti kiparangoto!

Sent from my VF-795 using JamiiForums mobile app
 
Haters wa kisukuma mna Tabu, ulitaka Kalemani abakie?! au angeteuliwa mwenye jina la John
 
Ameanza cheap sana. Huwa namuona jamaa kama muelewa sana. Naona ni mtu anayeweza kufikiri strategically na kufanya mambo yanayoacha alama. Ila hizi business as usual alizoanza nazo sio kabisa.
POLE
 
Tanesco sasaivi wanabadili nguzo,wanaweka nguzo za zege,

Muache kulaumu kila kitu nyie misukule ya dikteta, muacheni January apige kazi
Kwa hiyo hizo nguzo kazileta January?
 
Mkuu nimeusoma mchango wako. Yapo mawazo na ushauri mzuri kwaaendeleo ya Nchi.

Para ya mwisho ambayo umemnukuu Baba wa Taifa JKN ndio hasa ilikuwa inawapata wafanyakazi/Viongozi walio bora na waadilifu. Walikuwa wanapatikana tangia shuleni, vyuoni na makazini kwa wale wa kupandishwa vyeo na madaraka, na ndio maana Chuo cha Mzumbe kilijengwa kwa ajili ya mafunzo ya Utawala na Utumishi, vile vile kuwapiga msasa Watumishi wa Umaa waliokuwa makazini.

Unapoteuliwa kuwa kiongozi sehemu ya kazi, una ajiriwa kwenda kufanya kazi kwa ufanisi na wafanyakazi utakao wakuta ili kuleta tija, na sio kufukuza wafanyakazi. Kwa Kiongozi yeyote yule anayejua/anayefahamu nini maana ya uongozi; kufukuza na kuajiri (hire and fire) katika taasisi/kampuni ya muda mrefu ni sehemu ndogo sana katika kazi zake za kila siku, ni kama asilimia1-5 tu, sio haya tunayo yaona leo kuwa mtumishi akiteuluwa kushika madaraka anakuja na kaulimbiu ya kufukuza wafanyakazi kazi. HAIPENDEZI
 
Mkuu ingependeza sana kama hivi vyeo vya kuteulia (isipokuwa mawaziri) vingekuwa vinatangazwa kwenye maredio na magazeti nk. ili watu waombe na kufanyiwa usaili. Hatua hii ingesaidi sana kuondoa upendeleo wa kikabila, udini, ukanda na ajira za kingono.
 
Makamba atachoka akifuata kila ushauri unaotolewa humu...kila mtu anaonekana anataka kumfundisha kazi.
Maoamba anaijua muchezo yote ya taneco maana kuna mingine alishiriki pia hivyo sion cha kumfundisha kwa sasa
 
Watu wanataka kuweka watu wao ambao watakuwa wanatii maelekezo bila kuhoji.

Hata hivyo tumpe muda.
 
Haitakuwa fair kum-judge J. Makamba mwanzoni .

Mbona alipokuwa Wizara ya mazingira aliweza kukomesha matumizi ya mifuko ya plastic?

J . Makamba anaweza kuleta tija Wizara ya nishati.

Tumpe muda.
 
Labda waje wafanya kazi kutoka nje, lakini hawa wazee wa madili na kukwamishana kwa makusudi, tutaendelea kuwa wa hivi hivi
 
Haters wa kisukuma mna Tabu, ulitaka Kalemani abakie?! au angeteuliwa mwenye jina la John
Katika maisha yangu siishi kwa kujipendekeza, au kwa ushabiki. Naishi katika kweli, wala siishi kwa maneno ya kuazima na uzushi. Nimeongelea teuzi zinavyofanyika. Nadhani ungekuja na hoja kunionesha huyo unaemtetea amefanya jambo gani la manufaa katika nchi wakati akiwa waziri na hata mwenyekiti wa kamati ya nishati. Pia sijamtaja Kalemani, ila nimeongea uteuzi uzingatie watu tofauti wenye uwezo.
Unakuja hapa mara utaje kabila na majina, sasa hiyo ndo hoja?
Kuna semi ya kiswahili; Mwana mwelevu ni faida kwa taifa na jamii, ila mwana mpumbavu ni mzigo kwa mamaye.
 
Tanesco shida yao ni pesa hizo zingine ni siasa tu .Utafukizaje wafanyakaza wakati shirika linajiendesha kwa hasara?Je kawapa bajeti ya kutosha kukalabati miundombinu ya shirika ?Sasa kama hajafanya hivo tunamwomba aache siasa kwenye kazi za kitaluma.
Vunjeni mikataba ya kihuni Tanesco ipate mapato ili itoe huduma za viwango .
 
Tanesco kuna rushwa sana hivyo upelekea target ya ku double customers base ikwame,watu wengi wanataka umeme lakini maofisa wa TANESCO wanasabotage ili wateja watoe rushwa na wasipotoa maofisa wa tanesco hawafanya saveyi wala hawatoi control number.

January Makamba simamia ilo hakika uta double customers basi kama sio kutripo....watu wengi sana wanahitaji umeme ila ndio hivyo maofisa wa TANESCO wanataka Rushwa.
 
Nakubaliana na wewe huyu kipara ngoto sio anatembelea nyota ya baba yake ila baba yake anatembeza nyota yake kwa mtoto wake. Wote ni watu laghai tu wamejaliwa mdomo tu.
 
Januari Makamba njoo huku usikilize malalamiko ya watu. Hata na mimi yalinikumba haya.
 
Nyie hata angeteuliwa Nani, bado mngekosoa tu, hamueleweki watz, kwanza mna chuki kubwa na Samia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…