Waziri Makamba: Sasa Serikali itanunua shehena ya mafuta moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji

Wanasiasa adhabu yao wanastahili kufungwa maisha bila kujali uzito kosa as far as ana utambulisho KAZI = mwanasiasa . Mi wa Tandahimba tani za ujazo nitajuaje ninkiasi gani Kwa pipa .
 
Awamu ya tano iliacha strong negotiation team ya Taifa .Taifa linahitaji kuiboreaha Kwa kwasomesha na kuwatrain wengine .huu ujanja ujanja wa kiongozi kujilipua na kwenda kunegotiate hotelini hatuna historia nao tangu awamu ya tatu .hata makamba akija na mistari watanzania tuwe makini nao end results yake huwa si njema Sana .
 
Napataga wasiwasi viongozi wetu wakishikwa mikono??!! Nikama unapelekwapelekwa hivi ama unavutwavutwa hivi au unabembelezwa hivi...
Swali ni je, serikali inataka kufanya biashara ya mafuta??
Swali dogo la anyongeza. Je, serikali imewahi kufanya bashara gani kwa mafanikio kwa miaka kumi ya karibuni??
Tusiwe mazuzu,tuishauri serikali!
 
Ni mkakati mzuri waziri ameonyesha ubunifu Katika suala la mafuta
 
HUYU JAMAA NDIO HAMNA KITU KABISA KIPINDI CHA NYUMA AKIWA WAZIRI HAKUWAHI KUTAMBUA KUWA FLOWMETER HAIFANYI KAZI LEO AJE ASEME ATASHUSHA BEI KWA KUNUNUA DIRECT TOKA KWA WAZALISHAJI.FAILURE YA KWANZA YA SERIKALI YA AWAMU YA SITA INAANZIA KWA HUYU MUONGO MUONGO.MAMA SAMIA HII NCHI UKISIKILIZA MANENO YA WATENDAJI NA HIZI STORY ZA TAARIFA/RIPOTI /UCHAMBUZI WATAKUDANGANYA SANA HAWA WAPIGAJI WANAJUA KUREMBESHA MAANDISHI.
 
Siasa tu hizi....kama ingewezekana JPM asingeacha kutekeleza hili kwa sababu alikuwaga na bifu na madalali. Sasa Makamba marafiki zake na mabosi wake wa zamani ndo wenye filling stations ataanzia wapi kuwageuka?
Unachanganya mambo mkuu.
Kuna madalali na kuna wenye vituo vya mafuta.
Mimi nina vituo vya mafuta lakini hili la kuondoa madalali nalifurahia kwani linaniumiza sana.
Madalali wanaweka bei kubwa mno kwa walaji wao wa mwisho (sisi wenye vituo vya mafuta).
 
Siasa tu hizi....kama ingewezekana JPM asingeacha kutekeleza hili kwa sababu alikuwaga na bifu na madalali. Sasa Makamba marafiki zake na mabosi wake wa zamani ndo wenye filling stations ataanzia wapi kuwageuka?
Mimi nikivyomwelewa ni serikali itanunua mafuta ya dizeli direct kwa ajili ya matumizi yake hajasema kwa ajili ya kila mtu.Ina maana dizeli kwa private sekta Wenye makampuni private ndio wataendelea kununua na kutuuzia

Private wataendelea kununua petrol kuuzia private sector na serikali, serikali ilichoshinda hapo ni kununua dizeli sio petrol!!

Kwa hapo ni kuwa kampuni za private zitaendelea Kama kawa kitu pekee ambacho kwao ni kuwa hawatachora supply dizeli kwa serikali kwa kipindi Cha December watachukua TPDC
 
Habari njema hizi, January kwa hili la kuwatoa middle men katika business ya kuagiza mafuta nchini, yaani Bulk procurement litakuwa la maana sana sanaaa..

Nasisitiza hii bado ni Habari njema, tunasubiri utakelezaji wake. Maneno mazuri au plan nzuri sio vitendo, ingawa plan nzuri ndio mwanzo wa vitendo vizuri, yaani lazima kwanza u plan vizuri, kisha utekeleze vizuri uliyoplan.. Hapo tutasema hongera hongera.

Good job so far.. Let's wait and see.
 
If it is not broken…. Don’t try to fix it
 
Mimi naona ikitekelezwa itakuwa jambo nzuri sana tu. Wasiwasi wetu ni kwamba kuondoka hao madalali might be challenging. Hilo tu.
 
Tuwekane sawa kwanza, kwani mafuta tunayotumia huwa yananunuliwa na serikali au makampuni ya mafuta?
Sasa itakuwaje kumlazimisha importer auziwe na supplier aliyechaguliwa na serikali tu?
Na mpango endelevu ni upi ....tunavyohangaika na bomba la Hoima ni kwa nini tusijenge kiwanda kushirikiana na Uganda ili tusafishe haya mafuta na kuacha kuagiza?
 
Je hii ni taarifa ya Wizara ya nishati ama ni ya January Makamba? Ukisoma maelezo yanaonyesha umimi mwingi. Mara nilienda, nilikutana, nilifanya mazungumzo..... Huu ni ubinafsi wa hali ya juu. Amegusia kidogo sana ushiriki wa watu wengine katika mazungumzo. Just one man show, badilika.
 
Kwa mujibu wa takwimu za ewura kwenye kuondoa tozo, inaelekea tozo na kodi zinachukua karibia nusu ya bei tunayolipa, kwa hiyo hata tukisema bei ya kununua ni sifuri bado yakifika hapa huenda yakauzwa karbia au zaidi yabei za sasa
 
Hiyo ni 2030 mazee
 
Hatua ya kwanza ni kupunguza tozo na kodi kwenye mafuta haraka kwa wastani wa tsh 500
 
Baada ya cocaine/heroin yanafuatia mafuta kwenye biashara zenye rushwa ya kutisha kwa viongozi wa kisiasa nk. Exxon wapo wanatunishiana msuli na serikali ya Marekani! wazalishaji wa mafuta hao hao ambao Makamba kasema tutanunua kwao moja kwa moja ndio hao hao ambao hutengeneza "supply" na "demand" kwa makusudi kabisa....hapa kwetu zipo tetesi kuwa Kalemani alitemeshwa uwaziri na wafanyabiashara wa mafuta.
Makamba hebu waza nje ya MAZOEA: gesi yetu Mtwara ndiyo turufu yetu....inaweza kutupeleka mbele zaidi!
 
Haka kajamaa ni kichwa, naamini kataweza. Na katataka kufanikisha ili tukaone kana uwezo wa kuwa rais
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…