Samcezar
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 13,095
- 22,731
Ukiona kimya jua kesi imeshaishaHivi wale waliokuwa wwnaiba mafuta na jengo tukaonyeshwa
Wale walikuwa ni untouchables? Maana kwa kweli sikuwasikia tena
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ukiona kimya jua kesi imeshaishaHivi wale waliokuwa wwnaiba mafuta na jengo tukaonyeshwa
Wale walikuwa ni untouchables? Maana kwa kweli sikuwasikia tena
Tumpe muda, hicho alichokisema kama kitafanyika kutakuwa na ahueni. Sema pamoja na yote hayo wafute yale makodi kibao ya mafuta ili na sisi bei iwe ndogo kama wenzetu wa Zambia.Porojo tu hamna la maana hapo!
Sema 'ninapata shida sana..' achana kabisa na hii ya kusema 'tunapata shida..'..Tunapata shida sana kumuamini waziri wa madini kwani historia haimbebi kama mtendaji mzuri asiye na makandokando.
Na suala la yeye kuwa karibu na marehemu Ruge linafanya image yake ni mtu wa kujibrand tuu.
Mkuu hili pekee linaweza lisiwe na impact kubwa kama hawataondoa ule utitiri wa kodi kwenye kila lita moja ya mafuta inayoingia nchini. Wewe hushangai Zambia mafuta yao yanapitia bandarini kwetu na sote tunanunua pamoja huko duniani lakini pale Tunduma ukivuka na kuingia Zambia tofauti ya bei ya mafuta kwa lita ni zaidi ya 700/= juu kwa huku kwetu wakati Zambia ni chini.Mheshimiwa waziri kwa hili la kuondoa mtu kati kwenye uagizaji wa mafuta ukifanikiwa utakuwa umewasaidia sana watanzania. Mungu akusaidie maana najua mpambano wake si wa kitoto.
Nadhani mambo ya tankers za mafuta kwa nchi kubwa kama Tanzania yamepitwa na wakati na ni uharibifu wa barabara na kuongeza conjestion barabarani. Hivi kweli tunashindwaje kujenga bomba la mafuta from Dar Port, Mtwara Port na Tanga Port kwenda mikoani?? Mfano bomba to Morogoro, Dodoma mpaka Mwanza? Pale Chalinze kuna kuwa na branches kwenda Iringa mpaka Mbeya na lingine Tanga mpaka Manyara? Tungelianza hili kama lile la TAZAMA 30 yrs back je mpaka sasa si tungeshamaliza??Nji rahisi ya kurahisisha hili zoezi ni Serikali kuweka miguu moja kwa moja kwenye biashara hii either kuifufua tipper na kuiongezea uwezo au kuanzisha haraka ujenzi wa refinery plant kubwa kabisa na kuagiza mafuta ghafi meengi na kuyarefine then kuuza kwa majirani na mengine kuyatumia wenyewe....
Kupitia TPDC kumiliki OIL tankers zetu kwa ajili ya kubeba crude oil kwa ajili ya refinery plant yetu...hii itatusaidia kubalance bei za mafuta kwa kiasi kikubwa na kuleta unafuu mkubwa..
Kwa ule utitiri wa zile kodi kwenye mafuta utashangaa imeshuka shilingi tano mkuu note my word... Yaani hapa zile kodi kwa maoni yangu zinachukua 60% na hawa waagizaji na watu wao wa kati ni 40%Kwa hiyo ndiyo yatashuka au??
Kwa nini unapost uzi ule ule? Hivi tatizo huwa linakuwa ni nini ni kutokusoma uzi husika au vp? Hili jambo huwa linanishangaza sana.Serikali kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) itaanza kununua shehena ya mafuta moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji wakubwa badala ya kununua mafuta hayo kwa watu wa kati ili kubidhiti mfumuko wa bei
Aidha serikali itaanzisha hifadhi ya kimkakati ya mafuta (Strategic Petroleum Reserve)ili kuwa na akiba kubwa ya mafuta wakati wote kwaajili ya dharura na pale bei itakapopanda kwa kiwango cha huu
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Arusha, Waziri wa Nishati, January Makamba alisema serikali iliiwezesha TPDC kushiriki zabuni ya kishindani na makampuni mengine ya kimataifa ambayo kila mwezi yanaleta mafuta nchini
Alisema TPDC imefanikiwa kushinda sehemu kubwa ya zabuni hiyo kwa kutoa bei ndogo zaidi ya kuagiza mafuta ya dizeli nchini kwa mwezi Desemba mwaka huu
Alisema katika kudhihirisha hatua hiyo kuwa ya manufaa mwezi Agosti 2021,wakati bei ya mafuta ghafi duniani ilikuwa dola 73 kwa pipa, kampuni iliyoshinda zabuni ya kuleta mafuta ya dizeli nchini iliuza kwa dola 30 kwa tani za ujazo (premium).
Alisema safari hii licha ya bei ya mafuta ghafi kupanda duniani na kufikia dola 86 kwa pipa,TPDC italeta dizeli nchini Desemba mwaka huu kwa wastani wa dola 20 kwa tani za ujazo
Alisema pia katika ziara yake aliyoifanya nchi zinazouza mafuta akiwa na watendaji wengine wamefanikiwa kushawisho nchi rafiki kujenga kituo kikubwa cha upokeaji na uhifadhi mkubwa wa mafuta(fuel terminal) kwaajili ya soko la ndani ya nchi lakini kwa mahitaji ya nchi za Afrika Mashariki na Kati na nyinginezo za mbali pale itakapohitajika
"lengo la serikali kununua mafuta moja kwa moja kwa wauzaji wakubwa ni kudhibiti upandaji wa mafuta hivyo kupitia Shirika la TPDC tutaanza kununua mafuta hayo kwa wauzaji wakubwa na si wakati"
Alisema iwapo kutatokea dharura huko Duniani na kushindwa kuagiza mafuta kiasi cha mafuta yaliyopo nchini yanatosheleza kwa wastani wa siku 15 tu
Alisema katika hatua ya muda mfupi kuiimarisha TPDC kwakuruhusu haraka kuajiri watumishi weledi na wajuzi wa biashara wa biashara ya mafuta ili iendelee kununua mafuta kwaniaba ya serikali kwa ufanisi zaidi
Pia kupitia mfumo wa uagizaji wa mafuta wa pamoja(bulk Procurement Reserve)ili kubaini mapungufu na kuboresha kwa kiwango kikubwa ikiwemo kufanya tathimini ya utendaji na watumishi wa taasisi zote za serikali zinazohusika na biashara ya mafuta ikiwemo TPDC,EWURA na Wakala wa Uagizaji wa Mafuta wa Pamoja(PBPA) ili kuhakikisha kuwa taasisi hizo na watumishi wake wanatimiza wajibu wao kwa weledi
Alisema katika kuendelea na utekelezaji wa maelekezo ya Rais Samia Hassan Suluhu ni kuendelea kupitia tozo na kodi mbalimbali zinazochangia kuongezeka kwa bei ya mafuta nchini pia serikali itaendelea kuweka mazingira mazuri ya kibiashara na sekta binafsi ili kuwe na ushindani wa haki na uwazi kwa !anufaa ya watumiaji mafuta nchini
Alisisitiza serikali itaongeza ufuatiliaji wa karibu zaidi kwenye sekta ya mafuta kwakutumia vyombo na mamlaka mbalimbali ili kubaini na kudhibiti hujuma na udanganyifu katika biashara ya mafuta ikiwemo uwekaji wa adhabu kali zaidi ikiwemo kunyang'anywa leseni pale itakabyobainija hivyo
Alisema pia serikali itaboresha miundombinu ya upokeaji na uhifadhi wa mafuta nchini hasa katika bandari ili kuhakikisha kunaufanisi zaidi ikiwemo kufanyia kazi mapemdekezo ya tume iliyoundwa na Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa kuhusu biashara ya mafuta nchini
Hata hivyo Makamba alisisitiza kuwa bei ya mafuta nchini kwakiasi kikubw inachangiwa na bei a mafuta n
Duniani ambazo serikali inanafasi ndogo kwenye kudhibiti hata hivyo serikali itaendelea kuchukua hatua mbalimbali ili kuhakikisha yaliyoko ndani ya uwezo wa serikali katika kudhibiti bei ya mafuta yanafanyiwa Kazi
View attachment 1993633
Ila Binadamu bwanaaa, sasa wewe unatakaje? Ulitaka aukatae uwaziri au alipoingia wizarani atulie tuu na kula mshahara?Siasa tu hizi....kama ingewezekana JPM asingeacha kutekeleza hili kwa sababu alikuwaga na bifu na madalali. Sasa Makamba marafiki zake na mabosi wake wa zamani ndo wenye filling stations ataanzia wapi kuwageuka?
Hahahahaha.......umeuliza kwa uchungu sana chifu!Ila Binadamu bwanaaa, sasa wewe unatakaje? Ulitaka aukatae uwaziri au alipoingia wizarani atulie tuu na kula mshahara?
Nadhani mambo ya tankers za mafuta kwa nchi kubwa kama Tanzania yamepitwa na wakati na ni uharibifu wa barabara na kuongeza conjestion barabarani. Hivi kweli tunashindwaje kujenga bomba la mafuta from Dar Port, Mtwara Port na Tanga Port kwenda mikoani?? Mfano bomba to Morogoro, Dodoma mpaka Mwanza? Pale Chalinze kuna kuwa na branches kwenda Iringa mpaka Mbeya na lingine Tanga mpaka Manyara? Tungelianza hili kama lile la TAZAMA 30 yrs back je mpaka sasa si tungeshamaliza??

Kaja na bomu. Bei za mafuta zitapaa kwa kuwa bidhaa hiyo itaadimika - "supply chain monopoly in offing".Kaja na begi la umeme tuende kumpokea au
Ukiona kimya jua kesi imeshaisha
TAARIFA KWA UMMA KUTOKA WIZARA YA NISHATI KUHUSU ZIARA YA WAZIRI JANUARY MAKAMBA
Kama inavyofahamika, bei ya mafuta ghafi duniani imeendelea kupanda kwa kasi na kwa kiwango kikubwa, kutoka dola 50 kwa pipa mwezi wa Januari mwaka huu hadi dola 86 kwa pipa leo tarehe 31 Oktoba 2021.
Hali hii inapelekea bei kupanda kwenye vituo vya kuuzia mafuta na mitaani hapa nchini.
Kama itakavyokumbukwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, alielekeza hatua mbalimbali za kikodi, kisheria/kanuni na kiutawala ili kupunguza makali na athari za ongezeko hili la bei. Wizara ya Nishati imeanza kutekeleza maelekezo hayo na pia kuratibu hatua mbalimbali za Wizara na taasisi nyingine za umma na kufanikiwa kupunguza ongezeko kubwa la bei ya mafuta kwa mwezi wa Oktoba.
Katika kutimiza azma ya Mheshimiwa Rais ya kuhakikisha kwamba bei za mafuta haziumizi wananchi, na shughuli za uchumi haziathiriki, Wizara ya Nishati ilichunguza na kubaini uwezekano wa unafuu wa bei iwapo Serikali yenyewe itanunua mafuta moja kwa moja kutoka kwenye mitambo ya kusafisha mafuta (refineries) ya nchi rafiki badala ya kuachia watu wa katikati (intermediaries) kununua kwa nchi hizo hizo rafiki zetu na kutuuzia kwa bei kubwa.
Kutokana na hilo, katika duru la kwanza, kuanzia tarehe 22 hadi 29 Oktoba 2021 nilifanya ziara katika nchi tatu – Saudi Arabia, Umoja wa Falme za Kiarabu na Algeria – ambazo zinazalisha mafuta kwa wingi na kuuza kote duniani. Katika nchi hizo, nilikutana na Mawaziri wenzangu wa Nishati, na viongozi wengine waandamizi wa Serikali na makampuni 2 ya mafuta ya Serikali za nchi hizo. Vilevile, nilibeba ujumbe maalum wa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa viongozi wa nchi hizo.
Katika ziara hiyo, niliongozana na Ndugu Michael Mjinja, Kamishna wa Petroli na Gesi katika Wizara ya Nishati na Ndugu James Mataragio, Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC. Pia, mabalozi wetu katika nchi hizo walishiriki katika vikao na mazungumzo niliyoyafanya.
Madhumuni ya ziara hiyo yalikuwa ni kama ifuatavyo:-
1. Kuzungumza na nchi rafiki zinazozalisha mafuta ili kuangalia uwezekano wa Serikali, kupitia Shirika la Mafuta Tanzania (TPDC), kununua mafuta moja kwa moja kwenye mitambo yao ya kuzalisha mafuta (refineries) na hivyo kupunguza gharama zinazowekwa na wanunuzi wa kati.
2. Kubadilishana uzoefu na nchi hizi rafiki kuhusu uendeshaji wa sekta ya mafuta na gesi.
3. Kuimarisha mahusiano yaliyopo na kujenga ushirikiano mpya katika eneo la mafuta ili nchi yetu ipate jawabu la kudumu la kujihakikishia upatikanaji wa uhakika wa mafuta na kwa bei isiyopanda ghafla na kwa kiwango kikubwa.
Katika nchi zote hizo tatu, nilifanikiwa kukutana na kufanya mazungumzo na Mawaziri wenzangu wa Nishati, viongozi wengine waandamizi na wakuu wa mashirika ya mafuta ya taifa ya nchi hizo.
Kutokana na heshima ya nchi yetu na Rais wetu, na urafiki wa nchi yetu na nchi hizi, nilipokelewa vizuri na viongozi wote katika nchi zote hizi na walipokea na kukubali hoja na haja ya mashirikiano katika sekta hii ya mafuta. Kwa kifupi, yale yote ambayo nchi yetu iliyapendekeza kwenye nchi hizi yamekubalika.
Baadhi ya mafanikio ya ziara hiyo ni kama ifuatavyo:
1. Serikali yetu imekubaliana na Serikali za nchi hizo na makampuni yao ya Taifa ya mafuta kushirikiana katika masuala ya mafuta na gesi. Katika miezi ijayo, baada ya taratibu za kiserikali na kisheria kukamilika, makubaliano hayo yenye maslahi kwa nchi yetu yatatangazwa.
2. Kwa mara ya kwanza, ile azma ya miaka mingi ya Serikali, kununua shehena ya mafuta moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji sasa imetimia. Hata kabla ya mwisho wa safari yetu, mnamo tarehe 28 Oktoba 2021, tuliiwezesha TPDC kushiriki zabuni ya kiushindani na makampuni mengine ya kimataifa ambayo kila mwezi hushiriki zabuni ya kuleta mafuta nchini. TPDC imefanikiwa kushinda sehemu kubwa ya zabuni hiyo kwa kutoa bei ndogo zaidi ya kuagiza mafuta ya dizeli nchini kwa mwezi wa Disemba mwaka huu. Hali hii itapunguza makali ya bei ya mafuta ya dizeli kwa mwezi Disemba. Kudhihirisha kwamba hatua hii ina manufaa, kwa mfano, mwezi Agosti 2021, wakati bei ya mafuta ghafi duniani ilikuwa dola 73 kwa pipa, kampuni iliyoshinda zabuni ya kuleta mafuta ya dizeli nchini ilituuzia kwa dola 30 kwa tani za ujazo (premium). Safari hii, pamoja na bei ya mafuta ghafi duniani kupanda na kufikia dola 86 kwa pipa, TPDC italeta dizeli nchini mwezi Disemba kwa wastani wa dola 20 kwa tani za ujazo.
3. Tumefanikiwa kushawishi nchi rafiki tulizotembelea kushirikiana na nchi yetu kujenga kituo kikubwa cha upokeaji na uhifadhi mkubwa wa mafuta (fuel terminal) kwa ajili ya soko la ndani ya nchi yetu lakini kwa mahitaji ya nchi za Afrika Mashariki na Kati na nyingine za mbali pale itakapohitajika. Kituo hiki kitatuhakikishia kuwa na kiasi cha kutosha cha mafuta ndani ya nchi wakati wote. Kwa sasa, iwapo kutatokea dharura huko duniani na tukashindwa kuagiza mafuta, kiasi cha mafuta yaliyopo nchini yanatutosheleza kwa wastani wa siku 15 tu. Mazungumzo kuhusu taratibu za kuanzisha kituo hiki yataanza mwezi wa Novemba.
4. Baada ya wiki mbili kuanzia sasa, kutakuwa na ziara za viongozi na watalaam kutoka katika nchi tulizotembelea kuja Tanzania kwa ajili ya kukamilisha taratibu za utekelezaji wa makubaliano yetu kwenye maeneo tuliyokubaliana kushirikiana. Wizara ya Nishati itaendelea kuratibu na kufuatilia ili kuhakikisha
kwamba mafanikio yaliyopatikana kwenye ziara hii yanadumu na makubaliano na nchi hizi rafiki yanatekelezwa kwa maslahi mapana ya nchi yetu na watu wake.
Wakati huo huo, katika kuendelea kurekebisha sekta ndogo ya mafuta, Serikali itatekeleza yafuatayo:-
1. Kama hatua ya muda mfupi, kuiimarisha TPDC kwa kuiruhusu haraka kuajiri watumishi weledi na wajuzi wa biashara ya mafuta ili iendelee kununua mafuta kwa niaba ya Serikali kwa ufanisi zaidi.
2. Kama hatua ya muda wa kati, lakini yenye jawabu la muda mrefu, Serikali itaanzisha Hifadhi ya Kimkakati ya Mafuta (Strategic Petroleum Reserve) ili kuwa na akiba kubwa ya mafuta wakati wote kwa ajili ya dharura na pale bei duniani itakapopanda kwa kiwango kikubwa.
3. Kupitia mfumo wa uagizaji wa mafuta wa pamoja (Bulk Procurement System) ili kubaini mapungufu na kuboresha kwa maslahi mapana ya Taifa.
4. Kufanya tathmini ya utendaji na watumishi wa taasisi zote za Serikali zinazohusika na biashara ya mafuta ikiwemo TPDC, EWURA na Wakala wa Uagizaji wa Mafuta wa Pamoja (PBPA) ili kuhakikisha kwamba taasisi hizi na watumishi wake wote wanatimiza wajibu wao kwa weledi na uadilifu na kwa maslahi ya nchi.
5. Kuendelea na utekelezaji wa maelekezo ya Mheshimiwa Rais ikiwemo kuendelea kupitia tozo na kodi mbalimbali zinazochangia kuongezeka kwa bei ya mafuta nchini.
6. Kuendelea kushirikiana kwa karibu na wadau wa biashara ya mafuta nchini, ikiwemo TAOMAC na TAPSOA, na kuweka mazingira mazuri ya biashara ya mafuta nchini kwa sekta binafsi kuendelea kushiriki ili kuwe na ushindani wa haki na wa uwazi kwa manufaa ya watumiaji mafuta na nchi kwa jumla. Serikali itaongeza ufuatiliaji wa karibu zaidi kwenye sekta ya mafuta kwa kutumia vyombo na mamlaka mbalimbali ili kubaini na kudhibiti hujuma na udanganyifu katika biashara ya mafuta na kuweka adhabu kali zaidi, ikiwemo kunyang’anywa leseni, pale itakapobainika hivyo.
7. Kurekebisha miundombinu ya upokeaji na uhifadhi wa mafuta nchini, hasa kwenye bandari zetu ili kuhakikisha kwamba kuna ufanisi zaidi.
8. Kuendelea kuyafanyia kazi na kutekeleza mapendekezo ya tume iliyoundwa na Mheshimiwa Waziri Mkuu kuhusu biashara ya mafuta nchini.
HITIMISHO
Bei ya mafuta nchini kwa kiasi kikubwa inachangiwa na bei za mafuta duniani, ambazo Serikali ina nafasi ndogo kwenye kuzidhibiti. Hata hivyo, Serikali itaendelea kuchukua hatua mbalimbali kuhakikisha kwamba yale yaliyo ndani ya uwezo wa Serikali katika kudhibiti bei ya mafuta tunayafanyia kazi.
January Makamba (Mb.)
Waziri wa Nishati
31 Oktoba EWURA: Taarifa kwa umma kuhusu bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli kuanzia 1 Desemba 2021
All these looks very fine. Swali langu dogo la kueleweshwa ! Miaka ya nyuma kidogo tualiambiwa kitu kinachoitwa bulk purchase ya mafuta huo utaratibu unasaidiaje changamoto ya bei kwa sasa kwa soko la mafuta duniani? Pia tofauti ya hiyo bulk purchase na hiki anachotuambia MH. Waziri ni nini?TAARIFA KWA UMMA KUTOKA WIZARA YA NISHATI KUHUSU ZIARA YA WAZIRI JANUARY MAKAMBA

31 Oktoba 2021
View attachment 1993488
Makamba akikuambia nje kuna giza toka ukajiridhishe kama Kweli kuna gizaAll these looks very fine. Swali langu dogo la kueleweshwa ! Miaka ya nyuma kidogo tualiambiwa kitu kinachoitwa bulk purchase ya mafuta huo utaratibu unasaidiaje changamoto ya bei kwa sasa kwa soko la mafuta duniani? Pia tofauti ya hiyo bulk purchase na hiki anachotuambia MH. Waziri ni nini?
Bomu limelipukaKaja na bomu. Bei za mafuta zitapaa kwa kuwa bidhaa hiyo itaadimika - "supply chain monopoly in offing".
Desemba imefika, walisema yatashuka Ila ndio kwanza yamepandaMuda ndio msema kweli.