Waziri Makamba: Sasa Serikali itanunua shehena ya mafuta moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji

Habari nzuri sana hii.Huu ndio ubunifu.Huyu Waziri wetu,ni mchapakazi na mbunifu.
Tayari, kilaza m'moja kashalewa anaanza kumwaga sifa. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Aiseeeeeee ndio maana CCM imetoboa miaka 60.
 
Mheshimiwa waziri kwa hili la kuondoa mtu kati kwenye uagizaji wa mafuta ukifanikiwa utakuwa umewasaidia sana watanzania. Mungu akusaidie maana najua mpambano wake si wa kitoto.
Hivi katika akili ya kawaida tu na nyepesi, hao waliotangulia wote hawakuona hiyo solution?!

Hapa kuna mchezo tunachezewa mchana kweupe. Ni swala la muda tu tutajua shida imejificha wapi.
 
Usisahau kuwa nyie ndio wamiliki wa makampuni makubwa ya mafuta na mnalinda maslahi yenu
Hii ni changa la macho. Hivi kimsingi eti ni kwamba eti jamaa hawa wachuuzi wa mafuta wafutwe kishkaji tu wawe wapole ili serikali iagize yenyewe.

Magufuli alishindwa kufanya hilo swala na vile alivyokuwa anapenda kuwakomoa hawa madalali wa soko huria.

Kuna kitu kitakwenda kufanyika, ukweli utakuja kujulikana na watu hawataamini namna tutakavyokuwa tumepigwa.

Ogopa sana mtu anaefosi kuonekana ni smart na brain kali above all. Na mbaya zaidi awe na tamaa ya uraisi huku anapretend hana shida nao.

Its just a matter of time. True colors will show.
 
Me too. This guy is very fishy and creepy in a political way.
 

Tatizo kubwa la bei ya mafuta nchini ni kodi na tozo mbalimbali.

Kwani hata tozo za stika za usalama barabarani nazo kama yalivyo mafaini yasiyokuwa na kichwa wala miguu barabarani si nayo ni gharama na kero zaidi kwa wenye magari?
 
Mtu anachungulia 2030 Kwa uchu jalafu unampa dili la kunegotiate si ndo Yale ya pesa za gadaffi
 
MI NAFIKIRI TURUHUSIWE KUAGIZA MAFUTA KILA MTU KAMA AMBAVYO TUNAAGIZA BIDHAA NYINGINE.MFANO UNAAGIZA ZAKO TANI 100,UNATUMIA ZIKIISHA UNAAGIZA TENA ARABUNI
 
Hivi katika akili ya kawaida tu na nyepesi, hao waliotangulia wote hawakuona hiyo solution?!

Hapa kuna mchezo tunachezewa mchana kweupe. Ni swala la muda tu tutajua shida imejificha wapi.
Nguvu ya pesa baba. Hata hii Januari ajipange sana
 
Siasa tu hizi....kama ingewezekana JPM asingeacha kutekeleza hili kwa sababu alikuwaga na bifu na madalali. Sasa Makamba marafiki zake na mabosi wake wa zamani ndo wenye filling stations ataanzia wapi kuwageuka?
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] hili nalo ni neno tena zito sana. Nimewaambia haya maneno pia kuwa magu hii kitu angeweza ifanya overnight kama ingekuwa ni possible.
 
Kwanini Kabla hawakufanya hivyo ?

What are the Pros and Cons

Don't get me wrong binafsi nadhani this is the best solution..., ila nashangaa common sense haiku-prevail hapo kabla; cha muhimu tununue kabla ila sio exclusive deals hawa madalali kama wakija na bei ya chini basi tuchukue kwao pia
 
Bei ya mafuta inaongezwa na serikali yenyewe kwa kuongeza tozo na kodi kwa watoa huduma na pia tozo nyingi zaidi ya 21 kwa kila taasisi ya seriakli kwenye mafuta.... hizo tozo zikiondolewa hata wasinge agiza wenyewe bado mafuta yatashuka.....

Uzuri bei ya mafuta duniani iko wazi kabisa na mafuta yasingepanda kama serikali isingeliongeza mzigo wa kodi na pia kama kweli serikali inataka kushusha bei ya mafuta iondoe hizo tozo zaidi ya 21 kwenye mafuta .....

Mafuta hata wakiacha hao hao wanao agiza waagize bado mafuta yanweza kushuka kama wataondoa mlolongo wa kodi......kuwepo na dhamira ya kweli ya kushusha bei ya mafuta kwa kuanza kuondoa makodi na matozo story za kuagiza wenyewe.

Serikali isijiingize kwenye biashara halafu baadae tuje tuambiwe story nyingine... oooh mafuta yamepanda tulipokuwa tuna nunua oooh sijui nini oooh bei itaongezeka kidogo
 
Kumtoa mtu wa kati iyo ni vita kubwa sana
 
Hahahahaha... .lakini ndiye aliyelazimisha TPDC kujenga filling stations kila mji ili baadaye ifanye biashara ya mafuta kwa niaba ya Serikali. Au umesahau?
Mnafiki huwa anajisahau kwasababu ili uwe muongo miaka yote inabidi uwe na kumbukumbu balaa jambo ambalo ni gumu sana.
 
Madalali uchwara ndio tatizo la hii inchi kusababisha mifumuko ya bei. Tutokomeze madalali uchwara tutasolve hii kitu.
 
Hakujawahi kuanzishwa kitu Tanzania halafu kikawa na muendelezo wenye tija.Tutakuja kusikia 'tunapigwa' tena kwenye hili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…