Waziri Makamba: Sasa Serikali itanunua shehena ya mafuta moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji

Porojo tu hamna la maana hapo!
Tumpe muda, hicho alichokisema kama kitafanyika kutakuwa na ahueni. Sema pamoja na yote hayo wafute yale makodi kibao ya mafuta ili na sisi bei iwe ndogo kama wenzetu wa Zambia.
 
Tunapata shida sana kumuamini waziri wa madini kwani historia haimbebi kama mtendaji mzuri asiye na makandokando.

Na suala la yeye kuwa karibu na marehemu Ruge linafanya image yake ni mtu wa kujibrand tuu.
Sema 'ninapata shida sana..' achana kabisa na hii ya kusema 'tunapata shida..'..
 
Mheshimiwa waziri kwa hili la kuondoa mtu kati kwenye uagizaji wa mafuta ukifanikiwa utakuwa umewasaidia sana watanzania. Mungu akusaidie maana najua mpambano wake si wa kitoto.
Mkuu hili pekee linaweza lisiwe na impact kubwa kama hawataondoa ule utitiri wa kodi kwenye kila lita moja ya mafuta inayoingia nchini. Wewe hushangai Zambia mafuta yao yanapitia bandarini kwetu na sote tunanunua pamoja huko duniani lakini pale Tunduma ukivuka na kuingia Zambia tofauti ya bei ya mafuta kwa lita ni zaidi ya 700/= juu kwa huku kwetu wakati Zambia ni chini.
 
Nadhani mambo ya tankers za mafuta kwa nchi kubwa kama Tanzania yamepitwa na wakati na ni uharibifu wa barabara na kuongeza conjestion barabarani. Hivi kweli tunashindwaje kujenga bomba la mafuta from Dar Port, Mtwara Port na Tanga Port kwenda mikoani?? Mfano bomba to Morogoro, Dodoma mpaka Mwanza? Pale Chalinze kuna kuwa na branches kwenda Iringa mpaka Mbeya na lingine Tanga mpaka Manyara? Tungelianza hili kama lile la TAZAMA 30 yrs back je mpaka sasa si tungeshamaliza??
 
Kwa hiyo ndiyo yatashuka au??
Kwa ule utitiri wa zile kodi kwenye mafuta utashangaa imeshuka shilingi tano mkuu note my word... Yaani hapa zile kodi kwa maoni yangu zinachukua 60% na hawa waagizaji na watu wao wa kati ni 40%
 
Kwa nini unapost uzi ule ule? Hivi tatizo huwa linakuwa ni nini ni kutokusoma uzi husika au vp? Hili jambo huwa linanishangaza sana.
 
Siasa tu hizi....kama ingewezekana JPM asingeacha kutekeleza hili kwa sababu alikuwaga na bifu na madalali. Sasa Makamba marafiki zake na mabosi wake wa zamani ndo wenye filling stations ataanzia wapi kuwageuka?
Ila Binadamu bwanaaa, sasa wewe unatakaje? Ulitaka aukatae uwaziri au alipoingia wizarani atulie tuu na kula mshahara?
 

sorry namaanisha tankers ( meli za mafuta)
point yangu sio tanker magari ya mafuta hapana, nilikuwa namaanisha tankers ( meli za mafuta) owned by GOT....

Kujenga hizo pipe lines ni gharama kuubwa sana, bado tungeamua kutumia bandari moja say Tanga port na kuwe na storages kubwa pale... kuwe na rail line itakayoconnect kanda zote...kwa maana ya North, lake zone nk ambazo tayari tunazo ni repair ndogo tu....wale wa kusini mtwara, lindi, Songea na Mbeya...baada ya meli kuoffload pale Tanga, meli ndogo itapeleka Mtwara na rail line itawapelekea huko...

La msingi lingine la kuanza nalo mapema ni kuondoa tozo zote kwenye mafuta kama pilot na kuona mafuta yatakuwa bei gani yalishuka..
 
You can’t fault people for trying.

Uzuri ni kwamba wamebaini inventory ya mafuta kwa siku 15 ni National security risk, wanahitaji more storage.

Tatizo ni kwamba serikali inataka kujipa monopoly ya kununua mafuta sourced from one region. Sasa wakianza kutandikana M.E au Iran akipiga mkwara si kasheshe kwetu.

This is why hakuna nchi makini duniani inaagiza nishati yake kutoka eneo moja tu, sehemu moja ikileta shida, bado una source zingine za kupata nishati.
 
Kweli nimeamini serikali ya awamu ya tano ilikuwa ya majungu wivu na chuki binafsi maana hata Leo hii magufuli angelikuwa hai ningelimuuliza kwanini akili kubwa kama hii ya huyu kijana makamba kwa nini ulimtoa wizarani jibu asingelipata angebaki na kigugumizi tu
 
 
All these looks very fine. Swali langu dogo la kueleweshwa ! Miaka ya nyuma kidogo tualiambiwa kitu kinachoitwa bulk purchase ya mafuta huo utaratibu unasaidiaje changamoto ya bei kwa sasa kwa soko la mafuta duniani? Pia tofauti ya hiyo bulk purchase na hiki anachotuambia MH. Waziri ni nini?
 
Makamba akikuambia nje kuna giza toka ukajiridhishe kama Kweli kuna giza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…