Waziri Makamba: Sasa Serikali itanunua shehena ya mafuta moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji

Nchi inapigwa bila huruma, hawa watu hawana nia ya kusaidia ile nchi iendelee na wako pale kupiga tuu au ni vilaza kweli kweli hawajui cha kufanya na hawana idea nini cha kufanya nchi iende mbele, karne hii huna maji wala umeme ni mambo ya ajabu sana na watanzania wasikubali huo upuuzi
 
Habari nzuri sana hii.Huu ndio ubunifu.Huyu Waziri wetu,ni mchapakazi na mbunifu.
Hapo mwisho kwa kiasi katudanganya.Mafuta nchini bei inakuwa kubwa kwa sababu ya makodi lukuki wanayoyaweka.Hili kamezea.Alitakiwa aliseme kwa uwazi,Makodi hayo yasiyokuwa ya lazima ambapo hayo hayo pia yapo Tanesco,Hayo yangeondolewa au yakafutwa kabisa Mtanzania angalau angepumua.

Ni jambo la kusikitisha sana kuona matumizi mabaya sana ya magari ya serikali.Naomba ieleweke kwamba hizi ni kodi za wananchi, zitumieni mkijua kuwa mtanzania huyu aliyekatwa kodi kwenye kila biashara, ndiye huyu huyu mtoto wake anakwenda shuleni anaandikia mapajani akiwa amekaa chini.

Lakini wakati huohuo,viongozi wanakuwa na msururu mrefu wa mav8 wakiunguza fedha za Mtanzania wa chini ambaye anashindwa kulipa ankara ya maji.Na sasa wametengeneza tena utaratibu wa kuzila kwa kuanza makongamano na masemina elekezi kila mahali na mengi sana yanafanyika Arusha.Nadhani unajua ni kwa nini yanafanyika Arusha na kila ofisa au ofisi wamekuja na magari ya Serikali.

Mwoneeni huruma huyu mtanzania.
 
Why government shouldn't hedge oil to protect this changes
Hahaha not sure hata kama wana idea na hedging...lakini to be fair sio wao wanaonunua, walishatoa vibali vya 10% kwa mabilionea wa kihindi, na kinachofuata hakiwahusu
 
Uzuri ni kwamba they understand the ned to increase storage capacity.

But when it comes to price stabilization kuongelea ni kupoteza muda kwa nchi ambayo procurement tender inafanyika monthly.

Maan hapo kuanza kuelea how business relationship trust evolve between a supplier and customers its a different story nje ya Tanzania (trust me) na huu utaratibu wetu wa sasa wa monthly procurement tenders sio kampuni nyingi zinaweza kuingia mkataba wa muda mrefu na suppliers wa kununua mafuta kwa muda mrefu kwa bei ya kupanga kukwepa future price increase.

Nyie watu mnahitaji diaspora wa maana sio wale wenye makelele ya ovyo na January hii wizara sio size yake kwa watu wanaoijua.

It’s only easier if you know it.
 
Lini kitafufuliwa kiwanda cha TIPER walau tusafishe mafuta ghafi ili by products zingine tuzipate tupunguze tatizo la ajira na bidhaa za petrolleum zishuke bei. Lini tutaanza na sisi kuvuna mafuta tulionayo kwa maslahi ya woote na sio wachache kama tunavyoona huko kwenye baadhi ya nchi za wavaa kobazi
 
You need people who understand how to strategies those business approaches first in order to make profit; maelezo yako yapo to generic and blameworthy without merit.

Na wapo humu JF watu wenye uwezo huo. Tatizo lenu watu wanatumia miakili yao kuelezea swala technically wakaonekana ovyo tu; halafu jitu jinga likaandika upumbavu mtupu mkalipa likes 100 what the fu*k.
 
Bado naamini Makamba despite his rubbish ni kiongozi mzuri.

☝️Why so, he’s open minded na mtu wa kujifunza; consequently along the way he would make mistakes. Nonetheless he takes criticism abroad. You only neet to look at his body language kwenye ziara ya kukagua maji wakati mkurugenzi wa TANESCO anaongea; silently he was saying I made a mistake with this idiot.
 
Hongera kwa Waziri Makamba. So far ni jitihada nzuri sana kama zitashusha bei ya mafuta maana hali si hali.

Watu wanaobeza nashindwa kuwaelewa kwenye hili.
Haya leo ni miezi 6 imepita, Bei imeshuka?
 
Miezi 6 Sasa, hakuna Bei iliposhuka
 
Jamani, binafsi namuelewa sana huyu broo japo sijawahai hata kutana naye.
Ngoja niombe kuhamia wizarsni kwake nimsaidie utendaji ktk senior post.
Una chombo chochote kinachotumia hayo mafuta anayozungumza Mhe Waziri?
 
Ifufueni TIPA ( kiwanda cha kusafisha mafuta) au anzisheni chengine . Kuna faida tele
1: ajira Kwa watu .
2:kununua mafuta ghafi , petrol, dizel , lami n.k (rahisi kwetu)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…