So what are actual elements of negotiations based on that info:
Mfano what clause will be used in the contract to mitigate political risks na wewe kama nchi unajilinda vipi?
Na kuna aina ngapi za mikataba unayoijua wewe kwenye oil and gas.
Elements of negotiations nilishakueleza kwenye post niliyokutumia hapo juu.
Wakati wa negotiations vitu vingi muhimu huangaliwa,
Kuna mambo ya muundo wa mkataba (contract structure); standard za uhasibu; mchango wa mwekezaji kwenye miradi ya kijamii kama shule, hospital, maji, barababara; Afya na mazingira; stabilization clauses; vifungu vya kumaliza mkataba (termination).
Kuhusu clause hapa huwa tunatumia "stability clauses" vifungu hivi husaidia kupunguza risk za kisiasa endapo kama uongozi ukibadilishwa au kama mihimili ya serikali ikaamua kubadili sheria au regulatory matters zikaamua kubadili baadhi ya sheria.
Stability clause husaidia mwekezaji afanye kazi katika mazingira yenye stable rule of law hata kama mazingira ya uongozi sio stable. Kwa kifupi hata kama inchi inaweza kuwa na kelele za kisiasa kifungu cha stability clause huendelea kumlinda mwekezaji.
Na kifungu hicho huitaka serikali kuilipa kampuni fidia kama kutatokea mabadiliko yeyote ya sheria za taifa, au vidhibiti au utawala unao athiri kampuni au uendeshaji au biashara ya kampuni.
Mfano serikali ikaamua kuunda sheria mpya ya mazingira ambayo kwa namna moja ama nyingine ikaonekana kuibana kampuni kwa kuongeza gharama za kampuni, kifungu cha stability clause kitaruhusu kampuni kutoifuata hiyo sheria au kuiamuru serikali ilipe kampuni fidia kwa gharama itakazo ingia endapo ikiifuata hiyo sheria mpya.
Kwa kuongezea stability clause ndio yenye uwezo wa Kufreeze bunge na serikali au vidhibiti vingine vinavyotunga sheria mpya.
Stability clause ndio hutumika kama kinga ya kampuni hata mahakama hukosa nguvu. Mahakama zote za ndani ya nchi huwa disempowered kwenye mkataba wa gesi au mafuta na hicho kifungu cha STABILITY CLAUSE.
Kuhusu swala la mikataba bwana Kilatha, tuna aina tatu za mikataba.
1. License au Concession Agreement.
2. Production Sharing Agreement (PSA)
3. Joint Venture au Service Agreement
Kila mkataba hapo una faida na hasara zake. Siwezi kuelezea kwa kirefu sababu ya muda.
Kuhusu kujilinda
1. Serikali inatakiwa ichague team ya negotiaters wenye uelewa na mambo ya biashara ya mafuta na gesi na wenye uzoefu na sheria, mambo ya uhasibu, mazingira, na usimamizi wa mafuta.
2. Serikali lazima ihakikishe inatumia regulatory powers kwenye hiyo mikataba ili kulinda public interests zote za kimazingira, kibiashara, kodi n.k
3.Serikali pia lazima ihakikishe inatengeneza mazingira mazuri ya hali ya uwekezaji ili kuchochea ukuaji wa uchumi na ajira wakati inatengeneza sheria za uwekezaji na penalties kwaajili ya hizo kampuni za mafuta.
4. Au wakati mwingine serikali inaweza kutafuta wataalam wa kimataifa wa fedha na sheria watakaoishauri wakati wa mazungumzo na hizo kampuni kubwa.
5.Lakini pia moja ya uamuzi wa kwanza ambao serikali lazima iufanye ili kujilinda ni kuchagua aina nzuri ya mkataba. Kila mkataba una terms zake na una faida na hasara zake. Hivyo aina ya mkataba ambayo serikali itachagua itakua ni hatua ya kwanza kabisa ya kulinda public interest.
Naomba niishie hapa