Waziri Makamba ujue siyo kila kitu ni cha kubinafisisha

Tanesco ibinafsishwe haraka sana iwezekanavyo

Hata mfumo wa vyama vingi mlipoulizwa mwanzo mlikataa sababu hamuwezi kuona mbali
 
shida ni ccm
 
Te
Team Jiwe mnajulikana
 
Wapi alipotangaza anataka TANESCO ibinafsishwe? Au chuki zako tu.
Tafadhali ndugu mwananchi, ukijibiwa hilo suali na yeyote yule basi naomba uni-tag manake hili suala la kubinafsisha TANESCO nimelisikia sana safari hii hapa, nami nilipojaribu kuhoji ni lini hizi habari zimetangazwa, bado sijapata jibu!!
 
Watanzania ni watu wa ajabu sana

Hivi hapo wapo wanapiga majungu ili Makamba atimuliwe
Shida ya Makamba ni alivyojipozisheni,shida ndo inaanzia hapo,kakaa sehemu ya kurushiwa Mawe,Uraisi asahau
 
Reactions: Ame
Tukisema CCM imechoka na kuishiwa mbinu/ubunifu ktk kukuza uchumi watu wanatutukana.
Ccm haijachoka,Ila ni mapungufu na mikakati ya hovyo ya wachache wanayoibuni,ambayo huipa adha nchi,naungana na ww ktk hili kwanza Mambo ya kubinafsisha si ndo Yale ambayo yalimshinda hata hayati mkapa!?,kwani nchi inafeli wapi? na kwanini !?mpaka mtafute watu wa nje ndo Wawa endeshee mashirika yenu na taasisi zenu!? wakija wanakuja na mikakati yao kulingana na nn wanataka ku gain,ni ujinga kubinafsisha kila kitu ,kwann kusiwekwe mikakati madhubuti ya usimamiaji!?nn kinashndkana !!?au ndo kutafutiana ma-gap ya biashara na upigaji Kama zama zile!????huwa najiskia vibaya Sana kuona kiongozi anakimbilia agenda ya kubinafsisha huko ni kufeli kwa ubongo kufikili ,na kubuni!! Kama ni kuwataka watu wa nje kufanya biashara nchini hatukatai,Ila waje na vitu vipya ambavyo ndani ya nchi havipo na hatujawahi kuwanavyo ,mf.viwanda vya kutengeneza magari,vifaa tiba,viwanda vya kutengeneza mashine za kilimo/pembejeo,viwanda vya madawa ya binadamu ,n.k,sio hivi ambavyo tumevianzisha wenyewe kwa kuumiza akili kweli, kwa kujichangachanga na vikodi vyetu vya miamala ya sm na kadhalika ,halafu tunawakabidhi wengine waviendeshe ,upuuuz kabisa!!!!
 
Shida ya Makamba ni alivyojipozisheni,shida ndo inaanzia hapo,kakaa sehemu ya kurushiwa Mawe,Uraisi asahau
Bila shaka amewekwa na hajajiweka mwenyewe

Urais ni mapema sana kuuzungumzia kwa sasa na nina uhakika hawezi kuwa Makamba
 
Tulikuwa na fastjet hapa kila mtu aliweza kupanda ndege, mkawafanyia figisu figisu Sasa ni shida tupu

Serikali iwe bize kukusanya kodi na kusimamia ulinzi basi mengine waachie sekta binafsi
 
Umenena vyema mkuu
 
Enzi za Kikwete Tanesco nusura ibinafisishwe baada ya kuwa na madeni makubwa ya kulipia capacity charges kutoka kwenye generator za kampuni la symbion.
Sio kweli...

Mkapa ndie aliibinafsisha TANESCO na TRC, huku TANESCO akaiweka chini ya Management Contract ya NetGroup Solutions ya Makaburu, na TRC kwa RITE ya Wahindi.

Na hayo yalitokea hata kabla ya hao akina Symbion!

In short, umeleta mada ambayo wala huna facts zake, manake hata ukiulizwa ni lini January alisema anataka kubinafsisha TANESCO, sidhani kama utakuwa na jibu sahihi!!
 
Unabinafisaji uendeshaji maana mswahili hawezi akaendesha kitu kwa ufanisi na ishu ya security inabakia kwenye serikali kwa national security.
Check tu mfano Tazara wameshindwa japo market ni kubwa na ya uhakika.
Mfano wa Tazara sio kweli. Uliza kabla ya kupotosha wengine, kwa mfano, maamuzi ya uendeshaji wake yanafanyikaje ukizingatia ni mradi wa serikali mbili. Tukirejea kwa tanesco au mashirika mengine ya umma, yana mamlaka kiasi gani kufanya maamuzi kitaaluma bila kuingiliwa na wanasiasa. Yawezekana baadhi ya mashirika hayana uhuru huo kwa maana ya kila mara kukimbilia Wizarani kupata baraka wakati mwingine kutoka kwa maofisa wasiokiwa na taaluma/uzoefu stahiki.
 
Tafadhali ndugu mwananchi, ukijibiwa hilo suali na yeyote yule basi naomba uni-tag manake hili suala la kubinafsisha TANESCO nimelisikia sana safari hii hapa, nami nilipojaribu kuhoji ni lini hizi habari zimetangazwa, bado sijapata jibu!!
watu wanaleta stori za vijiweni hapa na kulazimisha sote tuziamini.
 
Hili suala la kubinafsisha umeme naona Kuna Roast arm, dowanzi na Zi mbioni.
Ona body ili uamini.
Tunarudi kulekule kibaya zaidi 2mbili na mzito wamezibwa midomo.
 
Kwani kunanini? Mbona nyuzi ximekuwa nyingi kwa Tanesco?View attachment 1972913
Haya mkamateni sasa na huyu maana wengine wasio na majina wakiwasilisha ujumbe wao kwa michoro vikaragosi mnawakamata.

Malkia sijui anafanya nini jikoni wakati juu ya meza vyombo vya kupakulia chakula vimewekwa tayari kupokea shibe ya watu paka shube linaibuka na kukaa juu yake likiwa limekataza misuli ya shingo na macho yameiva kwa kusubiri kuletewa msosi bila utaiva saa ngapi.
 
Kukusanya trillion 2 sio tafsiri ya kupata faida, wanaweza kukusanya trillion 2 na gharama za uendeshaji zikawa trillion 3

Hakuna waziri anaweza tu kuanzisha mchakato kubinafsisha shirika bila kuwa na technical facts za kwa nini atake kubinafsisha. Wala si personal idea inaweza kufanya maamuzi makubwa kama kubinafsisha tanesco
 
Watanzania hawatakubali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…